Msinunue Namba za magari badala ya Gari lenyewe

mm jamaa yangu kanunua gari Mark II Oktoba 2015 JK anamkabidhi JPM
namba alipewa DAB nyie mmekimbiza mpaka DGS?
Hii ni October 2014.

Mimi DFZ nina uhakika nayo, nipo na kadi naiangalia hapa,

Pia DAA Ilianza September 2014,
 
Kuna kitendo niliwah kuona kwa macho mteja anafanyiwa na mafundi...
Nasema hivii....fundi wa kibongo si ndugu yako....kua naye makini...
Kumkomoa Muuzaji unaenda na mshikaji wako kabisa ambaye Wala sio fundi akikonyezwa atakwambia,siku ya Pili unaenda na mshikaji mwingine,siku ya tatu na mshikaji mwingine siku ya nne unaenda na fundi.
 
Dar gari nyingi za zamani zimeshaliwa na chumvi huku chini. Sishauri saaana kununua namba A mazingira ya Dar, labda mikoa mingine isiyo na chumvi.
Inategemea tu na utunzaji wa mtu, kuna jamaa ana crest yenye namba A, lakini alivyoitunza kama imetoka japan jana, na yupo dar, watu wengi huwa wana ishangaa sana!!
 
Kumkomoa Muuzaji unaenda na mshikaji wako kabisa ambaye Wala sio fundi akikonyezwa atakwambia,siku ya Pili unaenda na mshikaji mwingine,siku ya tatu na mshikaji mwingine siku ya nne unaenda na fundi.
Hapo kama nimekuelewa hivi kwa hii technique yako
 
Kumkomoa Muuzaji unaenda na mshikaji wako kabisa ambaye Wala sio fundi akikonyezwa atakwambia,siku ya Pili unaenda na mshikaji mwingine,siku ya tatu na mshikaji mwingine siku ya nne unaenda na fundi.
hyo gari sku ya kwanza mpaka ya nne inakungoja ww tu??? na je ww huna kazi mpaka uwe na muda wa kwenda na kurudi daily?? mana sku nne tayar week ishakata hapo!!
 
Namba gani unayozungumzia ?Gari za beforward ziko numbered how??
yaani mtu anakwambia natafuta Clugger lakini NAMBA D, huyo mtu ananunua namba. Unampatia Clugger namba D ambayo tangi iingie Tanzania inabeba magazeti usiku saa nne kutoka Dar Kwenda Mbeya.

hiyo gari inakuwa imechoka kuliko Clugger ya Mdosi /Mhindi NAMBA B anaishi Upanga na kufanya kazi upanga, jioni anawasha gari kwenda kula Sharwama Kariakoo na kurudi nyumbani.

Gari ya mhindi mpaka ifike km 1000 za gari ya magazeti ni baada ya miaka 2. Nunua gari usinunue namba.
 
yaani mtu anakwambia natafuta Clugger lakini NAMBA D, huyo mtu ananunua namba. Unampatia Clugger namba D ambayo tangi iingie Tanzania inabeba magazeti usiku saa nne kutoka Dar Kwenda Mbeya...

Well, hii ni kwa watu wanaonunua magari third hand (and more??) kutoka kwa watu hapa nchini, ila kama unaagiza from Japan it doesnt apply.
 
Well, hii ni kwa watu wanaonunua magari third hand (and more??) kutoka kwa watu hapa nchini, ila kama unaagiza from Japan it doesnt apply.
Serikali ndiyo inaaagiza magari Japan kwa kuptia mawakala, wewe kaja-*** hugusi hizo. Lakini nikutoe tongotongo, toyota Tanzania wanaingiza gari "zero km"inawekwa namba, na inakaa yard zaidi ya miezi 6, kwahiyom inakuwa namba ya zamani lakini gari mpya, hata Yard za mtaani ndivyo.

Nunua gari achana na namba. Sawa na mwanaume anayechagua mke kwa kuangalia umri, tutakupa mtoto mdogo amber Rutyy ila kishaenda km 200000 wakati kuna wenye umri mkubwa kama Shose Sinare kitu kinasoma Zero kilometre.
 
Mkuu unavyosisitiza ninunue gari nisinunue namba sikuelewi aliekwambia mimi naangalia namba ni nani? Niko determined kuagiza gari used from Japan so habari za kuangalia namba mimi hazifanyi kazi kwangu.

My initial take nilikua sijaelewa kuna uhusiano kati ya beforwad na namba za usajili za hapa bongo as in beforward doesnt assign any number kwenye magari yao.
 
hyo gari sku ya kwanza mpaka ya nne inakungoja ww tu??? na je ww huna kazi mpaka uwe na muda wa kwenda na kurudi daily?? mana sku nne tayar week ishakata hapo!!
Gari huwa zinachukua hata wiki had mwezi mpaka ziuzwe haziuziki kirahisi mkuu
 
Watu ni kwamba hawaelewi Kuna gari namba A imenyooka kuanzia Engine hadi body...
 
Uko sahihi mkuu,nilienda moshi nikawa nashangaa gari rav 4 # ATR kama imetoka Japan Jana,Dar factor nyingi zinachangia gar kukongoroka haraka
Moshi namba A na B zipo nyingi sana na zimenyooka mno.
 
mm jamaa yangu kanunua gari Mark II Oktoba 2015 JK anamkabidhi JPM
namba alipewa DAB nyie mmekimbiza mpaka DGS?

Nahisi umekosea kumbu kumbu ama umedanganya hiyo namba na mwaka.. mimi nina passo niliagiza be foward.. nimeisajili nchini september 20 mwaka 2014 na namba nilipewa DBD... hapo DA zilikuwa zimeshaisha sababu boda boda nao walikuwa wanapewa D za mwanzo.. namba zao MC zilikuwa bado hazijaanza kutumika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…