Msinunue Namba za magari badala ya Gari lenyewe

Ndio maana mm huwa namwambia mnunuzi kabisaa kukukagulia gari ya mkononi/Showroom gharama zangu ni 50000 ili kukwepa izo tamaa sometimes ata muuzaji anaweza kukuambia pitisha gari kuna posho
 
Mafundi wa kuokota hao fundi wako unaemwamini hawezi kukufanyia kitu kama icho
Kwli kabisa mie kuna fundi wangu niliwahi mwambie nina milioni sita anitafutie IST ambayo iko vizuri, akaniambia ngumu sana kupata kwa hiyo bei. Na kweli ni ngumu kupata gari nzuri IST kwa bei hiyo. Sasa kuna siku nikakuta kuna gari IST inauzwa milioni tatu na nusu ila imechoka balaa. Yaani ile choka kweli kweli mpaka taa zimefungwa na kamba kioo full maufa.

Nikaicheki nikafanya nao mawasiliano na wakati wa kwenda kuiona nikamstua fundi wangu. Tukaenda tukaiangalia ile gari inakatisha tamaa ilikuwa ya mwela mmoja hivi alikuwa anaitumia pia anasanya kama Taxi mtaani bodi imegongwa gongwa balaa ila engine yake ilikuwa bado nzuri kabisa. Nikamwambia fundi hii inaweza kurudi kwenye mstari akaniambia ukiwa na milioni 3 inarudi kama mpya na ilikuwa namba CZ. Tuka bargain pale jamaa wakaniuzia kwa 3 milioni.

Tukaondoka nayo hivyo hivyo mpaka gereji kwa fundi wangu nikamwambia aniletee makadirio ambayo yalikuwa kama ifuatavyo

1. Kunyoosha bodi na kupiga rangi (niliibadilisha toka nyeupe kuwa ya Grey) 700,000/=
2. Mazaga zaga ya chini tyre rod end, mabush, shock ups bearing na mengineyo vilikula kama laki 700,000 na ufundi
3. Nikanunua tyres mpya zilinicost 380,000
4. Kioo cha mbele 110,000
5. Nilipeleka kuweka seat cover na kuiweka sawa ndani pamoja na taa za mbele ilikula 500,000/=
6. Radio 270,000
7. Speaker za mtumba (balaa sana) 120,000/=
8. Show ya mbele nilinunua mpya ilikuwa kama 150,000/-
9. Kuiosha na kuondoa takataka zote ndani ilikuwa kama 30,000/=
10. Mfumo wa AC kuubadilisha ilikuwa 430,000/=
11. Mengineyo 100,000/=
JUMLA YA VIFAA NA UFUNDI 3,490,000
Ununuzi 3,000,000
Jumla kuu 6,490,000/=

Gari ilirudi kwenye mstari balaa yaani kuliko hata ingetoka JAPAN na huu ni mwaka wa pili namwaga oil tu na matengenezo madogo madogo kutokana na njia zetu mbovu. Yule polisi alikuja kuiona siku moja hakuamini alichoona ni namba tu ndio yenyewe gari tofauti
 
Kweli kabisa juzi nimekutana na Land Cruiser namba A lilikuwa jipya kabisa sijui mmiliki amelitunza namna gani

Wengine kama gari kaipenda sana huwa wanabadilisha parts nyingi sana (exterior) hasa akiona kuiagiza kama hiyo itakuwa bei ghari. Banda lote la nje linapachikwa vifaa vipya ( vyaweza kuwa mtumba pia kama ilivyozoeleka) inarudi kuwa na mwonekano mpya japo Number Plate ni ya Zamani.
 
Kabla ya kutaka namba D angalia hyo namba ina muda gani mtaan mpaka sasa
 
Kwa kweli kwangu kununua gari namba A au B hata kama ingekuwa imenyooka vipi bado hujanishawishi.

Sinunui namba kwa maana hata hilo la D silibebi tu bila kuangalia factors zingine.

Kama naweza kupata A iliyonyooka means naweza pata D nzuri vilevile and I'll go for D.
 
Kabla ya kutaka namba D angalia hyo namba ina muda gani mtaan mpaka sasa
Kuna magari yanaingia Tanganyika toka Zanzibar yanasajiliwa T....DUA ilhali huko Zenji limeendeshwa toka 2014.

Ukiangalia mtaani kwa Tanganyika unapotea.
 
Why 3000km, weka oil ya 9000km
Aina gani ya oil?
 
Ukiwa dereva mzoefu huhitaji fundi, gari ukiendesha huwa linaongea hali yake lenyewe.
Mafundi ni mafisi tu

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Hahahah. Pole yake. Hizo shida za engine mm naweza kumrekebishia. Nampimia engine management sensors zote kama zinafanya kazi vile inavotakiwa
Mimi nina namba C na A
Lakini namba A ninamheshimu kuliko gari ya D.
Miaka 4 lkn sijawahi kufanya service kubwa zaidi ya kumwaga oil na kubadili tairi tena mara moja tu.
Ukinunua tairi mpya unajua unapiga muda wa kutosha.
Ninapasua tope, milima na mabonde A anacheka tu na hatujui kukwama ni msumari wa moto

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Inategemea na aina ya gari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…