Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hii imewahi nikuta mara 3.Sio kuhesabu tu hata kukuchomekea pesa bandia,nikiwa nasoma bibi alitoa 1.5M crdb kisha tukaenda deposit nmb na zile bank zinatizamana, kufika pale Mara tunaambiwa 20000 ni bandia tukachukua Ile pesa yote na kurudi pale crdb yule teller akasema yeye hajui,bibi akasema naomba nielekeze ofisi ya manager nikazunguze nae yule teller alitoka kule ndani faster na kuomba msamaha kwa bibi kisha akampa Ile alfu 20 tunaondoka
Hiyo michezo ipo sana hela iliyoko kwenye bundle iliyo salama ni zile bundle za bulk na zenye sealed tu. Hizi za milioni moja moja wewe mwambie teller atoe rubber band apitishe kwenye mashine ukijifanya wa kishua utapigwa kila siku.Hivi karibuni mara kadhaa ninavyokuwa napokea pesa nyingi kutoka Bank (zile ambazo sio sealed) nikifika ofisini nakuta kuna pisi zinakua zinapungua
Mwanzo nilikuwa nikipata changamoto hii kwenye bundles za 10,000 na 5,000 ila karibuni hata hizi za 2,000 na 1,000
Rai yangu kwenu mnaopokea pesa nyingi kutoka Bank muwabe Bank tellers zile pesa ambazo wamepanga kukulipeni wazifungue wazipitishe kwenye mashine huku mkiwa mnaziona kama vile ambavyo tunavyowapelekea pesa wanazifungua na kuzihesabu mbele yetu.