Msipokeshe pesa watu ovyo, wamekuwa wagumu sana kulipa madeni

Msipokeshe pesa watu ovyo, wamekuwa wagumu sana kulipa madeni

LICHADI

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2015
Posts
4,491
Reaction score
12,560
Kwenye jamii zetu kuna wale watu ambao kila siku wao ni kukopa tu yaani akikulipa leo anakutarget week or siku kadhaa anakukopa tena yani ni kama pesa yako ushammilikisha yeye so inakaa kwako kwa muda mfupi tu yeye ndio anatamba nayo na watu kama hawa mwisho wa siku huwa ni matapeli siku akishindwa kulipa ndio ntolee.

Wengine utakuta mpo ofisi moja na kipato ni kimoja lakini mwenzio yeye kila siku anakukopa tu hebu jiulize mshahara wake kama haumtoshi we wako ndio unatosha kukopesha watu?

Kukopesha ndugu au marafiki pesa kwa sasa imekuwa ikiua mahusiano ya ukaribu ya watu wengi sana, watu wamekuwa wakitumia ngao ya urafiki au undugu kulia shida ukishawasaidia wanakimbia na pesa zako

Kwa sasa kopesha mtu pesa ndefu for your own risk, ni heri uwe kama gaidi tu utoe jibu moja tu huna hela or mpe ila usimdai kuepusha lawama maana, hali ni tete now.

Kwa sasa ni heri mtu umshauri akakope kwenye taasisi or kama kaajiriwa akakope tu kazini, ukiona mtu mpaka kafika kwako ujue huko kote hakopesheki.
 
Naamini kuna laana kwenye mikopo maana mwingine unaona kabisa huyu hawezi kukosa hii hela ila anakuzungusha tu.
Mkuu sio laana binadamu hawana hofu ya Mungu, ukiona mtu anakopa ujue ana matatizo akilipa ujue anatarget aje kukopa tena, piga mahesabu mtu unamkopesha anajifanya kasahau kama sio kukosa hofu ya Mungu.

Nishapoteza marafiki na pesa ila pesa zimerudika katika njia sijatarajia bora wapotee kuna watu anakucheki asubuhi nikopeshe elfu 10 jioni nakulipa, ndo kibati hutomuona tena.

Mimi binafsi sijisifu ila kukopa siwezi hata miaka 10 iliyopita sijakopa nakumbuka siku moja nilienda na jamaa town kununua nguo pesa haikubalance kama elfu 5 mpesa sina kitu akasema mwenyewe nikupe utanilipa siku yeyote basi kesho yake nilimpigia simu alfajiri maana niliumwa aje chukua nyumbani mpaka jioni simuoni nampigia simu nina wasiwasi jamaa aniambia utanipa siku yeyote itabdi nimtume mtu ampelekee tu
 
Hatukopi sisi jamani ni Ugumu wa Maisha sasa siku hizi tukiomba pesa mnatuita Ombaomba!
Nb:Nikopeshe=Naomba,Wote waliwahi kuwa ndugu wakati wa Shida Mkumbuke Damu nzito.
 
Back
Top Bottom