Msipokeshe pesa watu ovyo, wamekuwa wagumu sana kulipa madeni

Hata kwenye taasisi za mikopo ni hivyo hivyo.
Tunapata shida sana.
 
Mkiniona namkopesha rafiki yeyote niueni...hata kama ni elfu 10
 
Kuna jamaa anamadeni kinoma siku moja akanichana kuwa yeye huwa halipi madeni anachofanya anahakikisha hela yako anakaa nayo miez Kama 8 hadi uwe mkali Hadi kichaa kitake kupanda alafu anachofanya hatoi hela yake mfukoni anaenda kukopa kwa mtu Mwingine ili akulipe
Anasema mdai wa zamani siku zote ndo anasumbua sana ila mdai mpya huwa hana nongwa.

Baada ya wiki akajisahau akaja kuniomba nimkopeshe.
 
Huwa mna mambo ya ajabu sana baadhi ya watu
Yaani umkopeshe hajui bank ilipo?
Haya ya kukopana ni kuongezeana umasikini tu
Mbona kwingine hamna mambo haya?
Kila mmoja ana maisha yake sasa inakuwaje mtu anakuja na kukuambia nikope Na wewe unampa duu
Mimi kama ni huko mtu ananiomba mkopo ntamwambia sitoi mikopo ila ntakusaidia elfu kadhaa bure zingine ukajaze unakojua maana wengine ni ving’ang’anizi sana
 
Binafsi huwa nakopesha watu pesa kwa Nia njema kabisa.

Lakini Mimi huwa nikikwama Hakuna my hata mmoja ananikopesha. Kila mtu Hana.

Ila ndio Maisha tuliyochagua.

Tumeshajenga taifa la JANJA JANJA NA KUTOAMINIANA.

Muhimu kama humsaidii mtu na wewe hakikisha huombi msaada kwa mtu.
 
Mwambiee ipo siku yake.....ata ipata dawa.
 
Umeongea ukweli mtupu👍
 
[emoji2][emoji2][emoji2]
 
Inaitwa jibebe wana tozo wajukuu wa tozo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…