Msisahau ku-update Android zenu kwenda Android 13

Sawa sawa
 
zinakaa chaji mzee.
 
N
imecheka kwa sauti
 

Mm natumia iOS 17 na mambo yapo safi Japo haikawa stable sana labda ikitoka public beta wataongeza na feature zingine
 
Kwenye Redmi Note 10 pro ilishakuwepo hata kabla ya update ya Android 13.
Hizi Redmi naona zinasifiwa sana ila Kuna mdau tunafanyag nae kazi sehem moja alinunua Redmi note 10 Yan simu ipo slow kweny ishu za network bado setting zake kama vile tofaut sana n wenzake.

Nikajaribu kukumbuka kabla ya kununua oppo A74 nilivokua na mzuka wa Redmi,
Baada ya kuuliza zaidi nikaambiwa Xiaomi ndo best phone kutoka kampuni hio inayotengeneza Xiaomi na Redmi

Sasa mm najiuliza Redmi mnazosifia zinatoka nchi gani au ndo hizi hizi ninazoziona...?? Ila mnajaribu zipa sifa zisizokua nazo..? Mana inawezekan zikawa na feature nzur na nying ila software ni hopeless.

Hapa nafifikiria kununua Xiaomi then hii nimwachie wife ila nikifikiria sifa za simu mnazotoa na wengine tunaziona kwa uhalisia napata kigugumizi.
 
Hata Redmi 9A ipo vizuri kwenye network, hiyo ya rafiki yako ilikuwa na matatizo labda
Xiaomi anatengeneza simu za bei rahisi, bei ya kati na bei ya juu pia. Usije ukanunua Redmi za laki 2 halafu utegemee eti iwe nzuri kama simu ya laki 5, hapana.

Kuhusu swali lako kuwa zinatoka nchi gani, jibu ni kwamba Xiaomi zinatoka nchini China lakini wanatengeneza simu kwa ajili ya regions tofauti tofauti
Mfano unaweza kukuta kuna Redmi Note 10 ya Indian version, Redmi Note 10 Chinese version, EU version na Global version

Hizi Indian version ni bei rahisi ila zinakuwaga na matatizo mengi ya hardware na hivyo ni vyema kuepuka kununua Xiaomi za Indian version ingawa sio zote ila Xiaomi nyingi zinazoleta matatizo ni hizi za India.

Lakini Xiaomi nyingi zinazokuja Bongo ni Global version na zenyewe ziko poa sana. Xiaomi ni simu nzuri na Redmi ni simu zao za bei rahisi mfano Redmi Note 10 Pro nk.
Most important thing, avoid Indian version
 
Hapa nimekupata... mana nilikua nishajipanga kumchukua Xiaomi mi 11 lite ila nikawa na hofu ila Sasa nirudishe nia.
 
Hakuna UI bora kwenye simu za Android kuliko One UI ya Samsung, hakuna.

Hizo oxygen os, sijui MIUI, color OS sijui nani hazimfikii Samsung.

Ile fluidity ya One UI, mpangilio wa apps, visual impression na mambo mengine mengi haina mfano.
Nina s10 nimeona niweke Microsoft luncher angalau appearance imevutia lakini ui as default ni mbaya. Wachina wamemzidi sana
 
Mkuu samahan naomba kufahamu KWA hio hizi simu za global version hazina shida maana naonaga unakuta hata iphone 15 ipooo global version bei chee (mitandaoni)

Changamoto zozote kuhusu hizi simu za global version naomba kufahamu??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…