Msisahau ku-update Android zenu kwenda Android 13

Msisahau ku-update Android zenu kwenda Android 13

Hakuna UI bora kwenye simu za Android kuliko One UI ya Samsung, hakuna.

Hizo oxygen os, sijui MIUI, color OS sijui nani hazimfikii Samsung.

Ile fluidity ya One UI, mpangilio wa apps, visual impression na mambo mengine mengi haina mfano.
Kwani pure Android ya Google Pixel na hiyo One UI ya Samsung ipi ni software bora[emoji23][emoji23]
Again inajulikana na ipo wazi kuwa One UI ni bora kuliko ColorOS, MIUI, Realme UI, etc. Lakini vipi kuhusu Stock Android[emoji41][emoji41]
 
Mi yangu kila siku inanipa notification ya ku update lakini naiogopa isije ikaleta maseke mana masimu yenyewe aya ya bei chee nshawai update moja bhana wee ikaanza chagua laini kumbe simu nlipigwa hilikua ya voda wajanja waliichezea ikawa inasomanlaini yeyote baada ya kupokea maboresho ikarudi vile ilivyopaswa kuwa nilimind sana
hii ilinikuta kwenye galaxy Note 5 enzi hizo, simu Duka la samsung ilikuwa kama 1.5M ila mie nikaipata mpya Makumbusho kwa 400K, ilikuwa poa sana kila kitu mpaka nilipoupdate.. mzigo ukawa hausomi line yeyote... Kumbe bwana ilikuwa simu ya USA-VERIZON... haisomi bands za Bongo.
Toka that day sitaki simu ya hela ndogo na pia lazima nifatilie kama custom ROM ya simu husika ni Global. Hii kitu ipo especially SAMSUNG.

Kwa wale ambao mnanunua simu zenu za samsung kkoo ama m/kumbusho chondechonde msiupdate hizo androids, mtakuja mlie na kusaga meno!
 
Imebidi niwe mpole baada ya kujaribu kudownload io update na nikapata hio error
Screenshot_20221114-060208_One%20UI%20Home.jpg
 
Hizo color sijui nini bado sana kwa One UI. Acheni kujifariji na simu za viwango vya kawaida.

Xiami, Oppo, Redme nk bado sana kumfikia Samsung. Samsung anawazidi kila kitu, kila kitu. Yuko mbali sana.

Ukipata hela kwenye Android nunua Samsung, ukikosa hela ukapata kidogo nunua hizo Xiaomi, Oppo nk na ukikosa hela kabisa nunua tecno.
hivi unazijua Huawei mkuu?
 
Aisee kama hiyo Samsung ni "budget phone" usijaribu kuiupdate. Ogopa sana.
One UI update ni nzito kwa budget phones kuhimili. Usije ukaja kutukana Samsung zote humu ndani
Nijibu bila kificho. KUANZIA IPHONE 12 KUENDELEA, sijawahi zishika nikazitumia zaidi ya kuziona kwa watu na hua sizichunguzi , je display yake ina quality nzuri kama ya samsung hizi s series mie now nina s9 ila quality ni nyoko . Hoja ya pili kwa samsung s9 setting ipi inaifanya simu iruhusu asilimia za mwanga kutokana na mtumiaji ulipo ( brightness setting kua automatic) .
 
1. Split Screen.
2. Float Screen.
3. Guest Account (unakuwa na accounts kibao ndani ya simu na zinajitegemea)
4. Touching gestures za kutosha with the screen off
Na vitu vingine viingi ambavyo kwenye Samsung sikuviona.
Nimetumia Samsung S10+ na ndio nikahamia Oppo
Mbona hizo feature zpo samsung kitambo,nliwahi tumia A10 nkakuta,sjui kwa sasa
 
Mhhhhh, mkuu nina mashaka na unachokisema.

Mwaka 2019/20 nilikua natumia S10+ na function ya Mult window ama split screen ilikuwepo wewe unasema hukuiona?

Umenipa mashaka na maelezo yako.
Hata me namshangaa
 
Wakuu naomba kuwakumbusha kwamba Android 13 ilishatoka toka mwaka Jana August na kwa Samsung imeanza kutoka October 22.

Simu yangu ilipata updates October 22, hivyo natumia Android 13 toka kipindi hicho.

Kitu kimoja nilisahau nimependa na ningependa kuwashirikisha ni uwezo wa kutokuonyesha nani anakupigia hadi pale utakapotoa lock ya simu.

Kama simu iko locked na mtu akapiga, haitoi mwanga wala kuonyesha jina zaidi ya mlio wa kuita/ringtone kuna mtu anakupigia. Hivyo ili kuona jina la mtu lazima utoe lock.

Hii ni feature nzuri kwa wale wazee wa nyumba ndogo.[emoji23]

Anyway, nawakumbusha tu, msisahau ku-update Android zenu. Wale wapenzi wa Samsung, tutegemee mambo mazuri kwenye Galaxy Unpacked tarehe 1 Februari 2023.

View attachment 2482989
Mkuu asante kwa taarifa hii. Samsung yangu juzi kati inaita haionyeshi namba nikajua mbovu kumbe ni android 13. Gracias senor!
 
Back
Top Bottom