Msishangae tumeona Watanzania wengi wanataka Haki

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Watanzania wengi hawajali vyama vya siasa wanajali Haki. CCM wanatumia pesa za serikali lakini kwasababu ya rushwa kubwa iliyopo serikalini na wananchi kukosa haki zao za msingi kuanzia mahakamani, chaguzi, polisi na mambo mengine tusishangae Watanzania wengi kufuatilia mkutano wa Chadema kuliko yale maonyesho ya mkutano wa CCM Dodoma.

Wakati Chadema wakionglea mambo ya kitaifa Raisi Samia na genge lake yuko na wasanii machawa wanatuonyesha mavazi mbali mbali na kuimba kama vile hii ni nchi ya wajinga jinga. Chadema tukubaliane nao au tusikubaliane nao wameheshimisha nchi yetu. Si kweli kwamba Watanzania hawapendi haki maana sasa ni kwanini wamefuatilia Chadema kwa kiasi hiki.

Yaani imefikia wakati Raisi anachagua makamu wake kwa hisia tu! hakuna kikao chochote, hatujui nani kampendekeza, hatujui kwa misingi ipi kapendekezwa, hakuna kupiga kura yeyote! yaani sasa huyo makamu atakuwa naye Chawa tu! Kwa utamaduni huu wa kitoto kitoto wa CCM hatutafika labda wabadilike

Watanzania wanahitaji mambo machache tu

1. Watanzania wanataka HAKI za kuweza kuzungumza, kuchagua watu wao kwa uwazi
2. Kupiga vita rushwa sio kusema tu kwa maneno
3. Uwazi kwenye rasilimali zao. Mikataba ya uwazi na sio mikataba ya 10% kwa wachache waliopo madarakani

Hayo mambo matatu hawajali ni chama gani CCM, Chadema au ACT wanaongoza bali ni mambo ambayo watapigania.
 
Nasubiri michango ya wengine kwanza ila jua kuwa una point kubwa to note.
 
Bila haki hata ukusanye wakata viuno wa pididi na waimba ngonjera wa nchi nzima bado watu hawatakukubali.
 
Sio tu wanataka HAKI,Bali wanaipenda Haki,basi tu🙂
 
Nilikuwa mjumbe wa Mkutano mkuu wa CCM uliofanyika Dodoma!!

Fedha halali nimepwa na CCM Tsh 2,600,000 na wajumbe tulikuwa 1,971

Wajumbe wote tumelipwa Tsh 2,600,000 × 1,971 = 5,124,600,000

CCM inapata wapi fedha mbona barabara nchi nzima ni mbovu na watu hawana maji safi na salama?
 
Watanzania wengi hawajali vyama vya siasa wanajali Haki. CCM wanatumia pesa za serikali lakini kwasababu ya rushwa kubwa iliyopo serikalini na wananchi kukosa haki zao za msingi kuanzia mahakamani, chaguzi, polisi na mambo mengine tusishangae Watanzania wengi kufuatilia mkutano wa Chadema kuliko yale maonyesho ya mkutano wa CCM Dodoma.

Wakati Chadema wakionglea mambo ya kitaifa Raisi Samia na genge lake yuko na wasanii machawa wanatuonyesha mavazi mbali mbali na kuimba kama vile hii ni nchi ya wajinga jinga. Chadema tukubaliane nao au tusikubaliane nao wameheshimisha nchi yetu. Si kweli kwamba Watanzania hawapendi haki maana sasa ni kwanini wamefuatilia Chadema kwa kiasi hiki.

Yaani imefikia wakati Raisi anachagua makamu wake kwa hisia tu! hakuna kikao chochote, hatujui nani kampendekeza, hatujui kwa misingi ipi kapendekezwa, hakuna kupiga kura yeyote! yaani sasa huyo makamu atakuwa naye Chawa tu! Kwa utamaduni huu wa kitoto kitoto wa CCM hatutafika labda wabadilike

Watanzania wanahitaji mambo machache tu

1. Watanzania wanataka HAKI za kuweza kuzungumza, kuchagua watu wao kwa uwazi
2. Kupiga vita rushwa sio kusema tu kwa maneno
3. Uwazi kwenye rasilimali zao. Mikataba ya uwazi na sio mikataba ya 10% kwa wachache waliopo madarakani

Hayo mambo matatu hawajali ni chama gani CCM, Chadema au ACT wanaongoza bali ni mambo ambayo watapigania.
Tutafika hapo wala sio siku nyingi. Wanaccm nahisi wengi kutokipigia chama chao kura mwaka huu kwa kutuletea wagombea legelege walafiwalafi wapigaji wapenda hela na mali. Watu hawaheshimu hata katiba na utaratibu wa chama chao. Ngoja tusubiri kuona.
 
Nilikuwa mjumbe wa Mkutano mkuu wa CCM uliofanyika Dodoma!!

Fedha halali nimepwa na CCM Tsh 2,600,000 na wajumbe tulikuwa 1,971

Wajumbe wote tumelipwa Tsh 2,600,000 × 1,971 = 5,124,600,000

CCM inapata wapi fedha mbona barabara nchi nzima ni mbovu na watu hawana maji safi na salama?
"Wajomba" kutoka uarabuni. Hawa "wajomba" wako tayari kumwaga shekeli zaidi huko October ili waitafune bongo.
 
Back
Top Bottom