#COVID19 Msisitizo Askofu Gwajima ni msimamo juu ya msimamo kuhusu Chanjo ya COVID-19

Kwa nini hii chanjo iwe kizingimkuti? Wanaokataa si wapuuzi wana hoja za kukataa kuchanjwa
Hakuna MTU amepewa amri ya kuchanja Chanjo ya COVID-19 bali ni hiari lakini Askofu Gwajima kashikia bango msimamo wake kutimiza agenda anayofahamu.
 
Msaada tutani kwenye video kama kuna udanganyifu au la ! Kama ni kweli hajachoma sindano ya chanjo ya covid-19; inapaswa hatua za kisheria zilichukuliwe kwa wahusika wote kwa udanganyifu kwa jamii.
Tazama video
https://www.facebook.com/
Tayari serikali imechukua hatua Kwa WATUMISHI wake walifanya igizo la upotoshaji kuhusu Chanjo ya COVID-19 Kwa Jamii.

Soma taarifa hapa chini

 

Leo hii Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima, amekanusha madai kuwa amelishwa sumu kutokana na msimamo wake kuhusu chanjo.

Askofu huyo ameeleza kuwa hajalishwa sumu, hakuna wa kumfanyia hivyo.

Akizungumza leo Jumapili Agosti 8, 2021 wakati wa ibada kanisani kwake kuwa, “Wanataka kusingizia watu, labda kusingizia kwamba serikali imeninywesha sumu. Niwahakikishie kwamba hakuna serikali imemnywesha sumu Gwajima kwa kuwa serikali ndiyo inasema chanjo ni hairi. Hakuna wa kuninywesha sumu na hatotokea.
Askofu huyo ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Kawe alizungumzia pia suala la chanjo huku akisema suala la afya ya mtu linapaswa kulindwa na mtu mwenyewe.

“Labda nitoe changamoto kwa wanaojiita watalaam waje walete andiko linaloonyesha kemikali zilizopo kwenye chanjo.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa kuratibu utafiti wa taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu (NIMR) Dk Paul Kazyoba ameeleza kuwa chanjo hiyo ni salama na imeanza kutolewa baada ya tafiti nyingi kufanyika na kujiridisha usalama wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…