Deogratias Mutungi
Senior Member
- Oct 1, 2019
- 140
- 181
Salaam waungwana wa Jamii forum
Baada ya ripoti ya CAG kubainisha madudu kwenye Wizara na taasisi mbalimbali za kiserikali, ikiwemo ubadhirifu wa mabilioni ya walipa Kodi maskini wa nchi hii, sasa ni dhahiri wapigaji wanaanza kutumia neno Rais kama taasisi kuhalalisha uhuni na ufisadi huu.
Afrika uwajibikaji ni mtihani mgumu na pengine si ustaarabu tuliouzoea lakini Kwa ripoti ya mwaka huu sharti kila Wizara na taasisi iliyobainika kuboronga na kupora pesa ya umma ni lazima wawajibike kwa kuwajibishwa na mamlaka husika baada ya kukaidi kufanya hivyo tangu watajwe na CAG.
Rai yangu ni kuwa ama wewe ni Waziri, Katibu Mkuu, Mkurugenzi au Mkuu wa idara yoyote kama umetajwa Kwa namna yoyote tafadhari wajibika, Cheo ni dhamana ya muda sawa na Koti linapokupwaya unalivua na kuliweka pembeni, tusipotoshe Kwa kutumia taasisi na nembo ya urais kuficha ufisadi unaoendelea ndani ya taifa hili linaloendelea kiuchumi na linalotegemea mikopo ya nje kuendesha bajeti yake, kuweni waungwana wajibikeni Kabla ya bunge kukunjua makucha yake, Nawasilisha! Asante.