Msituweke kwenye Magroup ya Mchango wa Harusi na Sendoff bila ridhaa yetu!

Msituweke kwenye Magroup ya Mchango wa Harusi na Sendoff bila ridhaa yetu!

Uzuri hatusihi kisiwani, yaani ungekuwa unaishi mwenyewe kisiwani huko ndio.ungesema haya mambo ya jamii hutaki na hufanyi.

Muhimu sana kushiriki haya mambo!!
 
We nawe kwaiyo waliokata tamaa za ndoa na umri umeenda kwamba wanawivu ndo maana hawatoi michango sidhan kama Kuna kitu kama icho

Kutoa ni moyo mtu apende mwenyewe sio Kwa sababu ulizoandika ww
 
Sherehe harusi ni watu , ndio maana utaona hata Wlfred tarimo, bilionea pale Moshi wana harusi ya binti yake na alikusanya michango kwa marafiki zake, harusi ilikuwa milioni 300 lakini alikusanya , so kwamba hana hela bali ni upendo.

Maskini hawapendi ushirika.
Marekani ianchangia nchi maskini, nchi maskjini zinanunua magoli ila huwa haizsaidii.
ushawahi kujiuliza kwanini ndege wafananao huruka pamoja?
 
Kumuunga mtu kwenye group bila ruhusa yake sio ustaarabu. Suala la kusaidiana waafrika ni jadi yetu kwaiyo ni vyema kumwambia tu mtu moja kwa moja kuliko kumuunga katika hayo magroup.

Vilevile tujifunze kusema hapana, kama hauna hela au hata kama unayo basi bajeti ya kutoa mchango haujupigia hesabu sema kweli kuliko kutoa ahadi hewa au kutoa pesa ambayo haikua kwenye mpango wa bajeti yako
 
Tuwekeni kwenye magroup ya kutoa michango kwa ajili ya kuuguzana.
 
Kuna jamaa yangu alinielekeza hauwezi kuungwa kwenye group lolote la WhatsApp bila ridhaa yako, mtu akitaka kukuunga hawezi ila inakuja link ambayo wewe mwenyewe utakuwa na maamuzi ujiunge au lah.
 
Kuna jamaa yangu alinielekeza hauwezi kuungwa kwenye group lolote la WhatsApp bila ridhaa yako, mtu akitaka kukuunga hawezi ila inakuja link ambayo wewe mwenyewe utakuwa na maamuzi ujiunge au lah.
hufikiri labda ni roho ya uchoyo na umaskini?
hufikiri kuwa Mungu ametufweka tufaidiane?

USA angegomea condom zake mngeweza kumudu bei ya soko
USA angegome p2 mngeweza kuzaa hao watoto mnaoua kila uchao kwa kutoa mimba?
 
Watu wafanye harusi kwa kadri ya uwezo walionao sio kutaka harusi ya kifahari kwa kutegemea michango ya ndugu, jamaa na marafiki huo ni ukichaa.
Mathalani kuna kikao cha harusi ya jirani hapa bajeti ni 30M kikao cha kwanza bwana harusi na ndugu zake sio wametoa ni jumla ya ahadi yao ni 5M tu.
Ina maana harusi yake itategemea michango yetu tu.
 
% m ni kubwa sana .
Vikaoa vingi nilivyoshiriki ndugu na wazzi wakichanga wanafika 2 m na mchango wa mwisho alipata 42 milion.
Kama huna roho ya kutoa wengine wana roho ya utoaji
 
Back
Top Bottom