Msiwaonee wababa...

Kuna kaile kitabia cha kujisahau.si akina dada/mama tu hata wanaume.Hiki ndo chanzo cha kuharibu kila kitu.
 

Lizz uko sawa kabisa,mimi naamini ni ngumu sana mtu kuanza tabia mpya ukubwani na mara nyingi tabia tulizokua nazo huwa hazibadiliki.Nafikiri tunashindwa kusomana tabia vizuri ILA wanawake wengi huwa wanajisahau mara baada ya ndoa.Yaani wanarelax na kusababisha kila kitu kibaki kuwa mazoea ndani ya nyumba.Hawana ubunifu wa kubadilisha mambo fulani fulani kuanzia kwenye chakula,mavazi,muonekano na mpangilio wa fenicha ndani,na mbaya zaidi huko chumbani ndio kabisaaa.Kila siku venue ni ilele,muda uleule,kwa namna ileile tena...........................nashindwa kusema mengine hapa.Kwani mwanaume ni baba yako?aibu za nini?kawaambia nani eti si heshima...si mnakuwa chumbani jamani...mnadhani kwa nini mlango hufungwa?Heshima itaanzia sebuleni kuelekea nje,wanawake wengine mnawakimbiza waume zenu bila kujua,mnawafanya hata wawaone kero wakati mwingine kwani atakuchoka,then mtaanza mizozo isiyoisha,badala ya mwanamke kurudi nyuma na kuangalia alipokosea anaanza malalamiko chungu nzima.

Simaanishi wanaume wote wanaobadilika sababu ni hizi(wapo wenye tabia mbaya),ila wengi huchoshwa na hayo mazoea na ndio maana hukimbilia nyumba ndogo.Kuna msemo huu "Even if you are on the right track,you will get run over if you just sit there"

Wanawake tuamke!
 
lizzy...
yeyote atakae ku wife
will be the lucky guy.....
honestly...
 
Kweli mwanammke anaweza kusababisha mtu apaone nyumbani pachungu? Au kitakuwa ni kisingizio tu..?
 
Kweli mwanammke anaweza kusababisha mtu apaone nyumbani pachungu? Au kitakuwa ni kisingizio tu..?
Kama ambavyo pilipili inaweza kuongeza ladha kwenye chakula na kukupendezesha au kukifanya kiwe kichungu kiasi cha mlaji kushindwa kula ndivyo hivyo hivyo inavyokua majumbani!!!
 
Ndoa ni mtihani mkubwa sana lizzy ukishaingia ndio utaweza kujibu maswali yako yote uliyouliza, usiwe na haraka na hata siku moja huwezi kujua mo matter what mpaka likukute, tumeona madada walio kwenye ndoa na still majibu hatuna
 
Kweli mwanammke anaweza kusababisha mtu apaone nyumbani pachungu? Au kitakuwa ni kisingizio tu..?
Mi nakwambia hajui ndoa inafananaje, inaweza kuwa tamu kama asali na chungu kama shubiri, ila asilimia kubwa ni wanaume wanaowaangusha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…