Msomi ambaye hajawahi kufeli "Nikki wa Pili" hajui kuandika

Msomi ambaye hajawahi kufeli "Nikki wa Pili" hajui kuandika

Usomaji wa vitabu sana unasaidia uandikaji wa misamiati kwa usahihi ukiachilia mbali Kiswahili si lugha mama kwako.Rejea kwa mwalimu Nyerere.
 
Mada yako haina maana hata. Kidogo mkuu kajipange hayo ni makosa ni kawaida tuu
 
1. Nikki wa Pili amejinadi kuwa hajawahi kufeli toka aanze kusoma

2. Nikki wa Pili anasema yeye anasoma sana vitabu

SASA
-Alikuwa anafaulu vipi mtu ambaye hajui hata kuandika spelling za neno jua pia spelling za mvua. Ukiangalia picha niliyoambatanisha utaona, kuna makosa ya kawaida katika uandishi lakini hilo kosa ni kwamba hajui kuandika. Je, mfumo wetu wa elimu ni kweli unashida kama yeye ambavyo huwa anasema?

-Mtu anayesoma sana vitabu huwa anajua sana misamiati na spelling, sasa kama yeye huwa anasoma anasoma nini hicho ambacho kiasi kwamba anashindwa kuandika maneno ya darasa la kwanza.

NIKKI PUNGUZA UJUAJI, UTAKUPONZA.

(Kaandika huko Instagram)
Jua kaandika Juwa
Mvua kaandika mvuwa
Mkuu kwa Dizain ya kizazi hiki kisichotaka kuchapwa wala usishangae
 
Mada yako haina maana hata. Kidogo mkuu kajipange hayo ni makosa ni kawaida tuu
Makosa ya kawaida ni yale ya typing error ila hayo makosa ni yanaonesha in jinsi gani msomi huyo haijui lugha yake ya kiswahili na hili ni tatizo kwa watu wengi sana hasa hasa waswahili wa dar wanamakosa mengi kama hayo kiasi kwamba kuna mtu mmoja alinishangaa nilipomrekebisha yaan mtu anakosea mpaka anaona yuko sawa na anaona ni kawaida kama wewe unavyojaribu kutetea makosa.
Na wengi wanaofanya makosa kama hayo hua wanashindwa sehemu ya neno ambako kuna a,e,I,o,u
Mfano.
1.Hanakuja badala ya anakuja
2.hendelea badala ya endelea
3.hingekuaje badala ya ingekuaje
4.hokolewa badala ya okolewa
5.hulimbukeni badala ya ulimbukeni
Makosa mengine ambayo watu hao ambao wanaofkiria kujua kiswahili ni kuongea saaana mara nyingi ukiwaambia waandike statement ya wanavyoviongea mara nyingi hua hivi.
Mfano: leho nilihenda ospitari kumsalimiha mjomba wangu halikua hanaumwa hugonjwa wa hajabu sana kwa kweli himenishtuwa sana sikutegemeha kuwa mjomba angeliha mpaka machozi, siunajuwa wanaume huvumilivu.

Tujitaidi kujifunza kiswahili tunu yetu
 
JF raha sana...hata mimi mwenye ka diploma kangu ka kuunga na gundi ila nikiwa hapa naweza kuwashambulia mpaka wenye master's zao
 
Mi nnachofahamu 90% hasa kwa waliofika degree wamesoma kumaliza makaratasi ya kile wanachokisomea,hiyo elimu haimsaidii yy,familia yake wala jamii yake huo ndo ukweli,vjn wengi tambo kibao mm injinia lkn anakaa Jf kulalamika ajila serikali haitoi,anasomea biashara,unamfungulia Kaduna na bado kanakufa ndo jamii hiyo ya tambo
 
Toka tetesi zivume kuwa jamaa anataka kugombea kupitia ccm jimbo la arusha mjin vijana mmeamua kumuandama kinoma
 
Back
Top Bottom