Mshua's
JF-Expert Member
- May 22, 2013
- 804
- 553
Msomi ni mtu aliyefikia ngazi ya chuo kikuu na kuspecialise kwenye taaluma fulani. Mfano: O'level alisoma kemia, A'level alisoma kemia, bachelor degrer alisoma kemia, master's degree alisoma kemia na PhD alisoma kemia. Huyu ndio unaweza kumuita msomi! Achana na na hao wanaosema msomi ni mtu anayeweza kuyamudu mazingira na kutatua changamoto. Kuna watu wapo vijijini wameyamudu mazingira ya kijijini na wanaweza kutatua changamoto zinazowakabili kulingana na mazingira wanayoishi vijijini hawajaenda shule hata darasa moja. Je, hao utawaita wasomi? Msomi ni mtu aliyesoma vitu vya darasani na kubobea kwenye kitu kimoja huyo ndo msomi.