Msomi ni nani

Msomi ni nani

Msomi ni mtu aliyefikia ngazi ya chuo kikuu na kuspecialise kwenye taaluma fulani. Mfano: O'level alisoma kemia, A'level alisoma kemia, bachelor degrer alisoma kemia, master's degree alisoma kemia na PhD alisoma kemia. Huyu ndio unaweza kumuita msomi! Achana na na hao wanaosema msomi ni mtu anayeweza kuyamudu mazingira na kutatua changamoto. Kuna watu wapo vijijini wameyamudu mazingira ya kijijini na wanaweza kutatua changamoto zinazowakabili kulingana na mazingira wanayoishi vijijini hawajaenda shule hata darasa moja. Je, hao utawaita wasomi? Msomi ni mtu aliyesoma vitu vya darasani na kubobea kwenye kitu kimoja huyo ndo msomi.
 
Mbobezi wa swala furani kitaaluma hizo zingine ni fitna za Mjini Mjini tuyy
 
Habar wapendwa,
nimekuwa nikijiuliza sana ni ipi tofauti ya msomi na mtu mwenye elimu maana unakuja kuta mtu amesoma ila elimu hana na mwengine ana elimu lakini hajasoma

je utofauti uko wapi? ???????
 
Msomi ana makaratasi mengi sana. Cheti cha la saba, cha form four, cha form six, cha degree, etc. na mara nyingi haya makaratasi hayamsaidii sana.
Ila mwenye elimu wala hana mbwembwe hizo na anaitumia elimu yake zaidi ya makaratasi
 
Mawakili ndo wasomi wengine wana elimu hata uwe profesa wa elimu, hatukuiti msomi lakini wakili ni msomi.
Hivi unajua ni bora kuelimika (kuwa na elimu) kuliko kuwa msomi kwa Tz??
Ebu angalia sasa mawakili wasomi hawajui hata kutafsiri taratibu za kumpatia mtu dhamana wanaishia kulalama wakati ufinyu wao wao wa akili??!!
 
Hivi unajua ni bora kuelimika (kuwa na elimu) kuliko kuwa msomi kwa Tz??
Ebu angalia sasa mawakili wasomi hawajui hata kutafsiri taratibu za kumpatia mtu dhamana wanaishia kulalama wakati ufinyu wao wao wa akili??!!
Ishu ya dhamana
Wao ndo wasomi, kupata dhamana ni haki yako lakin pia ni utaratibu wa kisheria unabidi uwe mpole kila kitu kilishapangwa na kipo kwenye sheria soma sheria ya mwenendo ya makosa ya jinai namba 20 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002, kifungu kuanzia 64--69 utaelewa namna ya kupata dhamana
 
Msomi anauwezo wa kuchanganua mambo kwa kina hata kama ameishia form 4 but mwenye elimu anaweza akawa amefika level ya juu but hawezi kureason
Umeongea kinyume chake. Elimu ni taaluma au maarifa yanayoendana na vitendo. Mtu mwenye elimu ataonekana kwa kufanya vitendo ambavyo ndani yake kuna maarifa na mara nyingi vinakuwa na matokeo chanya ila msomi linatokana na neno kusoma yaani aliyekariri maandishi fulani. Na kuna level tofauti tofauti za usomi na wala haziendani na vitendo. Tanzania tuna wasomi wengi ila hawana elimu
 
1. Msomi ni yule alaienda shule mfano sekondary mpaka chuo kikuu...
2. Mwenye elimu huyu ni mtu mwenye uelewa na kitu fulan anaweza kua msomi au asiwe msomi ila akawa na ufahamu na maswala fulan mfano mtu ambae hajasoma lakini ana yajau mambo ya dunia mfano elimu dunia
 
Back
Top Bottom