Mother Confessor
JF-Expert Member
- Jan 7, 2016
- 18,677
- 45,532
Msomi ni yule anayeweza kusoma na kuandika,.kama mm na wewe tu wasomi,😎
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mmmm. Are you sureMsomi ni yule anayeweza kusoma na kuandika,.kama mm na wewe tu wasomi,😎
Kwa hiyo mwanariadha ni mtu yeyote anayeweza kukimbia?Msomi ni yule anayeweza kusoma na kuandika,.kama mm na wewe tu wasomi,[emoji41]
Hasante sana umedadavua kiasi kama nakuelewa,,,lakini vipi hii imekaaje,,Hata madiwani nao wanasema wasomi hawana kitu.Kwa mtizamo wangu,nadhani pengine mtu HAJIITI msomi bali HUITWA msomi,na wanaomuita hivyo wana sababu zao za msingi (mara nyingi ni wana fani wenzie).Jamii ina uhuru wa kukubaliana na kikundi hicho cha wana fani au kukipuuza.Uluteni,kwa mfano, una mantiki zaidi jeshini kuliko uraiani ambako sanasana wanaofahamu kidogo watasema ni cheo cha nyota mbili.Lakini kijeshi uluteni ni zaidi ya hayo "mawe mawili",kuna uongozi wa moja ya vikundi vya kivita (platuni,kama sijakosea),nk.
Nadhani pia vyeti sio lazima vimaanishe usomi.Lakini again,wanaofahamu zaidi ni wale waliotunuku vyeti hivyo.Jumuiya ya wahadhiri inapoafikiana na kumteua mmoja wao kuwa profesa,kwa mfano,ina mantiki zaidi katika mazingira yao kuliko nje ya ulingo huo.Jinsi ya uprofesa huo utavyotumika ni suala jingine,na jamii ina uhuru wa kuuponda au kuuenzi uprofesa huo.
Na kuhusu vigezo gani vinavyoweza kufanya mtu aitwe msomi,nadhani pia majibu yanaweza kutofautiana kati ya walio ndani ya fani flani na walio nje ya fani hiyo.
Pia naomba nitofautiane kidogo nawe dada yangu katika hoja yako kwamba msomi lazima awe amebuni kitu.Nadhani usomi na ubunifu ni vitu viwili tofauti japo inatarajiwa msomi awe mbunifu ingawa si lazima awe mbunifu.Lakini pia kama unapozungumzia ubunifu unamaanisha kuja na kanuni (theory) mpya,then kuna mahala flani kitaaluma ni lazima uje na aidha theory mpya au uifanyie maboresho kwa iliyopo.Nje ya uwanja wa kitaaluma,huo unaweza usiitwe ubunifu lakini ndani ya ulingo huo,huo nao ni ubunifu.
Pia naomba kutoafikiana nae kwamba kile unachokuja nacho wakati unaingia chuo kikuu kinaondolewa na KUWEKEWA UNACHOTAKIWA KUAMINI...Nani anayekutaka kuamini?Labda kwa wenzetu wa sayansi ambao nyakati nyingine X ni lazima iwe X,lakini mara nyingi (japo si mara zote)huko kwenye "ungwini" ni namna mwanafunzi anavyoweza kucheza na hoja zake.Iwapo kuna mahala mwanafunzi analazimishwa kutetea hoja isiyo yake pasipo kuhoji basi hapo kuna kasoro.
Kuhusu kukutana (naomba kukunukuu)"watu wengi ambao nawafahamu, ambao wamekariri sana elimu ya darasani, wanayo madigrii lakini ukizungumza nao, utafikiri umekutana na mtu ambaye hajawahi kutia mguu darasani hata siku moja" hudhani kwamba tatizo linaweza kuwa mnahukumiana ndivyo sivyo?Yawezekana wao wanaamini mnaelewana katika mnachoongea lakini kumbe sivyo.Hudhani pia kwamba unaweza kuwa huwatendei haki kwa "kujipa mamlaka" (samahani kwa neno hilo) ya kuwahukumu?Au haiwezekani kwamba kwa vile hoja zao hazikuendana na matarajio yako ndio maana ukazihukumu kuwa ni kama za mtaani?
Mwisho,nadhani "makaratasi" (kwa maana ya vyeti) yataendelea kubaki na umuhimu wake hususan miongoni mwa wanafani husika.Kuwepo kwa vyeti feki hakuwezi kuondoa umuhimu wa vyeti halali just like kuwepo kwa noti feki kusivyoweza kuondoa umuhimu wa noti halisi.Jamii hailazimishwi kuthamini au kupuuza vyeti hivyo.Elimu itaendelea kupatikana mtaani,madarasani,kwenye karakana,semina,nk...ni kutoka katika mazingira hayo ndio wahusika watampachika mwenzao/wenzao joho la usomi,umahiri,ujuzi,ubobeaji,ujanja,nk.Watakaotuzwa joho hilo nao hawawezi kuilazimisha jamii iwathamini/iwakubali,bali matokeo ya kazi zao yanaweza kufanya hivyo.
Au niseme labda msomi ni mtu yeyeote mwenye hekima na busara,,na si veti vya shule,,hebu nisaidie hapoKwa mtizamo wangu,nadhani pengine mtu HAJIITI msomi bali HUITWA msomi,na wanaomuita hivyo wana sababu zao za msingi (mara nyingi ni wana fani wenzie).Jamii ina uhuru wa kukubaliana na kikundi hicho cha wana fani au kukipuuza.Uluteni,kwa mfano, una mantiki zaidi jeshini kuliko uraiani ambako sanasana wanaofahamu kidogo watasema ni cheo cha nyota mbili.Lakini kijeshi uluteni ni zaidi ya hayo "mawe mawili",kuna uongozi wa moja ya vikundi vya kivita (platuni,kama sijakosea),nk.
Nadhani pia vyeti sio lazima vimaanishe usomi.Lakini again,wanaofahamu zaidi ni wale waliotunuku vyeti hivyo.Jumuiya ya wahadhiri inapoafikiana na kumteua mmoja wao kuwa profesa,kwa mfano,ina mantiki zaidi katika mazingira yao kuliko nje ya ulingo huo.Jinsi ya uprofesa huo utavyotumika ni suala jingine,na jamii ina uhuru wa kuuponda au kuuenzi uprofesa huo.
Na kuhusu vigezo gani vinavyoweza kufanya mtu aitwe msomi,nadhani pia majibu yanaweza kutofautiana kati ya walio ndani ya fani flani na walio nje ya fani hiyo.
Pia naomba nitofautiane kidogo nawe dada yangu katika hoja yako kwamba msomi lazima awe amebuni kitu.Nadhani usomi na ubunifu ni vitu viwili tofauti japo inatarajiwa msomi awe mbunifu ingawa si lazima awe mbunifu.Lakini pia kama unapozungumzia ubunifu unamaanisha kuja na kanuni (theory) mpya,then kuna mahala flani kitaaluma ni lazima uje na aidha theory mpya au uifanyie maboresho kwa iliyopo.Nje ya uwanja wa kitaaluma,huo unaweza usiitwe ubunifu lakini ndani ya ulingo huo,huo nao ni ubunifu.
Pia naomba kutoafikiana nae kwamba kile unachokuja nacho wakati unaingia chuo kikuu kinaondolewa na KUWEKEWA UNACHOTAKIWA KUAMINI...Nani anayekutaka kuamini?Labda kwa wenzetu wa sayansi ambao nyakati nyingine X ni lazima iwe X,lakini mara nyingi (japo si mara zote)huko kwenye "ungwini" ni namna mwanafunzi anavyoweza kucheza na hoja zake.Iwapo kuna mahala mwanafunzi analazimishwa kutetea hoja isiyo yake pasipo kuhoji basi hapo kuna kasoro.
Kuhusu kukutana (naomba kukunukuu)"watu wengi ambao nawafahamu, ambao wamekariri sana elimu ya darasani, wanayo madigrii lakini ukizungumza nao, utafikiri umekutana na mtu ambaye hajawahi kutia mguu darasani hata siku moja" hudhani kwamba tatizo linaweza kuwa mnahukumiana ndivyo sivyo?Yawezekana wao wanaamini mnaelewana katika mnachoongea lakini kumbe sivyo.Hudhani pia kwamba unaweza kuwa huwatendei haki kwa "kujipa mamlaka" (samahani kwa neno hilo) ya kuwahukumu?Au haiwezekani kwamba kwa vile hoja zao hazikuendana na matarajio yako ndio maana ukazihukumu kuwa ni kama za mtaani?
Mwisho,nadhani "makaratasi" (kwa maana ya vyeti) yataendelea kubaki na umuhimu wake hususan miongoni mwa wanafani husika.Kuwepo kwa vyeti feki hakuwezi kuondoa umuhimu wa vyeti halali just like kuwepo kwa noti feki kusivyoweza kuondoa umuhimu wa noti halisi.Jamii hailazimishwi kuthamini au kupuuza vyeti hivyo.Elimu itaendelea kupatikana mtaani,madarasani,kwenye karakana,semina,nk...ni kutoka katika mazingira hayo ndio wahusika watampachika mwenzao/wenzao joho la usomi,umahiri,ujuzi,ubobeaji,ujanja,nk.Watakaotuzwa joho hilo nao hawawezi kuilazimisha jamii iwathamini/iwakubali,bali matokeo ya kazi zao yanaweza kufanya hivyo.
Wewe ahhhh banah kweliMsomi ni yule anayeweza kusoma na kuandika,.kama mm na wewe tu wasomi,[emoji41]
Msomi ni yule mwenye taaluma fulaniKwani msomi ni nani? Wabobezi nifafanulieni
mawakili tu ndo wasomi wengine wote ni wahitimuKwani msomi ni nani? Wabobezi nifafanulieni
Ahsante sana umedadavua kiasi kama nakuelewa,,,lakini vipi hii imekaaje,,Hata madiwani nao wanasema wasomi hawana kitu.
Naomba kuchangia tena.Au niseme labda msomi ni mtu yeyeote mwenye hekima na busara,,na si veti vya shule,,hebu nisaidie hapo
Msomi ni mtu aliyesoma.Kwani msomi ni nani? Wabobezi nifafanulieni
kaka nimekuelewa,,umedadavua hakika nimekuelewa vizuri,,ila kwa hili limeakaaje kama msomi ni yeyote aliyeenda shule,,kwamantiki hiyo basi hata aliyeishia darasa la saba na hakufaulu ni msome,,ila mwalimu wa SUA ni msomi wa taaluma...hapa ikoje,,Naomba kuchangia tena.
Nadhani kuna tofauti ya maana ya kitu na namna kitu hicho kinavyopaswa kuwa.Daktari wa SUA aliebukua na kupata udaktari ni msomi.Jamii ipende isipende,ili kuwa na ujuzi alofikia muungwana huyo lazima hatua flani zipitiwe,ikiwa ni pamoja na kuingia darasani,kutoa mihadhara,nk.Hizo ni taratibu za kuingia daraja la usomi.Usomi wa Msomi usipoweza kuisaidia jamii,au kutokuwa na manufaa kwa jamii,inapelekea kushuka thamani kwa usomi huo,lakini hakuondoi usomi.Kitakachotengua usomi wa mhusika ni kukiuka kanuni na taratibu za fani husika,na sio flani anapenda au flani hapendi.Ikumbukwe,walomwingiza katika daraja hilo sio jamii bali WASOMI wenzie.Wanaweza kuwa mabwanyenye wanaofikiria maslahi yao binafsi,lakini huo ndio ukweli mchungu wa maisha.Kwa mfano,Tuna viongozi wabovu,lakini kwa vile wamechaguliwa (wakati mwingine kwa kununua kura) wanaendelea kuitwa viongozi.Je wabunge wasiowakilisha VEMA wananchi wao hatuendelei kuwaita WABUNGE?
Nadhani kisifa (adjective) USOMI inatokana na kitenzi (verb) SOMA au KUSOMA.Kwa mantiki hiyo,USOMI unahusiana na KUSOMA,na nomino MSOMI ni MTU ALIESOMA.Wakati mwingine maneno ya kiswahili yanaleta maana flani yanapoelekwa kwenye lugha nyingine.Kwenye Swahili-english dictionary,ukisaka maana ya neno MSOMI kwa Kiingereza inakupa majibu yafuatayo:
msomi , pl wasomi { English: intellectual }
noun
msomi , pl wasomi { English: learned person , pl learned people }
noun
msomi , pl wasomi { English: lecturer , pl lecturers } [derived: soma V]
noun
msomi , pl wasomi { English: reader } [derived: soma V]
noun ,
msomi , pl wasomi { English: scholar , pl scholars } [derived: Swahili -soma]
noun
5 distinct results returned (chanzo:THE KAMUSI PROJECT)
Kwa mtizamo wangu unaoweza kuwa sio sahihi,nadhani kuna umuhimu wa kutofautisha MATARAJIO YA JAMII KWA "WASOMI" na MAANA YA NENO "MSOMI".
Bwaya anahoji iwapo Profesa anayepika tafiti zake kwa manufaa ya mafisadi, je naye ni msomi?Yes,ni MSOMI,lakini ANAYEKIUKA KANUNI,TARATIBU NA SHERIA ZINAZOONGOZA FANI YAKE.
Kuna baadhi ya sifa ambazo mtu akishafanikiwa kuzipata hubaki nazo kwa muda mrefu kama sio milele.Ni mithili ya ualimu,jina linaendelea kubaki MWALIMU hata pale mtu anapostaafu au kufukuzwa kazi.
Naomba kunukuu hoja nzito ya Bwaya kwamba "....Ninawafahamu wanasayansi wengi waliokimbia umande, ama kushindwa mitihani, ambao maarifa yao yanaheshimika mpaka leo. Je, hawa si wasomi hata kama hawana vyeti? Hawakuwahi kuitwa madokta wala maprofesa, lakini waliweza kuyatumia maarifa yao wenyewe ambayo wasomi wa enzi hizo hawakuwa nayo!" Binafsi,nadhani mwanzoni mwa mjadala niligusia juu ya umuhimu wa vyeti KAMA KITAMBULISHO lakini haimaanishi kwamba kutokuwa na cheti kunamuondolea mtu umahiri wake katika fani husika.Pia ili mtu aitwe msomi si lazima awe dokta au profesa LAKINI LAZIMA ASOME,iwe nyumbani,darasani au kwa njia ya posta au kujielimisha kwa elimu vitendo.HUWEZI KUWA MSOMI PASIPO KUSOMA.Utawezaje kuwa mwanasayansi kama hujasoma sayansi?
Mwisho,wakati JAMII INATARAJIA wasomi wafanye vitu kwa manufaa kwa jamii,kutakuwa na wasomi watakaotimiza matarajio hayo,na kuna wengine ambao hawatatimiza.Wote wataendelea kuitwa wasomi.Kitakachozidi au kupungua ni heshima yao kwa jamii na wanafani wenzao.Kinyume cha matarajio ya jamii kuhusu kinachotarajiwa kutoka kwa anayeitwa MSOMI hakibadili maana ya neno MSOMI...just like UONGOZI MBOVU usivyoweza kuondoa maana ya neno UONGOZI (bali kuathiri TASWIRA ya uongozi).
Swali,je kuna neno MBADALA kwa mtu aliyesoma sana lakini kusoma huko hakuinufaishi jamii?
Kwamba zile k tatu ya KKKNdugu,
Ukijua tu kusoma, kuandika na kuesabu basi wewe ni msomi
Kwahiyo aliye ishia darasa la saba sio msomiMsomi/Mwanachuoni ni mjuzi katika fani fulani kimaana na kimatendo na aliyekusanya misingi kumi ya fani husika.
Swali utamjuaje fulani ni msomi ? Hizi ni baadhi ya sifa za msomi yaani mwanachuoni.
1. Msomi hajiiti yeye ni msomi.
2. Msomi lazima awe ameidhinishwa na wasomi ya kuwa fulani ni msomi basi kachukueni elimu toka kwake. Kiistilahi kitendo hiki huitwa "Ijaza/Tazkiya".
3. Msomi lazima awe ameandika vitabu juu ya fani husika.
4. Msomi lazima elimu yake aifundishe yaani awe na wanafunzi, kwani husemwa ya kuwa "ukitaka kumjua msomi basi waangalie wanafunzi wake"
5. Msomi lazima awe amedumu katika fani husika kwa miaka mingi yenye kukidhi haja na kutajika.
Hizi ni baadhi ya sifa za msomi. Salamu hizi ziwafikie wale wajinga wajiitao "Wakili msomi" kisha wamehitimu miaka yao mitano na gamba lao kibindoni kisha akapiga mwaka ule mmoja.
Zingatia : Elimu ni ile unayotembea nayo kifuani mwako na elimu au usomi si wingi wa vyeti kabatini.
Utakuwaje na vyeti bila taaluma, maana yake umefoji yaani umedanganya, wewe huwezi kuwa msomi sababu una ujinga mara mbili.Kwahiyo mwenye veti vingi vyakutosha bila Taaluma sio msomi?
Atakuwa msomi endapo atakuwa na ujuzi wa fani fulani, haijalishi ana cheti au hana.Kwahiyo aliye ishia darasa la saba sio msomi
Ngoja niendelee labda utaelewakaka nimekuelewa,,umedadavua hakika nimekuelewa vizuri,,ila kwa hili limeakaaje kama msomi ni yeyote aliyeenda shule,,kwamantiki hiyo basi hata aliyeishia darasa la saba na hakufaulu ni msome,,ila mwalimu wa SUA ni msomi wa taaluma...hapa ikoje,,