Msoto wa maisha Dar es Salaam ulivyonifanya nitamani kuwa mwizi na mhujumu uchumi

Msoto wa maisha Dar es Salaam ulivyonifanya nitamani kuwa mwizi na mhujumu uchumi

Mkuu, ndio imeisha au bado inaendelea?

Nadhani wengi tunamatarajio ya kutaka kujua mwishoni hizi harakati zote zimekufikisha hatua gani kimaisha ili somo unalotupa likamilike.
Ndio imeisha mkuu, nipo kwenye ajira niliyoisomea chuo niko vijijini najishighulisha na kilimo na ufugaji, sitaki tena kashkash za mjini, nimeelezea kwa sababu nakumbuka nilipotoka na naona vijana wanaingia mitaani wakiwa na moto na hali ya kufanikiwa, hitimisho ni kwamba niliamua kutafuta pesa kwa njia halali japo nadhani Kama ningeendelea na ile njia haramu ningekua mbali sana
 
Dasaledee...

Jinsi vijana wanavyopambana kwenye huu mji najisikiaga kinyaa na hasira mtu akisema "...tatizo vijana wa siku hizi wavivu". Kuna kazi wanafanya baadhi ya watu basi tu huku ni mbali na dunia ila ilibidi amnesty int waingilie kati.
Dar watu wanapambana saaana
 
Hapo ndio mwisho ninaomba watu wazima kidogo watoe ushauri kwa vijana wanaopitia kipindi kizito au kigumu au graduate kuishi kwa namna bora ya kufanya taifa letu liwe bora zaidi.
Note mpaka Leo nina alama ya sehemu ya kichwa iliyopasuka nilikia nafuga nywele lakini hiyo sehemu nywele hazioti, nimekua naona huruma kwa wapambanaji Sana maana nakumbuka nilipotokea.
Ushauri wangu kwa vijana graduates waache uvivu na kujiona wana elimu kubwa hivyo kuchagua kazi.
Utakuta graduate anatumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii au kutext marafiki bila kufikiri hiyo mitandao (internet) inaweza kuwa chanzo cha yeye kupata pesa.
Utakuta kijana anaishi kwa wazazi au ndugu muda wote anatumia kuangalia Tv (movies & series & football) kichwa hakiwazi nje ya box kuhusu maisha.
Usharobaro mwingi sana kwa graduates huku wakiwa watupu mifukoni.
Nawaasa wawaze maisha na kufanya kazi yeyote halali kwa bidii,hizo kazi za ndoto zao professional zao zitakuwa muda ukifika ila wakati bado wanazitafuta wajichanganye kila eneo.
Waache kuigiza maisha ya kuwaona wasanii na watu maarufu namna wanavyoishi nao kuiga na kudhani maisha ni rahisi kama kujamb@

Pia wawe na heshima kwa wakubwa zao utakuta kijana kwa kuwa ana ndevu/mavuzi/matiti hasalimii mtu hata majirani kama sio ndugu hawajui kuwa adabu na heshima kwa watu ndio tiketi ya kufikia ndoto zao na kufurahia mema ya dunia.
 
Back
Top Bottom