Hii sehemu nitaongea kwa ufupi saana.
Huwa napenda sehemu zenye mchanganyiko maana huwa naamini pesa zipo.
Nilipita pale Karume nikaona watu wanaosha viatu kuna jamaa rafudhi yake alikua anaongea nikaona huyu wa nyumbani, tuliongea nae haswaa akawa Ananipa kazi ya kuosha viatu pc 1000 ananipa 5000 in short nikapiga kazi pale nikaanza kuzoeleka baada ya mwezi nikawa na hela kidogo ya kuchukua mzigo Kama 80,000 nikawa naingia mule ndani nachukia viatu vya watoto kwa 800 naosha then nauza kuanzia 3000.
Hapo pia msoto wake sio wa mchezo maana tunaanza kuuza viatu saa 8 usiku pale karume kwa nje, tunauza mpaka saa 12 asubuhi ikifika saa 1 asubuhi migambo wanazingua so tunaweka mzigo store mpaka saa 12 jioni ndio tunamwaga barabarani mpaka saa 3 usiku, hebu fikiria hiyo daily routine kwa kijana graduate Kama Mimi na wapo vijana wengi Sana wanaofanya hivyo mahangaiko ni makubwa but kinachopatikana ni kidogo, Mama akinipigia namwambia kila kitu kipo sawa.
Kwenye harakati ya kujichanganya na watu nikapata hili deal ambalo sitalizungumzia sana na ndilo lilinifanya niondoke Dar es Salaam na kusema sitorudi tena
Nilipata deal la kuuza Mafuta ya petrol na diesel kutoka kwa madereva wa mafusso na lorry wakienda huko wanarudi na mafuta tunakubaliana bei then mimi najua nitauzaje
Dah kwa Mara ya kwanza nikashika hela ambazo sikuwahi kushika maana nilikuwa napigiwa simu kila mahali demand ilikuwa kubwa lakini sikuweza ku-play smart nikakamatwa na polisi, huu msala ulikuwa mkubwa saana nahisi nilichomwa sikuwahi kulala polisi hapo kabla nikaambiwa nitapewa kesi ya uhujumu uchumi wakati Mimi nina mwezi tu tokea nianze kuuza mafuta😁😁....kwa ufupi msala uliisha japo haikuwa rahisi sitaongea mambo mengi hapa maana sikuwahi kuwaambia mtu hata mzee hakuwahi kujua Kama nilikamatwa nilipambana mwenyewe nikatoka!...
Nilitoa akiba yoote niliyokusanya kupitia hiyo biashara haramu nikachomoka...
Baada ya hapo nikaenda home Tabora sikukaa muda nikapata ajira, nikasema tokea moyoni sitorudi tena Dar maana kwa jinsi watu wanavyoishi ule ufahari unaweza Kufanya mambo maovu ili u survive. Unashangaa vijana hawana kazi lakini wanamiliki pesa chafu,
Vijana
Usitamani maisha ya mtu always kua wewe, hujui watu wanapatia utajiri.
Usije/usitamani kufanya biashara haramu zina hela sawa lakini ukibananishwa unaweza ukawa ndio mwisho wa ndoto zako humu duniani.
Kijana ukitoka nyumbani kwenda kupambana hakikisha unafikia kwa ndugu yako mtu mzima mwenye familia ili akusitiri kwa vitu vidogo Kama chakula, malazi huku wewe unaendelea kufikiri utafanya nini,
Kwa msoto niliopitia Dar ulinifanya kuwa mgumu na kuwaza kufanya biashara yoyote haramu ili nipate pesa but niliamua kuchomoka na kurudi kwa Mungu.
Tusisahau kupambana huku tukimuomba Mungu maana yeye ndiye mpaji wa vyote.
Lakini bado naamini humu duniani Kama umezaliwa familia maskini kutoboa kufika hatua ya kumiliki pesa sio rahisi kwakweli
Hapa simaanishi pesa ya nyumba na gari namaanisha pesa haswaaaa.