Mstaafu anakwama sababu ya kukosa ID ya NIDA

Mstaafu anakwama sababu ya kukosa ID ya NIDA

Nimefika ofisi ya nida hapa kdc wanasema siku hizi huduma ya online copy wanasema haipo
 
taratibu mkuu,
huyu mzee namba ya NIDA anayo ila kitambulisho cha Nida hana kama mamilion ya Watz wengi ambao bado wanasubiri.
Hebu hizi stress zisitupelekee hadi tukaanza kukosea heshima wazazi wa wa mtu.
Sina stress yoyote niko normal kabisa na nasimamia hoja yangu, ikiwa ana namba toka mwanzo alipaswa kuwa na kitambulisho au nakala ya kitambulisho ambayo majuzi wakati wa usajili wa line ya za simu zilikuwa zinapatikana online, lakini pia Mzee alijua anatarajia kustaaafu kitambulisho ni kitu mhimu Sana wakati wa kujiandaa kustaafu, nimesema ni mzembe siyo namdharau Ila Kwa aina ya kesi yake, kumbuka hata wazembe huzeeka. Kuna watu kwa asili ni wakuupuuza kila Jambo. Nikupe mfano Mimi nimwzaliwa kijijini mahali ambapo tulikuwa tunazaliwa popote hata njiani Kwa sababu ya kutokuwa na huduma za afya karibu. Lakini Kwa leo hii Nina Cheti cha kuzaliwa, Nina documents zote za nchi hii. Lakini mke wangu aliyezaliwa mount meru hosp Hana Cheti cha kuzaliwa wala kitambulisho, hata line alifungiwa ndo akaenda kuomba kitambulisho, pindi alivopata namba ya kumuezesha kusajili line hakuwahi kurudi tena NIDA, Leo hii Mtoto anatakiwa kuhakiki vyeti vya wazazi Kwa ajili ya kuomba mkopo WA elimu ya juu, mama Hana kitambulisho, Hana Cheti cha kuzaliwa.
Ndo maana nikauliza huyu mstaafu wa kada ipi ambaye alishindwa hata kufanya maandalizi ya kustaafu?
Mimi huwa siyo MTU wa kusapoti kila Jambo, ikiwa kukosoa nitakosoa. Kama nimekukera utanisamehe lakini na wewe chukuwa Hili kama somo ili uwe na nyaraka zote za serikali
 
Akatafute kitambulisho, Hilo siyo la kuhitaji ufahamu, ni mstaafu wa Kada gani hiyo ambaye hakujua hata umhimu WA kuwa na kitambulisho cha NIDA. Mzee wako ni mzembe na usishangae siku akipata mafao akatepeliwa tena hela yote.

Endapo alijiandiksha toka mwanzo ina maana ni mwaka elfu na 12 kama sijakosea, awamu JK na vile vitambulisho visivyo kuwa na sahihi ya mwenye kitambulisho, 2012 mpaka Leo ni miaka 9 Mzee ameshindwa kufuatilia kitambulisho kweli?
Hujielewi wewe. Yani kwakuwa wewe una kitambulisho unajiona mjuaji kumbe ni zwazwa tu. Halafu kuwa na heshima kwa wakubwa zako.

Watu tumefanya registration tokea last year tumeishia kupewa namba tu. Kila ukifuatilia ID unapigwa danadana tu halafu mjinga mmoja unaandika upupu wako hapa.
 
Wakuu heshima kwenu,

Mbali na kuwa ana namba ya kitambulisho cha NIDA mzazi wangu aliyefikisha umri wa kustaafu anakwama kufwatilia process zote ndani ya halmashauri anapofanyia kazi kwakuwa anakosa kitambulisho cha NIDA. Wahusika wanaopokea barua zake wamekataa kutumia namba ya NIDA wanataka kitambulisho.

Kwa wenye uzoefu ninaomba kujua ni wapi anaweza kupata kitambulisho hicho maana ni wale waliojiandikisha awamu ya mwanzo kabisa kabla ya zile foleni za mwaka jana.

Asanteni.
Nanyinyi mmezidi uzembe unauwezo wakushinda jamii forums lakini uwezo kumshauri maama kwamba nimuhimu sana kua na ID na sio namba ....bibiyake mwanaoa atakua anaumia sana
 
Hujielewi wewe. Yani kwakuwa wewe una kitambulisho unajiona mjuaji kumbe ni zwazwa tu. Halafu kuwa na heshima kwa wakubwa zako.

Watu tumefanya registration tokea last year tumeishia kupewa namba tu. Kila ukifuatilia ID unapigwa danadana tu halafu mjinga mmoja unaandika upupu wako hapa.
Imagine kitambulisho kiliombwa mwezi wa 2 mwaka 2015 hadi Leo wameniangalizia ofisi ya nida wilaya hakijatengenezwa. Hapo tatizo ni la mzazi wangu au serikali ? Maana namba anayo tangia hapo.
 
Imagine kitambulisho kiliombwa mwezi wa 2 mwaka 2015 hadi Leo wameniangalizia ofisi ya nida wilaya hakijatengenezwa. Hapo tatizo ni la mzazi wangu au serikali ? Maana namba anayo tangia hapo.
Fuatilieni tu mkuu kwenye ofisi zao ikiwezekana omba kuonana na mkurugenzi.
 
Nanyinyi mmezidi uzembe unauwezo wakushinda jamii forums lakini uwezo kumshauri maama kwamba nimuhimu sana kua na ID na sio namba ....bibiyake mwanaoa atakua anaumia sana
We nae Acha upoyoyo
Tatizo sio la mzazi ni lq kwenu NIDA
 
Wamecheki hakijatoka
Duh noma. Nakumbuka nilifanyaga field NSSF nikawa na print vi card vya wanachama vile. Yani unamwandikisha mtu ndani ya dakika kumi tayari usha print digital card yake anasema. Anaekuja kuchukua duplicate (walipoteza) ndio chap tu kwa haraka yani akishalipia ada ya duplicate dakika 2 kachukua kadi yake kasepa.

Sasa hawa NIDA kama waliona hawawezi bora wangetoa tender kuna makampuni yangeweza kuwa yameshakamilisha hili zoezi kwa asilimia 99.
 
Asisahau kunywa maji pia.
Siyo hasira mkuu hebu fikiria namba za mwanzo ni Enzi za Jk, na Mzee alitambua anastaafu hizi document alipaswa kupata haraka Sana. Tusimtetee Kwa sababu ni Mzee hata wazembe wanazeeka pia.
Ndo maana nikatamani kujua huyu Mzee ni mstaafu wa Kada ipi? Ambaye hata hakufaham kuwa wakati wa kuprocess mafao inatakiwa kuwa na nyaraka zote mhimu za serikali. Ndo maana nikashauri huyu mwanae amsimamie kila kitu akiachiwa peke yake atatrpeliwa. Kuna wastaafu kibao wanatepeliwa kizembe. Majuzi kuna mwalimu huko Mbeya kapigwa milioni 20 eti aliambiwa zikaatamiwe na chatu kuondoa mikosi. Huko Shinyanga nako nimeshasikia vilio kibao
Hujielewi wewe. Yani kwakuwa wewe una kitambulisho unajiona mjuaji kumbe ni zwazwa tu. Halafu kuwa na heshima kwa wakubwa zako.

Watu tumefanya registration tokea last year tumeishia kupewa namba tu. Kila ukifuatilia ID unapigwa danadana tu halafu mjinga mmoja unaandika upupu wako hapa.
Kati yangu na wewe Nani zwazwa sasa, kama ulikuja kugundua mwaka Jana kuwa unahitaji kitambulisho, vitambulisho vimeanza kutolewa lini nchi hii? Hivi unajua mstaafu wewe? Ni MTU ambaye kuulizwa kitambulisho siyo Jambo la Kwanza Maishani mwake, ukubali usikubali Mzee alifanya uzembe na hayo ndo matokeo ya huo uzembe sasa anajichelesha mwenyewe kupata mafao yake. Na wewe chukuwa Hili kama somo kwamba usipopanga mambo yako mapema utapangiwa. Watanzania wengi tunakasumba ya kusuburi mpaka siku ya mwisho
Nanyinyi mmezidi uzembe unauwezo wakushinda jamii forums lakini uwezo kumshauri maama kwamba nimuhimu sana kua na ID na sio namba ....bibiyake mwanaoa atakua anaumia sana
Nakubaliana na wewe, mzazi hakuona umhimu kitambulisho na mwanae naye akashindwa kumshauri mapema. Mpaka kuja humu jamii forum ina maana na yeye alikuwa hafaham utaratibu wa kuomba na kupata mafao achilia mbali kitambulisho, uzembe, uzembe, uzembe.
 
Hujielewi wewe. Yani kwakuwa wewe una kitambulisho unajiona mjuaji kumbe ni zwazwa tu. Halafu kuwa na heshima kwa wakubwa zako.

Watu tumefanya registration tokea last year tumeishia kupewa namba tu. Kila ukifuatilia ID unapigwa danadana tu halafu mjinga mmoja unaandika upupu wako hapa.
una stress zake huyu kaamua kumtolea mzee wa watu ambaye hata hamjui 🤣 🤣 🤣
 
Inawezekana mama aliandika taarifa tofauti na zilizomo kwenye mafaili yake yakazi ,msaidie mama haraka ukomkoa gani
Angeandika taarifa tofauti namba ya NIDA ingetoka? Ndo maana nilikuambia uache upoyoyo maana hujasoma uzi viruri. Kama namba ya nida (ambayo ni namba ya kitambulisho kinachotolewa na mamlaka ya serikali) kwa nini wasikitambue hadi wadai original kadi ambayo wanajua kabisa serikali kwa uzembe wake wamechelewesha kuvitoa?
Soma reply zangu zote utaona.
 
Duh noma. Nakumbuka nilifanyaga field NSSF nikawa na print vi card vya wanachama vile. Yani unamwandikisha mtu ndani ya dakika kumi tayari usha print digital card yake anasema. Anaekuja kuchukua duplicate (walipoteza) ndio chap tu kwa haraka yani akishalipia ada ya duplicate dakika 2 kachukua kadi yake kasepa.

Sasa hawa NIDA kama waliona hawawezi bora wangetoa tender kuna makampuni yangeweza kuwa yameshakamilisha hili zoezi kwa asilimia 99.
Copy zilikuwa zinatolewa online majuzi Tu wakati wa usajili wa line za simu, lakini pia wale ambao kumbukumbu zao zilikuwa hazionekani walishauriwa kuomba upya. Vitambulisho na wengi walipata, tatizo tuna uzembe wa kufanya vitu. Hatuna deadline mpaka ukishabanwa kama hivo ndo unaanza kupaparuka
una stress zake huyu kaamua kumtolea mzee wa watu ambaye hata hamjui 🤣 🤣 🤣
Usikariri vitu, Mimi nikiwa na stress wewe hapa jamii forum hutii mkono
 
Mimi nilikuwa mtu wa mwanzo kupata vitambulisho vya NIDA zoezi lilivoanzaga mwanzoni kabisa, mbona wameweka expire date kuwa ni 2024 hivi Wana maana gani Ina maada mda ukiisha hakitumiki Tena au?

Maana ninavoona process ya kupata NIDA ilivo ngumu why waliweka expire date
Nashauri wewe endelea kukitumia hichohicho (kama hakikukwamishi kupata huduma yoyote kutokana mapungufu yake).

Ikifika mwaka 2023 mwanzoni, nenda NIDA na elfu 20 uwaambie umekipoteza kadi yako ya NIDA. Watakufanyia process za ku renew. Unapo renew kwa kawaida huwa kuna option ya kubadili baadhi ya taarifa zako (ukipenda) kama vile picha, anuani, kuchukuliwa alama za vidole, na bila shaka kusaini.

Wakati unakisubiri hiki kipya kitoke (ndio maana nimesema uyafanye haya mwaka 2023) utaendelea kukitumia kile cha zamani maana kinakua bado kipo "madarakani".

Kikitoka kipya, kile cha zamani unakifanya namna itakavyokupendeza.

NB:
Zipo sababu za kuweka expiry time ya vitambulisho kutokana na kwamba kunaweza kutokea mabadiliko kadhaa (ya kiteknolojia na kiuendeshaji) yanayoweza kupelekea kuwa na uhitaji wa kubadilisha vitambulisho.
Mfano what if ikaamuliwa kwamba vitambulisho vianze kutolewa kwa kulipiwa ili kuifanya NIDA iweze kujiendesha na kufanya kazi kwa ufanisi, wakati huo ulishatoa vitambulisho "vya milele" kwa wananchi walio wengi ?
Zipo sababu zingine pia za kiteknolojia kama nilivyodokeza hapo juu.

Kitu ambacho nina hakika nacho ni kwamba kwa kadi siku zinavyosonga, ndivyo ambavyo tutakua tunapata vitambulisho vyetu ndani ya muda mfupi. Kwahiyo usijali sana kuhusu mambo ya THE LONG WAIT kama ilivyo sasa hivi.
 
Angeandika taarifa tofauti namba ya NIDA ingetoka? Ndo maana nilikuambia uache upoyoyo maana hujasoma uzi viruri. Kama namba ya nida (ambayo ni namba ya kitambulisho kinachotolewa na mamlaka ya serikali) kwa nini wasikitambue hadi wadai original kadi ambayo wanajua kabisa serikali kwa uzembe wake wamechelewesha kuvitoa?
Soma reply zangu zote utaona.
Sawa
 
Nimefika ofisi ya nida hapa kdc wanasema siku hizi huduma ya online copy wanasema haipo

Ni kweli huduma ya online copy ilisitishwa kitambo.

Mlifikia muafaka gani sasa na hao jamaa wa NIDA juu hitaji lako ?
 
Maswala ya wastaafu nahs bado ni kero sana.
kwani hawajui kwamba MC44 atastaafu may 2023 ili waandae lundo lake? Sa100 mulika hilo
 
Back
Top Bottom