Wakulungwa hamjamboooo....!??
Ule wakati niliokuwa nausubiria kwa hamu sasa umefika. Hatimaye bibi Kasinde amestaafu na kulipwa stahiki yake kwa kuitumikia Jamuhuriya Muungano wa Tanzania kwa kipindi kisichopungua miaka 35.
Yaani waliosema pesa sabuni ya roho hawakukosea, mweeh mweeh yaani najikuta namtabasamia kila nnayepishana naye njiani.
Hapa natembea kwa mguu hadi Ocean Road nikashangae na bahari...
Magorofa nimeyashangaa hadi naona shingo inataka kwenda mrama sasa...😅😅
View attachment 2079267
View attachment 2079268
View attachment 2079269
View attachment 2079270
Karibuni tukale samaki wa baharini kwa wale walioko feri.
Update:
Wacha nimalizie matukio ambayo sikuyarusha kwa wakati..,,
View attachment 2079849
Mjini kutamu nyieee.... acha tuu
Pamoja na kuwa nimestaafu shamba siendi ng’oo...😜
View attachment 2079851
Wakulungwa si watu wazuri....
Walimtegea jiwe bi Kasinde, nilijikwaa ila sikuanguka... kiatu ndo kilipata hitilafu ikabidi nipate huduma kwa shushani...