Mstari huu ndani ya Biblia wachungaji wa kileo hawaupendi, wanauruka kama haupo kabisa, ingawa ndio msingi mkuu wa Ukristo

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Wachungaji, mitume, manabii, walimu na Wainjilisti ambao ni viongozi wa makanisa ya kileo huu mstari wanauruka kama haeauoni.
Huu mstari unawahukumu, maana wanajikusanyia sadaka kisha kufungua maduka makubwa, kusomesha watoto wao nje ya nchi , wananunua range , v8 n.k huku waumini wakiambiwa wamtumaini Mungu atawainua. Hata yeye (kiongozi) alianza chini na sasa ameinuliwa na Mungu.
Si lazima kila mtu auze mali zake na kuzipeleka kanisani ila ni lazima pesa za sadaka , michango na misaada ndani ya kanisa zihesabiwe kuwa ni mali ya kila muumini, hakuna mwenye mamlaka nazo kuzidi mtu mwingine ndani ya kanisa.
Muwe na asubuhi njema.
Screenshot_20250121-081533.jpg
 
View attachment 3208453
Huo ni Ukristo wa Ujamaa, aliouanzisha Yesu mwenyewe , sasa tuko kwenye Ukristo wa Kibepari ulioasisiwa na shetani mwenyewe
 
The Bible is the biggest lie in the entire history
Kama kweli vile..hebu tafakari
''watakaotenda mema wataenda mbinguni kwa baba wakiimba na kufurahi milele,
Watakao tenda maovu watakuwa motoni wakiungua milele"

Mbona Kama wote watateseka tu,maana kuomba tu milele si mateso hayo!
 
Kuletewa na kuikuta hakuna tofauti.
Acha kutumia misamiati kwa kupotosha mkuu.

Tofauti ipo.

Kuletewa ni pale umetulia kitu kinaletwa.

Kuikuta ni pale umefika mahali ukakuta kitu kipo pale tayari.
 
Shetani ni mwerevu sana, na anatupasua ipasavyo.
 
Acha kutumia misamiati kwa kupotosha mkuu.

Tofauti ipo.

Kuletewa ni pale umetulia kitu kinaletwa.

Kuikuta ni pale umefika mahali ukakuta kitu kipo pale tayari.
Maana yangu ni kwamba kukuta hicho kitu au kuletewa si muhimu bali cha muhimu ni hicho kitu chenyewe. Yani mtu huwezi kuona dini ya kuletewa ndio nzuri kisa umeletewa tu au imani za asili ndio nzuri na sahihi kisa tu ni za asili.

Tumeona vitu vingi vya kuletewa vizuri na vibaya na tumeona mengi ya asili mazuri na mabaya.
 
Nimekusoma mkuu 👊🏾👍🏾
 
Sio huo tu ipo mingi mfano

1korintho 15:51
Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala(kufa) sote, lakini sote tutabadilika,

Hosea 13:14
Nitawakomboa na nguvu za kaburi; nitawaokoa na mauti; ewe mauti, ya wapi mapigo yako? Ewe kaburi, ku wapi kuharibu kwako? Kujuta kutafichwa na macho yangu.

1korintho 15:26
Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti.

1korintho 15:28
Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana(Yesu) mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote.

Ufunuo 21:3
Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.
 
Back
Top Bottom