mischa,
Linea nigra ni mstari mweusi uliosimama (vertical) ambao mara nyingi huanzia kwenye nyonga hadi kitovuni (kwa wanaume na wanawake) lakini kwa baadhi huonekana hadi sehemu ya juu ya tumbo (karibu na kifua) hii haimaanishi kuwa wao wanashida! Mstari huu huonekana zaidi/kwa urahidi kwa wanawake wenye ngozi isiyo nyeusi sana.
Wakati wa ujauzito, mstari huu 'hujitokeza' sana (huonekana zaidi) kwa sababu ya mabadiliko ya vichochezi (hormones) wakati wa ujauzito hasa ikisababisha na vichochezi vinavyotolewa na Kondo la nyuma (Placenta)...pamoja na hii rangi hii nyeusi ya mstari (nigra from word negro imaanishanyo nyeusi), huambatana na chuchu na sehemu inayoxunguka chuchu za mwanamke mjamzito kuwa nyeusi pia.
Baadhi ya wanawake (WENGI) hawaonyeshi kuwa na mstari huo, na kipimo cha 'kuzaa' au kutokuzaa hakipimwi kwa mstari huo.