Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 20,654
- 35,887
Upo msuguano wa dhahiri baina ya Spika na Rais. Spika ni kiongozi wa Bunge “Bunge” na Rais ni Kiongozi wa Serekali “Executive”. Wote ni Wakuu wa mihimili hapa anakosekana Jaji Mkuu ambae ni Mkuu wa Mahakama.
Ukizitazama kwa makini misuguano baina ya Rais na Spika utaona dhahiri kila mmoja anapenda kuonyesha ukuu wake na matamanio ya madaraka.
Tukiirejelea Katiba yetu ambayo Rais karundukiwa madaraka mengi,sioni ni namna gani Spika ataweza kupambana na Rais.
Rais anateuwa Mawaziri, Makaribu Wakuu,Wakuu wa Mikoa, Makatibu tawala wa mikoa, Wakuu wa Wilaya, Mabalozi, Majaji, Wakuu wa Mashirika ya Umma na Wenyeviti wa bodi za mashirika ya umma & Wakuu wote wa vyombo vya ulinzi na Usalama na mwisho kabisa anateuwa Wabunge kumi katika bunge la JMT.
Spika wetu yeye anateuwa Wenyeviti wa Kamati za Bunge na Wabunge 19 wasiokuwa na chama. Sasa kama ni mpambano Spika si lolote si chochote. Wateuzi wake wote hawana impact ya moja kwa moja kwa wananchi.
Spika Ndugai lazima atamke nimekosa nimekosa Mama nihurumie.
Ni hayo kwa leo
Ngongo kwasasa Kibanda Maiti.