Msuguano baina ya Spika na Rais ni ulevi wa madaraka

Msuguano baina ya Spika na Rais ni ulevi wa madaraka

Ndugai hana sababu ya kujiuzulu kwasababu tarehe 29/01/2021 atamkaribisha mh Rais Samia Suluhu Hassan mjengoni kwaajili ya maombi.

Tuvute subiri kiduchu nyama zipo chini.
 
Ndugai anaweza kumtoa rais kwa kuhamasisha kura ya kutokuwa na imani naye.

Udhaifu wa siasa zetu za upinzani wa kushindwa kutambua hakuna adui wala rafiki wa kudumu bali agenda ni mzigo.
Kumtoa rais sio rahis kama unavyo waza wewe aisee kifupi tu kasome katiba vizuri utaelewa
 
Upo msuguano wa dhahiri baina ya Spika na Rais. Spika ni kiongozi wa Bunge “Bunge” na Rais ni Kiongozi wa Serekali “Executive”. Wote ni Wakuu wa mihimili hapa anakosekana Jaji Mkuu ambae ni Mkuu wa Mahakama.

Ukizitazama kwa makini misuguano baina ya Rais na Spika utaona dhahiri kila mmoja anapenda kuonyesha ukuu wake na matamanio ya madaraka.

Tukiirejelea Katiba yetu ambayo Rais karundukiwa madaraka mengi,sioni ni namna gani Spika ataweza kupambana na Rais.

Rais anateuwa Mawaziri, Makaribu Wakuu,Wakuu wa Mikoa, Makatibu tawala wa mikoa, Wakuu wa Wilaya, Mabalozi, Majaji, Wakuu wa Mashirika ya Umma na Wenyeviti wa bodi za mashirika ya umma & Wakuu wote wa vyombo vya ulinzi na Usalama na mwisho kabisa anateuwa Wabunge kumi katika bunge la JMT.

Spika wetu yeye anateuwa Wenyeviti wa Kamati za Bunge na Wabunge 19 wasiokuwa na chama. Sasa kama ni mpambano Spika si lolote si chochote. Wateuzi wake wote hawana impact ya moja kwa moja kwa wananchi.

Spika Ndugai lazima atamke nimekosa nimekosa Mama nihurumie.

View attachment 2068769

Ni hayo kwa leo

Ngongo kwasasa Kibanda Maiti.
Leteni na ile ya kumuondoa rais kwa kura ya kutokuwa na imani naye
 
Mkuu wa muhimili mmoja ni Mwenyekiti wa Chama
 
Mkuu hicho kifungu kipo au hakipo?
Kipo lakini hatua zake ni ngumu sana kiutekelezaji.

Ngoja nitafute nitaliweka hapa soon.

Lakini Katibu wa Bunge ni mteule wa Rais !.Huyu atahusika pakubwa sana.

Rais ni Mwenyekiti wa Chama anaweza kulivunja bunge wakati linaandaa mkakati wa kumshtaki.
 
Rais anawashambulia wenzake hadharani sana. Waziri wa Kilimo yalishamkuta haya juzi tu. Leo ilikuwa zamu ya Ndugai na Kassim.
Tatizo ni katiba juu ya kifo na muda na ukomo wa kukaimu,huyu anakula faida ya udhaifu wa katiba lakini hakuchagiliwa na wajumbe,anatembelea nyota ya marehemu
 
Ndugai anaweza kumtoa rais kwa kuhamasisha kura ya kutokuwa na imani naye.

Udhaifu wa siasa zetu za upinzani wa kushindwa kutambua hakuna adui wala rafiki wa kudumu bali agenda ni mzigo.
Kwa vyovyote Ndugai ni mtetezi wa wapinzani
 
Unakosa adabu. Huwezi kumuita rais wa nchi kwamba ni mkuu wa muhimili. Kumlinganisha rais na jaji mkuu au spika ni kumkosea adabu jirekebishe.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Wasiwasi wangu ni kurudi kule kule kwenye serikali ya kusifu na kuabudu 24/7

Kila mtu atasifu na kuabudu, watabaki miamba wachache sana kama waliobaki enzi za uncle Magu (RIP)
 
Inashangaza sana wakubwa wanalumbana kuhusu 2025 badala ya kuhimiza kilimo cha umwagiliaji na wananchi kulima mazao ya muda mfupi kwa wingi.
Hiyo ndiyo CCM, uchaguzi ukiisha leo, kesho wanawaza uchaguzi ujao.
 
Umeeleza kirahisi sana, vita kati ya Raisi na Spika inategemea nani ana influence kubwa kwa wabunge. Ikiwa raisi ndio mwenye influence kubwa, anaweza kuhakikisha Ndugai hachaguliwi tena, ila Spika akiwa na ushawishi wa kutosha kwa wabunge, anaweza kumng'oa raisi madarakani kupitia impeachment.
Wewe ndio umeeleza kirahisi, unaishi bongo au Amerika?
 
Spika anaongea kihuni uliona wapi Nchi inapigwa mnada kama mashati ya mtumba na bado mnasema mpo na spika inawezekana alikua na maana nzuri ila kawasilisha kihuni sana...ametudharau sana ni vile Watanzania bongo zimelala angeongea mwingine angeitwa kwenye kamati yao ya maadili..
 
Back
Top Bottom