Msuguano baina ya Spika na Rais ni ulevi wa madaraka

Rais anawashambulia wenzake hadharani sana. Waziri wa Kilimo yalishamkuta haya juzi tu. Leo ilikuwa zamu ya Ndugai na Kassim.
Kesho zamu yako msituzinguwe
 
Katika nchi za kidemokrasi kazi ya spika kupitia bunge lake ni kuisimamia serikali na siyo kuibembeleza serikali. Kimsingi maneno ya Ndugai kuhusu mikopo yalikuwa sahihi kbs kwa mujibu wa majukumu yake kikatiba.
Sasa wanasema "what goes around comes around". Hii backlash yote dhidi ya kauli za ndugai ni mwendelezo wa kuminya demokrasi ambao akina ndugai wamepalilia kwa muda mrefu dhidi ya wapinzani ktk tanzania. Lissu aliwatabilia kitambo -"wakitumaliza sisi watawageukia ninyi ccm wenzenu". Ndugai ameendesha bunge kwa ubabe na ukandamizaji kwa wapinzani sasa mwacheni aonje matunda ya ukandamizaji aliopalilia hasa ktk awamu ya 5.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Tatizo ni katiba juu ya kifo na muda na ukomo wa kukaimu,huyu anakula faida ya udhaifu wa katiba lakini hakuchagiliwa na wajumbe,anatembelea nyota ya marehemu
Katiba mpya muhimu sana,hatupaswi kuisubirisha hata sekunde moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…