GE2025 Msukuma: Kocha akifanya vizuri anaongezwa mkataba, Tabasamu amefanya makubwa, mpeni Kura za Heshima

GE2025 Msukuma: Kocha akifanya vizuri anaongezwa mkataba, Tabasamu amefanya makubwa, mpeni Kura za Heshima

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku 'Msukuma' amesema wananchi wa Sengerema wanapaswa kumpa kura za heshima mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Hamis Tabasamu kutokana na mambo mengi makubwa ya kimaendeleo aliyowafanyia.

Msukuma amesema kocha anapofanya vizuri, anapaswa kuongezwa mkataba na kwamba Tabasamu amefanya mengi mazuri hivyo wananchi wamchague kwa kishindo.

Msukuma ameyasema hayo kwenye Uzinduzi wa Kampeni za CCM Jimbo la Sengerema, uliofanyika jana Jumapili, Septemba 21, 2025 katika Viwanja vya Stendi ya Zamani, Sengerema.

Pia Msukuma alitumia nafasi hiyo kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Samia Suluhu Hassan.

Viongozi mbalimbali walihudhuria uzinduzi huo, akiwemo Mwenyekiti wa CCM WIlaya ya Sengerema, Marco Makoye na mgombea ubunge wa Jimbo la Buchosa, Eric Shigongo.

 
Japo jamaa ni std 7 amejitahidi tofauti na mtangulizi wake Ngeleja ambae aliwahi kuwa waziri wa madini wilaya ilijaa ufisadi wa kutisha.
Wasomi tuna la kujifunza iweje tukipewa kazi tunachowaza ni matumbo yetu, natamani niione chadema ikiwala kabla sijalala mauti.
 
Back
Top Bottom