Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mbunge wa Geita, Joseph Musukuma kuhusu ubovu wa barabara na kilio cha wananchi:
"Jana kuna gari imepasua matairi pale kwenye Mlima Saranda... mtu mmoja akanitumia message ile gari ilivyo na matairi yake yalivyopasuka, halafu akaniambia, 'Nyinyi wabunge, yaani sisi tunahangaika na mashimo, ninyi mnatuletea Rio Ferdinand.' Ndio nani?"
"Na nimuombe Mheshimiwa Rais kama anatusikiliza; apande gari ya kupita kwa miguu (barabarani). Pengine labda wanamupitisha kwenye ndege haoni huku chini."
Kuhusu kuzuia bajeti hiyo isipitishwe hadi serikali itakapotoa majibu ya fedha:
"Mimi ningeshauri wabunge, sisi kama Bunge... leo tukipumzika saa saba, Waziri Mkuu ni wa kwetu humu ndani, Waziri wa Fedha yuko humu, wakakae waje hapa wakati tunahitimisha, watwambie hela zinaenda lini? Kwa sababu hela mshakusanya... Sasa tuzungumze nini sisi wabunge? Tuzungumze nini? ...Mimi nashauri, tusikubali kabisa kuipitisha hii budget, kabisa!"
"Mimi ni mwana-CCM, wapi tumefungwa kusema ukweli? Lazima tuwaombe, kama mnamshauri vibaya Mkuu wa Nchi basi mshaurini, tunahitaji pesa. Sisi tunaishi maisha ya barabarani, tunajua shida tulizonazo."
"Pesa mnakusanya, sheria tumetunga, halafu pesa haziendi. Ukienda kwenye account ya Road Fund leo mna bilioni 56 mwezi wa sita... Mnataka kuzipiga au mnataka kufanya nini? Achieni pesa tukatengeneze barabara za wananchi wetu!"