MSUKUMA: Sisi tunahangaika na mashimo barabarani, nyie mnatuletea Rio Ferdinand ndio nani?

MSUKUMA: Sisi tunahangaika na mashimo barabarani, nyie mnatuletea Rio Ferdinand ndio nani?

Mbunge wa Geita, Joseph Musukuma kuhusu ubovu wa barabara na kilio cha wananchi:

"Jana kuna gari imepasua matairi pale kwenye Mlima Saranda... mtu mmoja akanitumia message ile gari ilivyo na matairi yake yalivyopasuka, halafu akaniambia, 'Nyinyi wabunge, yaani sisi tunahangaika na mashimo, ninyi mnatuletea Rio Ferdinand.' Ndio nani?"

"Na nimuombe Mheshimiwa Rais kama anatusikiliza; apande gari ya kupita kwa miguu (barabarani). Pengine labda wanamupitisha kwenye ndege haoni huku chini."

Kuhusu kuzuia bajeti hiyo isipitishwe hadi serikali itakapotoa majibu ya fedha:

"Mimi ningeshauri wabunge, sisi kama Bunge... leo tukipumzika saa saba, Waziri Mkuu ni wa kwetu humu ndani, Waziri wa Fedha yuko humu, wakakae waje hapa wakati tunahitimisha, watwambie hela zinaenda lini? Kwa sababu hela mshakusanya... Sasa tuzungumze nini sisi wabunge? Tuzungumze nini? ...Mimi nashauri, tusikubali kabisa kuipitisha hii budget, kabisa!"

"Mimi ni mwana-CCM, wapi tumefungwa kusema ukweli? Lazima tuwaombe, kama mnamshauri vibaya Mkuu wa Nchi basi mshaurini, tunahitaji pesa. Sisi tunaishi maisha ya barabarani, tunajua shida tulizonazo."

"Pesa mnakusanya, sheria tumetunga, halafu pesa haziendi. Ukienda kwenye account ya Road Fund leo mna bilioni 56 mwezi wa sita... Mnataka kuzipiga au mnataka kufanya nini? Achieni pesa tukatengeneze barabara za wananchi wetu!"


View attachment 3592153
HEKO wabunge, hasa Msukuma, at least mmeanza kuelewa kuwa fedha za ROAD FUND zinatafunwa!
 
Naunga mkono hoja ,akili zaBashiteanazijua mwenyewe

kama unaamini yote ni maamuzi yake binafsi basi una safari ndefu sana, au umesahau kwamba raisi kikwete aliileta real madrid tanzagiza enzi akiwa raisi? tofauti iko wapi? and do you see the pattern?

mkiambiwa muslims wanaturudisha nyuma mnasema sijui udini, lkn matendo yao mnayaona na kila mwenye akili anaona kabisa kwamba wana wrong priorities na hawajui how to run a country, watu hawana maji, barabara mbovu, ajira hakuna ila fedha zote wanachezea kwenye anasa huku wananchi wakitaabika …

1779362025522.jpeg
 
Ishu ya Rio Ferdinand na Drogba ni ya kipuuzi sana. Mbaya zaidi Drogba na Rio kwenye social media zao hakuna walichopost kuhusu ziara zao. Kilichonikera ni kauli ya Msigwa kuwa Makonda ni rafiki sana na Rio kwahiyo Rio kaja kama rafiki wa Makonda. Alifika mbali kwa kusema Mayweather na Tyson pia ni marafiki wa Makonda. Mama aweke jicho kwa hawa watu wawili. Wanachokifanya ni kumchonganisha na wapiga kura.
 
Musukuma "done your research", let Rio enjoy good weza of Tanzania under mama.
 
kama unaamini yote ni maamuzi yake binafsi basi una safari ndefu sana, au umesahau kwamba raisi kikwete aliileta real madrid tanzagiza enzi akiwa raisi? tofauti iko wapi? and do you see the pattern?

mkiambiwa muslims wanaturudisha nyuma mnasema sijui udini, lkn matendo yao mnayaona na kila mwenye akili anaona kabisa kwamba wana wrong priorities na hawajui how to run a country, watu hawana maji, barabara mbovu, ajira hakuna ila fedha zote wanachezea kwenye anasa huku wananchi wakitaabika …

View attachment 3592258
Kwa malengo gani?
 
Ishu ya Rio Ferdinand na Drogba ni ya kipuuzi sana. Mbaya zaidi Drogba na Rio kwenye social media zao hakuna walichopost kuhusu ziara zao. Kilichonikera ni kauli ya Msigwa kuwa Makonda ni rafiki sana na Rio kwahiyo Rio kaja kama rafiki wa Makonda. Alifika mbali kwa kusema Mayweather na Tyson pia ni marafiki wa Makonda. Mama aweke jicho kwa hawa watu wawili. Wanachokifanya ni kumchonganisha na wapiga kura.
Mpaka hapo haijatusaidia kutangaza utalii
 
Pamoja na Std7 yake michango yake mingi ina mantiki na mashiko kuliko ma PhD holder uchwara hapo ndani
 
Kuna muda huwa nawaelewa wabunge wenye elimu ndogo bungeni[ baadhi yao], yaweza kuwa nature ya nchi yetu haihitaji watu wenye elimu.

Wasomi ndiyo masterminds wa mipango ya kuibia nchi kuliko akina msukuma. Huwezi kukuta darasa la 7 wapo nyuma ya mikataba ya wizi kama DP world, ngorongoro, BBT,n.k

Atleast darasa la 7 wanaweza point vitu vinavyoonekana kirahisi.

NOTE: kuna prof alifuata dawa ya kienyeji ya Corona😁
 
Usiwaamini hao, wakishamaliza kuponda wanaunga mkono hoja, akili zao wanazijua wenyewe.
 
Back
Top Bottom