Uchaguzi 2020 Msumari hatari kwa Mwigulu Nchemba

Uchaguzi 2020 Msumari hatari kwa Mwigulu Nchemba

Kosa lake kuu ni kukariri darasa la saba.
Hayo mengine yote ni 'yatokanayo'
Naona Pasko alimuuliza hilo swali hakujibu.

Anyways kila mtu ana siri yake ambayo asingetaka watu waijue.
 
Naona Pasko alimuuliza hilo swali hakujibu.

Anyways kila mtu ana siri yake ambayo asingetaka watu waijue.
Anaweza kuwadanganya watu wengine sio watu wa kata anayotoka mwigulu (kyengege)
 
Hili jimbo ni la Kitila Mkumbo basi tu CHADEMA 2015 walijikoroga kwa kuwafukuza na Zitto. Kitila kachukue jimbo lako uwakomboe wajomba zangu. Please Professor wajomba zangu wanakuhitaji.
 
Kama una taarifa zote hizo peleka Polisi waambie wamkamate wamshitaki.. Unatwambia sisi ili iweje?

Mlipokuwa mnashiriki naye hivyo vikao vya mauaji mbona ulikuwa kimya? Unatueleza leo ili iweje? Alivyotajwa kipindi kile cha mabomu Arusha mbona mlimtetea?

Upumbavu wenu Wa kujifanya mna huruuuma na Wananchi kipindi cha Uchaguzi pekee kawahurumieni Mama zenu.

Hamna M-CCM mwenye roho ya Ubinadamu hata mmoja. Wote ni mumiani, wanyonya damu.. Mkitofautiana kimaslahi ndiyo mnajifanya kujitokeza hadharani kuchafuana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
*MWIGULU UMEJIMALIZA MWENYEWE , USITAFUTE MCHAWI GIZANI*

Nimefuatilia sana mijadala hapa jukwaani kuhusu Mwigulu Nchemba kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020 Mwigulu akitamba kwa kujiita Mamba . Kwa tafsiri ya haraka Mamba ni mnyama anayeua binadamu na wanyama wengine bila huruma , kwa msiomjua Mwigulu halisi tulieni niwaeleze , ni kweli Mwigulu sio binadamu wa kawaida , ni mtu mwenye roho ya uuaji , roho mbaya , mwenye majivuno , mwenye majigambo , mwenye kulewa madaraka , mwenye tamaa na asiye na uzalendo wowote kiuhalisia . nasema haya kwakuwa nina uhakika nayo kwa kiasi kikubwa sana .

MWIGULU SIO KIONGOZI

Ukimfuatilia Mwigulu nyendo zake zote tangu alipoupata ubunge mwaka 2010 utakubaliana nami kwamba jamaa sio kiongozi anayeweza kuonyesha njia kwa watu wake badala yake amekuwa mwigizaji na mwenye kupenda sifa na kuabudiwa , mfuatulie anapozungumza amejawa ubabe na husuda nyingi . wananchi wa dunia Leo hawahitaji kuonyeshwa magofu ya madarasa na mabweni , haya ni mambo ya kawaida sana yanafanywa na Halmashauri . Mwigulu kwa miaka 10 hana mradi wowote wa kimkakati unaoweza kubadili maisha ya wananchi kiuchumi pamoja na yeye kujiita mchumi mbobezi . anachokifanya ni kujenga jamii ya kumwabudu kwa kuwakodi , kutembeza gari jimboni lenye mziki mkubwa likiwa linamwimba yeye na kumtukuza . hapendi kukosolewa kabisa anaweza kuua mtu asitudanganye hapa whatsaap .

*MWIGULU MIKONO YAKE INANUKA DAMU*

Kwa msiojua mambo ya gizani nawaonea huruma sana , Mwigulu huyu ananuka DAMU za watu ambao ni watanzania wenzetu , ameshiriki vikao vingi vya mipango ovu dhidi ya watanzania na mwenye vikao hivyo Mwigulu amenukuliwa akiweka option ya kuua watu akitumia neno USIBISHANE NA SHETANI .

Mwaka 2012 mmesahau ? mkutano wa chadema uliopigwa mabomu Arusha na watu kadhaa kuuawa ilikuwa ni mipango na pendekezo la Mwigulu akiwa naibu katibu mkuu wa ccm . alifanya kikao Arusha na vyombo vya Dola na kutoa pendekezo hilo tena kwa vitisho baada ya askari kushauri kwamba kutumia mabomu ya kivita kuua ni hatari kwa amani ya nchi yetu , Mwigulu ananukuliwa kumjibu kama hutaki kazi Vua sare . mwisho wa siku mkutano wa kufunga kampeni Arusha ulipigwa mabomu ya kivita na kumwaga DAMU za watu .
Uchaguzi mdogo Arumeru na Kalenga oparesheni zote za kudhuru na kuumiza watu ziliongozwa na Mwigulu , sio muumini wa democracy hata kwa sekunde moja , anaamini katika kuua ili ashinde .Rais Jakaya Kikwete hakupendezwa na mambo haya na kuonya kwamba Mwigulu anaenda ndivyo sivyo .

*MWIGULU NI MLA RUSHWA NA MWIZI*

Mwigulu akiwa waziri wa mambo ya ndani alifanya ufisadi mkubwa sana wa kukwapua pesa toka kwa makamanda wa polisi wa mikoa , alidai pesa kwa nguvu alizotumia kuwekeza kwenye team yake ya Singida United kwa lengo la kujikweza zaidi , alipotumbuliwa uwaziri na team ikafa . wakati Fulani Rais Magufuli amewahi kunukuliwa akihoji waziri anapata wapi mapesa ya kuanzisha team ya mpira ? Wakati yeye Rais hana uwezo huo . aje hapa aeleze alipata wapi pesa za kuendesha singida United na kwanini alipotumbuliwa team ikafa kifo cha mende ?

*MWIGULU ANA TAMAA ILIYOPITILIZA , UROHO , ULAFI NA UBINAFSI*

Wanaofikiri Mwigulu ni presidential material wako wrong kwa kiasi kikubwa sana , amepekuliwa vya kutosha sana na kubainika amejawa uroho hadi kutamani kupanga mipango ya kumpindua Rais aliyepo madarakani , Mwigulu alipoupata ubunge mwaka 2010 na kuingia bungeni akaanza harakati za Urais 2015 , akaunda genge la vijana ndani ya ccm kazi yao ikawa kumpamba na kumuimba mapambio yote ya uongo akiitwa Sokoine wa II , Mara field marshal na upuuzi mwingi ambao kiongozi makini hawezi kuufanya , rejeeni genge la akina JULIANA SHONZA, MTELA MWAMPAMBA , HABIBU MCHANGE , NYAKARUNGU na wengine wengi ambao Leo hii wamegeuka kumpinga Mwigulu hadharani kwakuwa wanamjua maujinga yake yote.

Baada ya mwaka 2015 alipofanya vurugu za kila aina Jimboni Iramba kwa kuiba mabox ya kura, rushwa na kuwakamata wagombea wenzake kwa kivuli chake cha Naibu waziri na kuwasweka ndani alifanikiwa kushinda kwa hila nyingi na kutamka kwamba yuko tayari kusikia watu wamevunjika miguu illi Mwigulu ashinde Ubunge .haya ametamka hadharani kabisa .

Akiwa waziri wa kilimo na baadaye waziri wa mambo ya ndani Mwigulu alianza harakati za kuutafuta URAIS kwa kuomba mialiko mingi ya shughuli za kidini na matukio mbalimbali hadi kuathiri utendaji wake wa kazi , akawa bize mno na mipango ya Urais na kujisahau kazi aliyopewa kumsaidia Rais , akaota sharubu na kujiona mwamba , akaonywa Mara kadhaa akajifanya jeuri , sasa anachati whatsaaap masaa 24 akiwa mbunge wa kawaida . akiwa waziri alikuwa hajibu meseji wala hachat whatsaap na simu alikuwa hapokei kabisa . maisha ni kama gwaride .

MWIGULU HAJASAIDIA WANA SINGIDA .

Huyu Mwigulu mnayemuona ana roho mbaya sana na hapendi kusaidia watu wa Singida , asiwazuge kwa kupiga picha na rundo la watoto wadogo ( fake life hiyo ) watu wengi wa Singida walijaribu kuomba msaada kwa Mwigulu alikataa kuwasaidia na hapokei simu , sizungumzii msaada wa fedha , msaada tu wa connection za ajira kwa vijana alikataa kutoa ushirikiano , wapo waliomuomba msaada tu mdogo wa uhamisho ndani ya wizara ya mambo ya ndani alikataa kabisa , alikuwa tayari kuwasaidia watu wa makete huko Iringa na kuwakana ndugu zake wa Singida.

Part 2.......nitaeleza jinsi Mwigulu anavyopanga mipango ya kuhamia upinzani endapo atapoteza nafasi ndani ya CCM , kwa sasa kimwili yuko CCM ila kiroho yuko upinzani .
Pumbavu sana, kwahiyo kutusaidia watu wa MAKETE,Njombe wewe kimekuuma sana. Mbinafsi kubwa wewe. Kwanza uelewa wako wa Jografia ya Tanzania ni ziro, Makete haipo Iringa.
 
KAMA HUMJUI MWIGULU NCHEMBA KAA KIMYA NI MTU MWENYE ROHO YA PEKE YAKE USIMLINGANISHE NA KITILA.

Sisi wanairamba tunayemjua tunakushangaa sana

Mwigulu ni mtu mwenye roho ya kipekee mno.

Nakumbuka Mwigulu alipokuwa anatafuta ubunge, alikuwa anatumia tax ya mtoto wa Kipakulo alipopata ubunge akawa dreva wake kwa muda, alipoteuliwa na chama na kupewa dreva wa Chama Mwigulu hakumuacha Ally na kumuambia aache udreva tax wa kuajiriwa akachague tax yake mpya showroom. Ally alichagua mwenyewe na mwigulu akailipia. Na kwa sasa Ally alipata zake connection anaendesha gari za halmshauri na maisha yanaendelea vizuri na familia yake.

Huyu Mwigulu alifundishwa na Mwl Malumbi mpaka akafaulu, alipoanza ubunge alikuta Mwl wake hana nyumba mwigulu akamnunulia nyumba mwalimu wake na iko makunda, sio wote wanaweza kufanya hivyo niambie ni nani huwa anakumbuka walimu wake?

Mwigulu alifundishwa darasa la kwanza na Mwalimu Mkumbo, alipougua Mwalimu Mkumbo huyo mwigulu alimpeleka kufanyiwa Matibabu India kwa zaidi ya miezi mitano na anaishi naye kama mama yake Mzazi, sio kila mtu ana roho kama hiyo.

Mwigulu aliwasaidia wasaidizi wake wa karibu wote wakapata nyenzo za kazi akina Sanga, Reuben wote magari, akina Mtela, Shonza, Kimeta, na wengine wachache niliowafahamu nikiwa msaidizi wake. Hata mimi siku hizi sifanyii kazi kitendea kazi cha kuazima. Ni nani alikuwa karibu na Mwigulu akashindwa kutimiza ndoto zake. Watu wengi huwa hawataki watu walio nao wapande juu lakini Mwigulu kapelekea vijana wengi watimize ndoto zao.



Mwigulu alikuwa anakuja na Mabati zaidi ya 1000 anawaita waislamu anawambia kaezekeni misikiti iliyofikia hatua ya kuezekwa. Hivyo hivyo kwa Makanisa, UKWATA SGD aliwapa NOAH mpya kabisa. Ni miongoni mwa watu ambao wamekuwa karibu sana na taasisi za kidini. Unaweza kusema ni jambo la kisiasa lakini wanasiasa ni wangapi na mbona wote hawafanyi hivyo?

Mwigulu amesomesha watoto sasa ni zaidi ya 300 na sio ndugu zake mpaka vyuo vikuu na sasa wako kwenye ajira, alikuwa anapewa mikutanoni tu. Wa ndugu zake ndio kabisaaaaaa, yeye ni baba wa wote, wote wako kwake na wanishi kwake. Unapomtembelea Mwigulu kwake huwezi kutofautisha watoto wake wan kuwazaa na wa wengine. Imekuwa ni familia ya watu wote. Nadhani watu wazima wenzangu tuna jambo la kujifunza kutoka kwa Mwigulu.



Mwigulu alipokuwa naibu Katibu Mkuu CCM alisaidia vijana wengi kupata ajira nimeshuhudia wakina Daudi Madelu, Julias, Peter, Mama Zingula, Khadija Magolanga Aunt Zuhura, Abel Makala, Mwimba mashairi wa singida,, Miraji Mtaturu, mbali na hao aliwasaidia baadhi kuingia serkalini kama Fadhili, Wilson na wengine wengi.

Mwigulu anapokuwa jimboni huwa anakuja analipa mchango kwa niaba ya Kijiji, Ameanzisha Miradi ya kujenga kama HOSTELS za sekondari za kila kata, ambapo kwa hii Singida hakuna anayefanya hivyo. Kambi za wanafunzi wahitimu anatoa chakula, sio kila mtu anafanya hivyo. Niambie ni nani anafanya hivyo kama siyo Mwigulu

Mwigulu hata kama hakujui, ukimwomba msaada Instagram anakuomba namba ya Mpesa, watu wengi hata hafahamiani nao kakutana nao kwenye mitandao ya kijamii mtu anaeleza shida yake na anatatuliwa. Kuna wakati mwingine unaweza ukakufuru kwa roho ya Mwigulu. Naomba tuongee machache huyu siyo wa kufananisha na mtu ambaye kwao alikimbilia kujenga kilabu cha pombe za kienyeji.

Ngoja tu niishie hapo ila ya Mwigulu ni mengi sana katika jamii aliyoyafanya, Acha kumchafua Mwigulu kama humjui, Hata hiyo lugha ya Mamba tatizo ni shule yako umefeli kutafasiri, maana yake ana nguvu kubwa sana jimboni kwa moyo wake huo, mithili ya MAMBA AWAPO KINA KIREFU CHA MAJI, Kwa elimu yako mtoa hoja usikute hata mithili huijui.

Unaongelea damu za watu, mbona waliopiga mabomu walipatikana na walikiri makosa? kwa akili zako mwigulu na kufahamika kote abebe bomu akapige mkutano? Ili apate nini? Tumia akili wewe jamaa za kuambiwa changanya zako.



KWA TAARIFA KITILA MKUMBO ANAYEKUTUMA KUMCHAFUA MWIGULU NDIO MIKONO YEKE INANUKA DAMU, WALIKUJA NA WENZAKE NDAGO WAKIWA KWENYE MKUTANO WA HADHARA WAKAMUUA JACKSON ALIYEKUWA AKIMTETEA MWIGULU, WAMEMCHOMA VISU MCHANA KWEUPE NA KITILA MKUMBO AKIWEPO MWENYEWE. NDIO MAANA HAKUBALIKI IRAMBA, KURA LABDA APATE MITANDAONI, IRAMBA ATAKUTANA NA MSIBA HUU. ASANTE MUNGU KWA AJILI YA MWIGULU, ALIMJENGEA NYUMBA MAMA MZAZI WA KIJANA ALIYEUWAWA, NA ANAISHI NA YATIMA WALE WALIOACHWA NA ANAWASOMESHA.
 
Back
Top Bottom