KWELI Msumbiji: Magaidi wamevamia Msafara wa Wanajeshi wa Tanzania na Lesotho

KWELI Msumbiji: Magaidi wamevamia Msafara wa Wanajeshi wa Tanzania na Lesotho

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Zipo taarifa zinadai kuwa Jeshi la Tanzania katika wilaya ya Nangade, Cabo Delgado waliingia kwenye mtego wa Magaidi katika kijiji cha Vondanhar, eneo la Palma. Aidha inadaiwa Jeshi la Tanzania lilikuwa likisafiri kwa magari ya kivita sambamba na jeshi la Msumbiji. Magari matatu ya jeshi la Tanzania yamechomwa moto na baadhi ya Silaha kuharibiwa.

Taarifa iliyotolewa na kikundi cha Kigaidi cha IS, imedai wamekamata baadhi ya Silaha ikiwemo Chinese Type 81-1 assault rifle pamoja na 12.7x108mm Type 54 HMG ya kwenye gari.

Zaidi inaelezwa kuwa haya ni magari ya JWTZ yapo chini ya himaya ya magaidi.

1669096815282.png

1669096826864.png
 
Tunachokijua
Msumbiji ilianza kupokea mashambulio ya kigaidi tangu Oktoba 17, 2017. Baadhi ya vyanzo vinaonesha Mashambulizi hayo yalikuwa na nia ya kupinga utamaduni wa magharibi, hata hivyo baadhi yameonesha nyuma ya mashambulizi hayo kuna suala la kiuchumi kwa kuwa mashambulizi yalianza miaka kadhaa baada ya kugundulika kwa gesi na rubi katika Jimbo la Cabo Delgado.

Jimbo la Cabo Delgabo ni jimbo la kaskazini mwa Msumbiji ambalo linapakana na mkoa wa Mtwara ulio kusini mwa Tanzania. Kwa sababu hiyo usalama wa Cabo Delgado ulionesha kuwa ni usalama wa Tanzania. Novemba 15, 2021, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan alitoa sababu ya kutoa majeshi ya Tanzania kwenda kusaidia kulinda amani nchini Msumbiji.

Majeshi ya Tanzania yaliingia nchini Msumbiji kwa makubaliano ya Mpango wa Jumuiya ya Nchi za kusini mwa Afrika (SADC) ambapo jumla ya nchi sita ziliazimia kutoa jumla ya askari 3000 kulinda amani eneo hilo, Tanzania ikiwa ni moja wa nchi hizo, nchi nyingine zikiwa ni Malawi, Afrika Kusini, Angola, Botswana na Zimbabwe.

Kuvamiwa na Maagaidi
Taarifa za askari wa Tanzania walioko Msumbiji kuvamiwa zilitufikia Novemba 19, 2022. Chanzo chetu cha uhakika kimefuatilia na kubaini kuwa uvamizi huu ulitokea tarehe 15 Novemba 2022 lakini hayo magari hayapo mikononi kwa Magaidi kama ilivyoripotiwa.

Aidha, Kutokana na unyeti wa jambo hili, hatutaweka taarifa za kina zaidi.
hakuna jambo baya kama kushtukiza hata marekani mwenyewe alishafanyiwa hivi na ubabe wake wote
 
MADAI
Zipo taarifa zinadai kuwa Jeshi la Tanzania katika wilaya ya Nangade, Cabo Delgado waliingia kwenye mtego wa Magaidi katika kijiji cha Vondanhar, eneo la Palma. Aidha inadaiwa Jeshi la Tanzania lilikuwa likisafiri kwa magari ya kivita sambamba na jeshi la Msumbiji
Watuachie magari yetu
 
MADAI
Zipo taarifa zinadai kuwa Jeshi la Tanzania katika wilaya ya Nangade, Cabo Delgado waliingia kwenye mtego wa Magaidi katika kijiji cha Vondanhar, eneo la Palma. Aidha inadaiwa Jeshi la Tanzania lilikuwa likisafiri kwa magari ya kivita sambamba na jeshi la Msumbiji...
Muhimu hakuna vifo wala majeruhi

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu hakuna wanajeshi waliopoteza maisha, ambush ilitokea kwa mbele na askari walikuwa wanatoka kuchukua maji walikuwa 24 tu ghafla ndio wakatokea kwa mbele hao jamaa na kuanza kushambulia msafara wa askari wetu...
hii sitaki kuisikia yani kakikundi kadogo hivio haka silaha magali kambi madawa chakula kanaazaje kusumbua nchi atimae nchi 5 kujikusanya kupeleka nguvu huko,nyiyi mko wengi fanya halaka mfute hako kakikundi
 
Hakuna kazi ngumu kama kupambana na adui anaye fanana na raia.
Ila sijajua tanzania infaidika vip kununua ugomvi ikiwa hatujui iwapo huenda hao magaidi wanazalishwa hapa Tanzania. na kuenda kupigana huko msumbiji. kwa sababu hao magaidi nimewahi kusikiliza video yao moja inaoneka wanaongea kiswahili pure kabisa cha hapa Tanzania.
tanzania tuko salama hakuna gaidi uganda zambia malawi kongo burundi rwanda kenya somali pote huko kuna watu wanaongea kiswahili kama cha tz lakini sio watzn
 
Mleta taarifa sijakuelewa, maana hujathibitisha kam ni taarifa ya kweli au uzushi hali umeileta ktk page ambayo ulitakiwa uwe na taarifa kamili ndo ulete hapa
hizo namba za magali yalio chomwa moto ni buludi sindio?
 
Nyie watz waga ni watu wang....ese tu na akili za kuku hampendi kabisa kuusikia ukweli wala kuujua ukweli sasa unabisha nini na wakati kuna askar zaid ya 10 maiti zao zimepokelewa leo airport na wameuawa kwenye iyo ambushi na bado kuna wengine wengi tu ambao ni majeruhi
picha tafadhari
 
Hebu tuongee ukweli...
Jeshi la kibongo ni la kichovu East Africa nzima...
Wanakula tu kodi zetu, kulala bure, kula bure na msharaha juu...
unawatukana watoto wa samia? ujui kuwa vita haina mcho
 
Ukweli ni kuwa ambush ilitokea.

Ambush mara nyingi adui anakusoma kwanza na anapiga pale anapoona panauma sana. Sasa kama msafara ulikua na magari na wanajeshi wapo loaded, physically seen, basi RPG itapigwa pale penye wengi as target sio mkubwa wa msafara bali askari wengi wafe....
akili yako nyingi sana nimechukua kiasi
 
hii sitaki kuisikia yani kakikundi kadogo hivio haka silaha magali kambi madawa chakula kanaazaje kusumbua nchi atimae nchi 5 kujikusanya kupeleka nguvu huko,nyiyi mko wengi fanya halaka mfute hako kakikundi
Buni hadithi sasa. Ambush unajua maana yake, hata mkeo akikuambush anakupiga kama mtoto. Vita sio movie kama za kina Rambo, ndio maana unaona Russia hajatimiza malengo kwa wakati Ukraine
 
Hebu tuongee ukweli...
Jeshi la kibongo ni la kichovu East Africa nzima...
Wanakula tu kodi zetu, kulala bure, kula bure na msharaha juu...
kazi yao kuonea na kutisha na kupasua matofali uwanja wa taifa......
Maiti zimepita Uwanja wa ndege kimyakimya.......
Hebu waangalie hawa hapa na mikwala yao lakini ni mafisi wakubwa..ni aibu sana
Halafu kila siku wanatuseveza eti wanalinda nchi ndio maana ina amani kumbe wabongo ni makondooo.... [emoji1787][emoji1787]

View attachment 2435030
Umelala ndani unalishwa chakula ujui watu wanafanya kazi gani. Unadiliki kudharau Jeshi la nchi yako. Huo ni utomvu wa nidhamu
INABIDI KILA MWANANCHI APITE UZALENDO KWANZA ILI KUITHAMINI NCHI YAKE MWENYEWE
 
Umelala ndani unalishwa chakula ujui watu wanafanya kazi gani. Unadiliki kudharau Jeshi la nchi yako. Huo ni utomvu wa nidhamu
INABIDI KILA MWANANCHI APITE UZALENDO KWANZA ILI KUITHAMINI NCHI YAKE MWENYEWE
kama wewe unalala nje hilo ni tatizo lako
siwezi thamini jeshi la wapumbavu, linalotumika kuwanyonya wananchi
 
kama wewe unalala nje hilo ni tatizo lako
siwezi thamini jeshi la wapumbavu, linalotumika kuwanyonya wananchi
Tukumbuke tulikotoka.
 
Back
Top Bottom