Msumbiji: Mchungaji afariki dunia akijaribu kufikia rekodi ya Yesu ya Siku 40

Msumbiji: Mchungaji afariki dunia akijaribu kufikia rekodi ya Yesu ya Siku 40

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Kudos Wadau.

Tunaendelea na vituko vya Walokole.

Mchungaji mmja aliyejulikana Kwa jina la Francisco Barajah wa huko Msumbiji amefariki akiwa kwenye mfungo wa siku 40 Akijaribu kuifikia rekodi ya Bwn.Yesu.

Nyie Wachungaji Yesu alikuwa ni roho nyie mnaigiza mambo yaliyo Nje ya uwezo wenu.

Hawa watu hawajifunzi tuu? Kuna Mwingine Nigeria alikufa Akijaribu kutembea kwenye Maji ya Bahari kama Yesu.Waajinga ndio waliwao acha wafe Kwa kukosa maarifa [emoji116]

----
Mchungaji Francisco Barajah wa kanisa la kiinjili la Santa Trindade katika jimbo la kati la Manica Msumbiji amefariki dunia baada ya kufunga kwa siku 40 akijaribu kufikia rekodi iliyofikiwa na Yesu kwenye Mlima wa Mizeituni wa Biblia.

Alifariki alipokuwa akitibiwa katika hospitali ya Beira ambako alihamishwa akiwa katika hali mbaya.

Baada ya siku 25 za kufunga, alikuwa amepungua uzito sana hadi hakuweza kusimama, kuoga au kutembea.

Siku kadhaa baadaye, kwa msisitizo wa ndugu na waumini, alipelekwa hospitalini lakini jitihada za kumrejesha kwenye afya hazikufaulu.

Waumini wa kanisa lake na majirani zake hawakushangazwa na mabadiliko hayo, kutokana na kupungua uzito na umbo lake kuharibika katika siku za hivi karibuni.
 
Mchungaji wa Msumbiji amefariki dunia baada ya kufunga kwa siku 40 akijaribu kufikia rekodi iliyofikiwa na Yesu kwenye Mlima wa Mizeituni wa Biblia.

Kifo cha Francisco Barajah, mchungaji na mwanzilishi wa Kanisa la Kiinjili la Santa Trindade katika jimbo la kati la Manica, kilithibitishwa Jumatano.

Alifariki alipokuwa akitibiwa katika hospitali ya Beira ambako alihamishwa akiwa katika hali mbaya.

Baada ya siku 25 za kufunga, alikuwa amepungua uzito sana hadi hakuweza kusimama, kuoga au kutembea.

Chanzo: BBC Swahili

Kuna Lori Moja la Mchanga Mbuyuni Tegeta limeandikwa IGA UFE nilikuwa sielewi maana yake ila sasa nimeelewa.

Mmeshaambiwa Kiimani Yesu Kristo hakuwa Binadamu wa Kawaida na Wengine wakisema ni Mungu halafu Mpuuzi Mmoja tu tena Binadamu Mwenzetu ameshashiba zake Makande na Maji ya Kandoro anataka Kumuiga kwa Kufunga Siku 40 bila Kula chochote kwanini Usife?

R.I.P Mchungaji.
 
Mbona wapuuzi kibao wanakufa Kwa ugoni,ulevi,hamtangazi?au hiyo ndio mwaona hoja kubwa
 
Back
Top Bottom