Msumbiji: Mchungaji afariki dunia akijaribu kufikia rekodi ya Yesu ya Siku 40

Msumbiji: Mchungaji afariki dunia akijaribu kufikia rekodi ya Yesu ya Siku 40

haya majitu ni majinga sana, na kwingineko huko yanauza hata mafuta ya alizeti wanayaita mafuta sijui ya mapako sijui nini , na wajinga wanawakubalia kabisaaaa. UKISHINDA unaua mipumbaf hata miaka mia kamwe hayaishi kabisaaaaa
 
fake news Ndugu zake wamekanusha amekufa kwa presha
Kudos Wadau.

Tunaendelea na vituko vya Walokole.

Mchungaji mmja aliyejulikana Kwa jina la Francisco Barajah wa huko Msumbiji amefariki akiwa kwenye mfungo wa siku 40 Akijaribu kuifikia rekodi ya Bwn.Yesu.

Nyie Wachungaji Yesu alikuwa ni roho nyie mnaigiza mambo yaliyo Nje ya uwezo wenu.

Hawa watu hawajifunzi tuu? Kuna Mwingine Nigeria alikufa Akijaribu kutembea kwenye Maji ya Bahari kama Yesu.Waajinga ndio waliwao acha wafe Kwa kukosa maarifa [emoji116]

----
Mchungaji Francisco Barajah wa kanisa la kiinjili la Santa Trindade katika jimbo la kati la Manica Msumbiji amefariki dunia baada ya kufunga kwa siku 40 akijaribu kufikia rekodi iliyofikiwa na Yesu kwenye Mlima wa Mizeituni wa Biblia.

Alifariki alipokuwa akitibiwa katika hospitali ya Beira ambako alihamishwa akiwa katika hali mbaya.

Baada ya siku 25 za kufunga, alikuwa amepungua uzito sana hadi hakuweza kusimama, kuoga au kutembea.

Siku kadhaa baadaye, kwa msisitizo wa ndugu na waumini, alipelekwa hospitalini lakini jitihada za kumrejesha kwenye afya hazikufaulu.

Waumini wa kanisa lake na majirani zake hawakushangazwa na mabadiliko hayo, kutokana na kupungua uzito na umbo lake kuharibika katika siku za hivi karibuni.
 
siku 25 bila kula ni nyingi sana.
Mi mwenyewe nasema Kamanda kaupiga mwingi sana, na ni vizuri sana kufa ukipambania amani ya roho kuliko kufia juu ya kinena ukiwa umepakaa vumbi la Kongo.

Pia hata hizo siku 25 ni imani imara ndiyo iliyomfikisha hapo, la sivyo hata wiki 1 tu asingetusua [emoji3]
 
Kuna rafiki yangu huku Mwanza..kapata madonda ya tumbo yanamtesa sana...ni baada ya kufunga kwa siku 7 mfululizo mwaka jana

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
Imani dhaifu sana hiyo, watakatifu wa Mungu tunagonga hadi siku 14, 21 bila kula hata kunywa maji na hakuna ugonjwa wowote.

Wakuu kuishi katika utakatifu wa MUNGU kunahitaji imani haswaa wala si wale wapuuzi wanaodanganya kuwa kwa Mungu ni tambarare.
 
Mi mwenyewe nasema Kamanda kaupiga mwingi sana, na ni vizuri sana kufa ukipambania amani ya roho kuliko kufia juu ya kinena ukiwa umepakaa vumbi la Kongo.

Pia hata hizo siku 25 ni imani imara ndiyo iliyomfikisha hapo, la sivyo hata wiki 1 tu asingetusua [emoji3]
Angekua mzungu angewekwa kwenye kumbukumbu ya dunia,kukaa muda mrefu bila kula.
 
Back
Top Bottom