Msumbiji Wamekodisha Bandari ya Nacala Kwa Malawi & Zambia Kwa Miaka 100. Tanzania Kupoteza Mteja namba 2 wa Dar Port

Una hoja za msingi....lakini pia umeweka hofu zaidi....
1.DRC atabaki kuwa mteja wetu for 50 years more
  • Miji Tajiri kwa madini(Katanga,Tangayika na Kasai) ipo karibu zaidi na Tanzania kuliko Kenya....
  • Corridor ya Kaskazini Mashariki ndiyo ina vita
  • Kutoka Kongo Kusini kwenda Kaskazini,Jiografia ni Korofi,,,Misitu mikubwa matawi ya Mto Kongo ni mengi mno
  • Kumbuka pia,hata DRC imegusa bahari
2.Zambia
  • Wanacho kifanya ni kuondoa utegemezi wa nchi moja, siyo kwamba kuachana na Tanzania moja kwa moja,,,hiyo ipo hata kwa Uganda,anatumia Bandari zote mbili,za Kenya na Tz.
  • Pia Kumbuka ,Akitolea Msumbiji, inabidi ajiandae na kodi za nchi mbili,Msumbiji na Malawi,,wakati huku mzigo wote unapitia nchi moja.
3.Angola
  • Hawezi kutupora mteja kwani ,Afrika tunategemea mizigo from Asia kuliko Amerika

Bandari zetu bado zitahitajika....tu
 
Ilifika
Ngonjera au siyo? Mda utasema.Tutafika mahala Bandari zetu zitakuwa zinategemea zaidi mzigo wa ndani ya Nchi zaidi kuliko wa Nje ya Nchi kama ilivyo Sasa hivi.
Ikifikia huko ina maana tutakuwa tumeendelea sana kiuzalishaji....and it's a good thing.
 
Mkuu hao DP World kabla ya kuwekeza hapa Tanzania walifanya upembuzi yakinifu, hapo msumbiji Beira port wao wapo. Hiyo Bandari ya Banana wanajenga na wamelenga mizigo yote inayopita Atlantic ocean.

Nilibahatika kukutana Director mmoja wa DP World anasema Target yao kubwa kuwa operators wa bandari zote upande Africa pia Mombasa Port wameiweka kwenye target ya kuichukua. Hapo Somalia tayari DP World anafanya kazi
 
Tukubali kwamba hatuna guts na uwezo wa kuona fursa za kiuchumi mapema na intelligence ya kuzifikia.
Huyu mchechu ndio tumempa mambo ya planning na yeye ukufuatilia kariba yake ni uongozi wa mabenk na kujineemesha yeye mwenyewe.
 
Mwaka 2019 DP world waliingia Rwanda na kuanzisha Economic Processing Zone na Logistics Centre. Hawafanyi kwa kubahatisha kuipata Dar Port ni mafanikiko, hiyo mizigo ya Congo,Malawi,msumbiji,Zambia tayari wanahudumia kupitia Beira
 
Bandari si ya Tanzania Bali ya AUE
 
Ngonjera au siyo? Mda utasema.Tutafika mahala Bandari zetu zitakuwa zinategemea zaidi mzigo wa ndani ya Nchi zaidi kuliko wa Nje ya Nchi kama ilivyo Sasa hivi.
Hii sio sahihi, tayari DP world yupo Rwanda na logistics centre. Mizigo ya Rwanda na Kongo mashariki kaweka mazingira ya kuja Dar.

Dp world sio nchi zenye bandari tu ndio anawekeza, anawekeza mpaka Land Locked countries kwa kuweka vituo vya Logistics
 
Mwaka 2019 DP world waliingia Rwanda na kuanzisha Economic Processing Zone na Logistics Centre. Hawafanyi kwa kubahatisha kuipata Dar Port ni mafanikiko, hiyo mizigo ya Congo,Malawi,msumbiji,Zambia tayari wanahudumia kupitia Beira
Kagame aliifungua hiyo economic zone mwaka jana, walishajipanga kwa muda mrefu kwamba mzigo huo wote ni lazima upitie bandari ya Dar kwenda huko nje.

Hiyo ni logistic chain nzima kaishikilia DPW, hivyo anayehoji kwanini tenda haijatangazwa huyo hafahamu kuhusu DPW kuwa tayati anayo economic zone huko Rwanda tangu mwaka 2019.

Tenda aliyopewa DPW ya kuendesha magati ya TPA iliangalia mchakato mzima wa kuutoa huo mzigo Rwanda na kuupitisha kwenye bandari ya Dar kisha ukaenda huko kwa mteja wa mwisho.
 
Umeandika points nyingi. Safi sana. Mimi nadhani pia DP World waanze na jambo dogo sana la kutoa mizigo bandarini kwa haraka. Kwa sasa mzigo kutoka inachukua hadi wiki 3 tangu meli kufika Tanzania. Inashangaza kwasababu tuliambiwa ingechukua muda mfupi zaidi. Bandari ya Nacala ni tishio ila maboresho yakifanyika bado TZ haitayumba kibiashara. Bandari ya Mtwara ikifanyiwa kazi itasambaratisha hilo suala la Nacala.
 
angola nao wamejenga reli kutoka lubumbashi hadi Lobito tayari shehena ya kwanza ya shaba kwenda us imeshawasili bandarini salama, halafu sisi tuko busy na wamasai wa ngorongoro
Ile itaisha 2029, wanaiboresha...maumivu ni makali
 
Mkuu suala la mzigo kuchukua wiki 3 nadhani sio upande wa DP World. Anayekuchelewesha ni agent wako
 
Issue sio viongozi, ila jamii ya watanzania ni wajinga sana. Tumeona wasomi hata wa kiwango cha PhD wameongopeana sana kuhusu mkataba wa Bandari hapa hadi unajiuliza kama usomi wetu una maana gani. Unadhani ingetokea Tanzania ndio imekodisha bandari ya Mtwara kwa Malawi au Zambia au Congo hizo kelele pangetosha kweli?

Kiukweli tuna kundi kubwa tu la wasomi halafu wajinga nchi hii. Wanachojua ni kuiba hela halafu kunywa pombe na kuiba wake za watu au wanachuo. Angalia kelele za Ngorongoro, ni ujinga wa kundi hilohilo la wasomi. Ni ngumu sana kufanya radical reforms katika nchi yetu tofauti na tunavyodhani.
 
Imagine Tanzania ndio ingekuwa imekodisha bandari ya Mtwara kwa nchi hizo, hali ingekuwaje? Wanaharakati fake wangekuwa wamepata hoja ya kupayuka mwezi mzima.
 
Mtanzania anataka afanye kazi ya milioni mbili apokee mshahara wa milioni kumi. Ufahari mwingi wa kijinga na ujuaji kwenye maongezi ya kawaida tu.

Suala la bandari limewaaibisha sio wasomi wa fani nyingine pekee yao mpaka wanasheria tena waalimu wa pale Mlimani wa muda mrefu. Wakajikuta wakiwadanganya watanzania wengi wenye elimu ndogo na kuwapotosha juu ya ukweli wenyewe wa suala husika.
 
Nacala port,Beira no zipo upande wa Atlantic?
 
Ujinga tuu umewajaa watu wasioelewa
Kuna wakati tunalaumu viongozi ila kuna watu hata hawako Serikalini lakini wana nguvu ya kujaza ujinga kwa watanzania hadi unashangaa. Tuna akili za muda mfupi sana. Kila kitu chenye long term impact kinapingwa.

Angalia program ya BBT imavyopingwa kwa ujinga. Tutawezaji kufikia kilimo cha maana kama hujaanzisha programs za kuwa na mashamba makubwa yenye miundombinu yote. To be honest, tuna ujinga mwingi sana kama nchi.
 
Mwaka 2019 DP world waliingia Rwanda na kuanzisha Economic Processing Zone na Logistics Centre. Hawafanyi kwa kubahatisha kuipata Dar Port ni mafanikiko, hiyo mizigo ya Congo,Malawi,msumbiji,Zambia tayari wanahudumia kupitia Beira
Mimi Sina tatizo na Rwanda na Burundi,hizo ni lazima watumie Dar Port Kwa sababu ndio njia fupi kwao,swala ni DRC na Zambia.

Kwa Zambia Bandari za jirani kwake ni Nacala,Beira na Lobito the same applies to DRC.

Wanatumia Dar Kwa sababu ya kukosa ufanisi kwenye Bandari hizo za Mozambique na kama ujiavyo so far wateja wakubwa wa Tanzania ni Zina na DRC
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…