Msumbiji Wamekodisha Bandari ya Nacala Kwa Malawi & Zambia Kwa Miaka 100. Tanzania Kupoteza Mteja namba 2 wa Dar Port

Msumbiji Wamekodisha Bandari ya Nacala Kwa Malawi & Zambia Kwa Miaka 100. Tanzania Kupoteza Mteja namba 2 wa Dar Port

Mkuu, sisi wenyewe tunashindwa kusimamia mipango yetu: Leo stand ya mabasi ya Magufuli haina tofauti na stand zingine, kama ya Kibaha maana zote mabasi yanapita tu hadi mwisho wa safari zao za Ubungo, Urafiki, Manzese hadi Kariako n.k; siku hizi kituo cha Magufuli ni transit tu. Serikali imetumia fedha nyingi kwenye project hii, lakini matumizi yake yanafikirisha.
Ndio hasara ya kukurupuka na kutochukulia jambo Kwa umaskini unaotakiwa.

Stendi sio kitu Cha kuweka mabilioni bila sababu za msingi
 
Hiyo Nacala(Nashala) kasikazini ya msumbiji kuna miji ya Mpemba na Palmas hayo maeneo yana reli inayotoka Nashala hadi Nampula kwahiyo kwenda Malawi ni kuongezea tu kutoka Nampula hadi Bulawayo/Lilongwe huko Malawi. Hii imekaa vizuri kwa Malawi/ Zambia na ni Mbaya kwa Tanzania. Changamoto. 1. Msumbiji ina waasi wa IS wameenea kasikazini ya nchi katika maeneo hayo ya Palmas, Pemba, Nashala, Montpuez, na na Nampula kiuslama ni changamoto kwa mradi. 2. Msumbiji ina changamoto z kiusalama katika eneo lake na mpaka na Malawi jimbo la NIASA ambapo reli inapita, kuna Waasi wa RENAMO kiongozi wao Dracama, wanaopingana na FRELIMO. 3. Mizigo mingi kwa nchi za Afrika inatoka Bahari ya Hindi China, India, Japan sasa ili meli ifike bandari ya Nacala lazima ipite Afrika mashariki kijiografia (Mombasa na Dar Es Salaam) kwahiyo Tanzania ina nafasi kibiashara. 4. Mozambique na Malawi ni maskini hasa, na ni wavivu wa kufanya lobbying za kutafuta na kufanya miradi mikubwa kwahiyo mpaka mradi ufike Zambia labda ni 2050 ambapo sisi tutakua hatua nyingine. 5. Tanzania itengeneze bomba la gas ya LPG, liende Malawi, Zambia, Zimbabwe, Botswana, South Afrika, Congo ,Burundi, Rwanda, pamoja na kiwanda cha LPG, hii itamuahi Mozambique maana Mozambique ana kiwanda tayari cha LPG pale Palmas ila hajapata akili ya kusambaza kwa waafrika wenzie, gas inaripa ukisambaza kwa jirani zako angalia Urusi na Qatara wanavyofanikiwa. 6. Tanzania iwekeze SGR kwenda Burundi, Rwanda na Congo tu, hao ndio wateja walio kiganjani kwetu, Uganda tumuachie Kenya, Malawi tumuachie Mozambique sio kutaka kila nchi uchukue wewe hiyo sio Uafrika. 7. Tujenge uchumi wa Tanzania na miundombinu yake, kwa ajili ya Tanzania na watu wake, si kwa ajili ya kuipata nchi fulani, maana biashara hubadilika, lakini ustawi wa nchi ubaki pale pale, kwahiyo Mozambique kuipa bandari Malawi huo ndio Uafrika, Tanzania haitaji kujitukana na kujilaumu.
umeongea point muhimu sana hatuwezi taka kila kitu kiwe kwetu, hata hiyo Lobito ni kwa ajili ya mizigo inayoenda marekani kwa maana ya kupita bahari ya atlantic ilakwa dunia ya sasa mizigo mingi inaenda asia hivyo bado hiyo copper itaendelea pita kwenye bahari ya hindi
 
Benguela railway tayari marekani ameingiza mkono anaijenga, copper ya congo kwenda USA itakuwa inasafirishwa KUTOKEA lubumbashi to Lobito by railway...ni maumivu...na KUTOKEA Dar port to Lubumbashi ni mbali kulinganiaha na Lobito to Lubumbashi. Yote hii imesababishwa na msongamano na ufanisi wa hali ya chini katika bandari za Africa mashariki
mzigo wa copper unahitajika kwa wingi kwenda bara la asia kuliko marekani alichokifanya marekani ni kutaka kumuovateki mchina ili apate madini hayo kwa wingi kumbuka marekani huyo ametaka reli iunganishwe na huo mradi ili aweze kuchukua nickel iliyopo kabanga (ngara )kwenda lobito
 
-Nirahisi sana kuwa kama Kagame, na ikawaona IS kama ndugu zako!,
Chadema watu wa negativity kwa taifa watapiga nderemo na vigelegele!
 
-Nirahisi sana kuwa kama Kagame, na ikawaona IS kama ndugu zako!,
Chadema watu wa negativity kwa taifa watapiga nderemo na vigelegele!

..miundombinu sio suala la Ccm vs Chadema.

..hata tukiwa na serikali ya TLP bado miundombinu itajengwa.

..hata wakoloni walijenga reli, bandari, ambazo leo tunaziboresha.

..kwa kifupi hakuna serikali isiyojenga miundombinu. Na miundombinu sio miliki ya chama cha siasa, au kiongozi fulani.
 
Hufahamu ya kuwa serekali yetu inapopata makwazo chadema hufurahia?
 
Kuishauri serikali ya CCM ni kupoteza muda wako tu...

Hao watu hawana akili ya kuhifadhi maarifa wanayoshauriwa...
 
Hufahamu ya kuwa serekali yetu inapopata makwazo chadema hufurahia?

..Na Chadema inapopata makwazo watu wa serikali hufurahia. Je, unafahamu?

..Pia kuna baadhi ya watu serikalini wanajihusisha na matukio ya utekaji, utesaji, na mauaji, dhidi ya wafuasi wa Chadema. Je, unaunga mkono?
 
Hii habari yako ni ya uongo. Nacala port haijakodishwa kwa Malawi kwa miaka 100. Na pia haijakodishwa tu
Malawi wamepewa eneo nje la kujenga terrminal tu

Hata huku Tanzania tuna Malawi cargo, tuna Zamcargo(zambia)
 
Kwa diplomasia ya uchumi najaribu kufikiri hivi:

Ni serikali ya Malawi na Zambia ndizo zinazokwenda kuwekeza hapo Nacala ?!!

Je nchi hizo mbili zitatoa zabuni kwa makampuni ya kigeni kuwekeza hapo kwa miaka 100?!!
Hii habari ni ya uongo, bahati mbaya kabisa mmeijadili kwa ukubwa. Jf hakuna watu makini?
 
Hiyo Nacala(Nashala) kasikazini ya msumbiji kuna miji ya Mpemba na Palmas hayo maeneo yana reli inayotoka Nashala hadi Nampula kwahiyo kwenda Malawi ni kuongezea tu kutoka Nampula hadi Bulawayo/Lilongwe huko Malawi. Hii imekaa vizuri kwa Malawi/ Zambia na ni Mbaya kwa Tanzania. Changamoto. 1. Msumbiji ina waasi wa IS wameenea kasikazini ya nchi katika maeneo hayo ya Palmas, Pemba, Nashala, Montpuez, na na Nampula kiuslama ni changamoto kwa mradi. 2. Msumbiji ina changamoto z kiusalama katika eneo lake na mpaka na Malawi jimbo la NIASA ambapo reli inapita, kuna Waasi wa RENAMO kiongozi wao Dracama, wanaopingana na FRELIMO. 3. Mizigo mingi kwa nchi za Afrika inatoka Bahari ya Hindi China, India, Japan sasa ili meli ifike bandari ya Nacala lazima ipite Afrika mashariki kijiografia (Mombasa na Dar Es Salaam) kwahiyo Tanzania ina nafasi kibiashara. 4. Mozambique na Malawi ni maskini hasa, na ni wavivu wa kufanya lobbying za kutafuta na kufanya miradi mikubwa kwahiyo mpaka mradi ufike Zambia labda ni 2050 ambapo sisi tutakua hatua nyingine. 5. Tanzania itengeneze bomba la gas ya LPG, liende Malawi, Zambia, Zimbabwe, Botswana, South Afrika, Congo ,Burundi, Rwanda, pamoja na kiwanda cha LPG, hii itamuahi Mozambique maana Mozambique ana kiwanda tayari cha LPG pale Palmas ila hajapata akili ya kusambaza kwa waafrika wenzie, gas inaripa ukisambaza kwa jirani zako angalia Urusi na Qatara wanavyofanikiwa. 6. Tanzania iwekeze SGR kwenda Burundi, Rwanda na Congo tu, hao ndio wateja walio kiganjani kwetu, Uganda tumuachie Kenya, Malawi tumuachie Mozambique sio kutaka kila nchi uchukue wewe hiyo sio Uafrika. 7. Tujenge uchumi wa Tanzania na miundombinu yake, kwa ajili ya Tanzania na watu wake, si kwa ajili ya kuipata nchi fulani, maana biashara hubadilika, lakini ustawi wa nchi ubaki pale pale, kwahiyo Mozambique kuipa bandari Malawi huo ndio Uafrika, Tanzania haitaji kujitukana na kujilaumu.
Tanzania itengeneze bomba la LPG liende Zambia, malawi, drc? Mkuu umetoa maoni pengine ya jambo ambalo hulifahamu

Unaifahamu LPG ni nn? Na Tanzania tunaitoa wapi?
 
Tanzania bado itabaki kuwa njia salama zaidi katika maswala ya Bandari kutokana na hali za kiusalama
Tuzungushe ukuta bandari zote kama mererani kuongeza usalama, tutapata wateja mpaka tububujikwe na machozi ya furaha.
 
Una hoja za msingi....lakini pia umeweka hofu zaidi....
1.DRC atabaki kuwa mteja wetu for 50 years more
  • Miji Tajiri kwa madini(Katanga,Tangayika na Kasai) ipo karibu zaidi na Tanzania kuliko Kenya....
  • Corridor ya Kaskazini Mashariki ndiyo ina vita
  • Kutoka Kongo Kusini kwenda Kaskazini,Jiografia ni Korofi,,,Misitu mikubwa matawi ya Mto Kongo ni mengi mno
  • Kumbuka pia,hata DRC imegusa bahari
2.Zambia
  • Wanacho kifanya ni kuondoa utegemezi wa nchi moja, siyo kwamba kuachana na Tanzania moja kwa moja,,,hiyo ipo hata kwa Uganda,anatumia Bandari zote mbili,za Kenya na Tz.
  • Pia Kumbuka ,Akitolea Msumbiji, inabidi ajiandae na kodi za nchi mbili,Msumbiji na Malawi,,wakati huku mzigo wote unapitia nchi moja.
3.Angola
  • Hawezi kutupora mteja kwani ,Afrika tunategemea mizigo from Asia kuliko Amerika

Bandari zetu bado zitahitajika....tu
1. Usikariri mambo hubadilika, hiyo njia uliyosema sio salama ndio kwa sasa imeomgeza importation za mizigo kwa zaidi ya 200% kupitia bandari ya Mombasa

Nchi ambayo Tz ilipaswa kuconcetrate nayo zaidi ni Uganda, hizi nchi ambazo zinapitisha mizigo yao hapa Tanzania kupitia bandari bado zote hazijafilia ukubwa wa mizigo ambayo Uganda inapitisha Kenya
 
Mimi Sina tatizo na Rwanda na Burundi,hizo ni lazima watumie Dar Port Kwa sababu ndio njia fupi kwao,swala ni DRC na Zambia.

Kwa Zambia Bandari za jirani kwake ni Nacala,Beira na Lobito the same applies to DRC.

Wanatumia Dar Kwa sababu ya kukosa ufanisi kwenye Bandari hizo za Mozambique na kama ujiavyo so far wateja wakubwa wa Tanzania ni Zina na DRC
Rwanda na Burundi lazima wapitishe mizigo yao Bandari ya Dar? Hujui tu unachosema
Rwanda kaongeza idadi ya kupitisha mizigo bandari ya Mombasa kwa zaidi ya asilimia 400%

Mizigo anayopitisha Mombasa kwa sasa imeshoot juu kabisa
 
Sababu ni za ufanisi na sio umbali ila kwa.kigezo Cha umbali ni lazima.

Pamoja na hayo, ukweli unabakia pale pale kwamba mzigo mkubwa wa Rwanda na Burundi unapitia Tanzania.
 
Sababu ni za ufanisi na sio umbali ila kwa.kigezo Cha umbali ni lazima.

Pamoja na hayo, ukweli unabakia pale pale kwamba mzigo mkubwa wa Rwanda na Burundi unapitia Tanzania.
Mkuu umeelewa ulichoandika mwanzo na unachoandika hapa?

Umesema Rwanda na Burundi lazima wapitishe mizigo yao Dar port, mm nimekuambia sio kweli na nikakutolea mfano kuwa Rwanda imeongeza kutumia bandari ya Mombasa kwa mizigo kwa zaidi ya 400%

Unasema ni ufanisi na sio umbali. Kwan issue ni ufanisi umbali au issue Ni Rwanda kutokua na ulazima uliosema?

Pia hii post uliyoweka kuhusu hiyo bandari kupewa Malawi kwa miaka 100 sio ya kweli. Mara nyingi nakuambia acha kuandika UONGO
 
Nchi ya Mozambique imeamua kuteka biashara ya Usafirishaji Kwa njia ya Maji Kwa Nchi zote za Sadc na kuiachia Tanzania maumivu makubwa.

Katika kutekeleza Hilo, Mozambique wameamua kuikodisha Bandari Yao ya Nacala Kwa Nchi ya Malawi na Zambia ambapo wataitumia Kwa kipindi Cha miaka 100 ijayo.

Nchi hizo 3 zinapanga kujenga miundombinu ya reli kutoka Nakala Hadi Mji Mkuu wa Malawi Lilongwe na kisha Hadi Mji Mkuu wa Zambia Lusaka.

Njia hiyo Mpya ya reli itapunguza umbali wa Zambia kuifikia Bandari ya Dar hivyo zaidi ya asilimia 90% ya mzigo wa Zambia utapitia Bandari za Msumbiji za Nakala na Beira.

Kwa hatua hiyo itakuwa ni pigo kubwa sana kwa Tanzania ambayo Bandari ya Dar ilikuwa inategemea zaidi mzigo wa Nchi ya Congo DRC na Zambia kama wateja Wakuu huko Nchi zingine zikiongesea ongezea shehena.

Endapo Zambia itaondoka rasmi kuwa mteja wa Tanzania sio tuu itapunguza mzigo wa Bandari ya Dar Bali itaua kabisa biashara ya Malori ya mizigo Tanzania ambapo Kwa sehemu kubwa yatahamia Nchi hizo za Zambia,Malawi na Msumbiji na zingine za Afrika Ili kuendelea na Biashara ya Usafirishaji.
View attachment 3080432

Pia soma: Bandari za Dar na Mtwara Kuwa Mashakani Kutokana na Nchi za Zambia,Malawi na Mozambique Kuzindua Upanuzi Mkubwa wa Miundombinu ya Nacala Port.

Kwa maelezo zaidi soma hapa Ili Kuongeza Ufanisi wa reli ya TAZARA,Tanzania na Zambia Ziiombe China Wajenge reli Mpya ya Makambako-Mtwara & Kasama-Lubumbashi/Likasi

Ushauri,;

Serikali ihakikishe mipango yetu yote Kwa Sasa iwe inalenga kuikumbatia DRC kuanzia Kusini Hadi Kaskazini maana ndio mteja pekee ambae walau jiografia inatupa nafasi.

Serikali ifanye yafuatayo
1.Lazima tujihusishe na kutafuta amani directly ndani ya DRC Ikibidi Kwa gharama zetu.

2.Lazima Sgr na Barabara zivuke na kuifikia DRC(Bukavu,Goma,Kinshasa,Kindu)

3.Lazima tuwashawishi Zambia na DRC tujenge reli kutoka Tunduma-Kasama-Lubumbashi-Likasi na Kutoka Makambako-Mtwara Port.

4.Lazima Sgr itoke Mpanda-Karema na Kigoma

5.Lazima tutafute pesa za kujenga meli kubwa za mizigo na abiaria ndani ya Ziwa Viktoria na pia tujenge Bandari,Barabara na reli upande wa DRC hata Kwa kuwakomesha pesa

6.Lazima tuwape DRC,Rwanda na Burundi Ardhi za Bure za kumhudumia mizigo Yao Pwani.

My Take
Tusipofanya hayo tunaenda kupoteza hata hiyo DRC Kwa Kenya,Angola na Mozambique na ikizingatiwa DRC inajenga Bandari na reli kuunganisha na Zambia na Angola.

Washindani Wetu wa Kenya wao Wana uhakika na Uganda,South Sudan, Northern DRC na somehow Ethiopia na Rwanda.

Tuachane na Mpango wa kujenga reli ya Mtwara Corridor hiyo Haina maana tena imeshakufa,Nguvu zote zielekezwe Kujenga kioande Cha kutoka Makambako -Mtwara.
View attachment 3080431
Mama anaupiga mwingi apongezwe kwa kusaidia malawi kupitisha mizigo msumbiji
 
Back
Top Bottom