Mswada/sheria ya tra kutoshikilia fedha za wafanyabiashara benki

Mswada/sheria ya tra kutoshikilia fedha za wafanyabiashara benki

Waaai

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2021
Posts
1,293
Reaction score
2,642
Nashauri kupelekwe mswada bungeni kuhusu hii sintofahamu ili wafanyabiashara wawe na imani na serikali yao.

NGOJA NITOE SCENARIO:

TRA imefanya uchunguzi wa mahesabu yangu na kugundua nililipa kodi pungufu miaka minne iliyopita, wananitoza faini na riba na kunipa notice ya mwezi mmoja kuilipa.

Mm namrudia mhasibu na mkaguzi wangu aliyetengeneza mahesabu kuwahoji kwann hawakugundua hili mapema mpaka adhabu na riba zisizolipika zinanikumba.

Baada ya utafiti inagundulika kuna makosa katika ukokotozi wa kodi, tunaandika barua kuhoji njia zilizotumika kukokotoa hilo ongezeko la kodi.

TRA wanaagiza nilete nyaraka za mauzo na manunuzi ya miaka hiyo minne iliyopita bila kusitisha notice yao ya mwezi mmoja.

Wakati tunapambana namna ya kukusanya na tracing ya nyaraka napata mteja ananiwekea pesa kwa ajili ya biashara, nakwenda bank kwa ajili ya drawing nakuta notice na account kushikiliwa mpaka nitakapolipa kodi...........

Sasa hapa tayari kuna conflict kati yangu na TRA tunahitaji mtu wa tatu kutusuluhisha ambaye ni mahakama.

KUWEPO SHERIA KUWA ISIZUIWE ACCOUNT YA MFANYABIASHARA BILA IDHINI YA MAHAKAMA ILI KUREJESHA IMANI YA KUFANYA BIASHARA KWA UHURU.
 
Serikali, Bunge na Mahakama vyote ni mali ya CCM. Hakika nawaambieni hakuna kitakachobadilika.
Hivyo hivyo tu sheria ikiwepo mameneja watakuwa na woga wa kuchukua hatua haraka haraka bila kutafakari.
 
Unapoitaja CCM huwezi itenganisha na dhuluma, wizi na ufisadi.
Pamoja na yote tumekaa na ccm kwa miaka mingi biashara zikifanyika. Bado biashara zinahitajika na imani inahitajika kuboreshwa.
 
Watu wameingia madarakani kwa wizi wa kura ndio wa kuogopa mahakama?
Sheria iwepo hivyo hivyo itasaidia hata kukomaza wanaoonewa wafikie kikomo cha uvumilivu.
 
Watu tuna machungu sana na hicho kikosi kinachoitwa TRA, makosa wafanye wao faini na unyang'anyi afanyiwe mfanya biashara
 
Watu tuna machungu sana na hicho kikosi kinachoitwa TRA, makosa wafanye wao faini na unyang'anyi afanyiwe mfanya biashara
Na hivi hawajasoma Financial Account, wao wamesomea tax account na sheria ya kodi basi huwa wanafanya makosa. Kinachowaponza wafanyabiashara ni utunzaji wa nyaraka. Unakuwa huna prove.
 
B11AE78B-3AEA-4450-B3A7-CECF0357CF2A.jpeg

Soma sheria inasemaje section 89 (2b) unatakiwa utunze nyaraka za kibiashara kwa miaka 5. Ipo ivyo duniani kote, kama ujafanya ivyo unajitafutia matatizo makubwa.

Malalamiko ya kodi Tanzania ni uelewa mdogo wa walipaji, waziri nae anaingia kichwa kichwa kutoa maagizo bila ya kusoma sheria.
 
Upo sawa kabisa. Ila miaka mitano ni mingi sana. Kwann tusimalizane kwenye mwaka wa biashara husika?

Hesabu zilizoletwa end of june 2019 basi malizana na mfanyabiashara 2020 June hilo zoezi liwe limeisha unakaa nazo za nn ili kuwekwe maadhabu na riba?

Sasa unadhani document za miaka mitano ya biashara nyuma ni rahisi kuzihifadhi? Na documentation ni gharama sana. Filling cost? Usafi? Unless tuingie 100% kwenye e-filling.
 
Accountants kwenye mashirika makubwa wana mbinu nyingi za kukwepa kodi; lengo la kuweka miaka mitano wakija kustukizia mchezo leo wanataka kukagua na miaka ya nyuma kama ulikuwa ukiwaongopea kwa mbinu hizo.

Hivyo ndio ilivyo duniani sio Tanzania tu.
 
D5DAFB9F-E3FC-476C-B7FE-9912A603069F.jpeg

Hilo lingine watu wengi utasikia nimekadiriwa kodi kubwa kushinda mauzo, ukilipa kodi kubwa ya makadirio na mauzo yakawa tofauti unatakiwa urudishiwe overpayment.

Kodi sio tatizo Tanzania, ni uelewa mdogo wa walipaji na maafisa wachache wa TRA wenye kutumia sheria vibaya.
 
Sasa hapa tayari kuna conflict kati yangu na TRA tunahitaji mtu wa tatu kutusuluhisha ambaye ni mahakama.

KUWEPO SHERIA KUWA ISIZUIWE ACCOUNT YA MFANYABIASHARA BILA IDHINI YA MAHAKAMA ILI KUREJESHA IMANI YA KUFANYA BIASHARA KWA UHURU.
Jambo jema sana tumeonewa sana waziri tusaidie hizi sheria zimepitwa na wakati
 
Back
Top Bottom