KERO Responded Mtaa wa Chungurira - Wilaya ya Tanga Mjini tuliahidiwa umeme wa REA, hakuna kilinachoendelea

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mtaa wa Chungurira, Kata ya Tangasisi, Wilaya ya Tanga Mjini, Mkoa wa Tanga. TANESCO walitueleza kuwa wanapitisha umeme wa REA, hivyo wananchi tukafanya wiring na fittings kwa kukopa fedha, wengine wakajenga hata chumba kimoja ili wapate huduma hiyo.

Hata hivyo, tangu mwezi Agosti hadi leo Oktoba 2026, hakuna umeme ulioingia eneo letu, hali hii imetuacha na madeni tuliyokopa kwa matumaini ya kupata umeme, lakini huduma hiyo bado haijapatikana.

MAJIBU YA TANESCO KUHUSU CHANGAMOTO HIYO 👇​
 
Habari, ndugu mteja na pole sana kwa changamoto hii.

Tunashukuru kwa hii taarifa. Tunaomba muda kidogo, ndugu mteja ilitufanye ufuatiliaji juu ya huu mradi na kurejea na majibu stahiki.

Tunaomba uvumilivu kwa muda. Asante. ^FL
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Habari, ndugu wateja wetu, na asante tea kwa kuwasiliana nasi. Tunaomba tutoe mrejesho juu ya suala hii.

Tafadhali tambua kuwa hatua za utekelezaji zinaendelea na tayari mahitaji ya eneo hilo yalishaainishwa na kuwasilishwa. Taratibu za utekelezaji zitakapo kuwa tayari mradi utaanza na Kama unavyojua eneo hilo lipo tanga mjini, kutokana na eneo hilo kuwepo ndani ya jiji kuna hatua kadhaa zinapitiwa kupata mradi Kama ilivyo REA, ikiumbukwe REA ilikuwa mahususi kwa maeneo ya vijijini.

Hivyo tunaomba muendelee kuwa wavumilivu taratibu zikikamilika utekelezaji utaanza.

Aidha, tunashauri kutumia njia sahihi kupata taarifa sahihi na kujiepusha na vishoka wakati Mnaendelea kusubilia huduma.

Asante. ^NI
 
Back
Top Bottom