Mtaa wa Chungurira, Kata ya Tangasisi, Wilaya ya Tanga Mjini, Mkoa wa Tanga. TANESCO walitueleza kuwa wanapitisha umeme wa REA, hivyo wananchi tukafanya wiring na fittings kwa kukopa fedha, wengine wakajenga hata chumba kimoja ili wapate huduma hiyo.
Hata hivyo, tangu mwezi Agosti hadi leo Oktoba 2026, hakuna umeme ulioingia eneo letu, hali hii imetuacha na madeni tuliyokopa kwa matumaini ya kupata umeme, lakini huduma hiyo bado haijapatikana.