Mtaa wa John Rupia Tanga

Mtaa wa John Rupia Tanga

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
MTAA WA JOHN RUPIA TANGA
Moja ya vibao vingi vya Mtaa wa John Rupia kipo pembeni ya Msikiti Ngazija, Tanga.

Nimefikia hoteli jirani na kwa hakika ni mkabala na msikiti huu na ndiyo nikabahatika kuona kibao hicho.

Nilipata kuwauliza wahusika miaka mingi nyuma wakati naishi Tanga walipotoa jina la ''Maua,'' kwa mtaa mmoja mkubwa Ngamiani.

Niliuliza ''Maua'' ina maana gani katika historia ya Tanga?

Nikasema kwa nini mtaa ule haukupewa jina la Hamisi Heri au Abdallah Rashid Sembe waasisi wa TANU na wapigania uhuru wa Tanganyika?

Sikupata jibu?

Nilipoona kibao cha John Rupia, Tanga nilijisemeza moyoni kwangu nikajiambia, ''John Rupia tayari ana mtaa Dar es Salaam,

Kwa nini mtaa huu haukupewa jina la mpigania uhuru mwingine kutoka Tanga aliyeacha alama kubwa katika harakati za uhuru, mathalan mtu kama Peter Mhando kijana aliyeitumikia TANU lakini akafa mapema mwaka wa 1958 kabla ya uhuru kupatikana?

Hapana sababu ya kurudia majina ya viongozi ambao tayari tumeshawaadhimisha.
 
Yaani kilichokuuma hapo ni jina la kikristu badala ya jina la kiislamu

İl-hali wenye tanga yao wako very peaceful

Hatari sana we mzee…. Unazeeka na chuki zako
 
Yaani kilichokuuma hapo ni jina la kikristu badala ya jina la kiislamu

İl-hali wenye tanga yao wako very peaceful

Hatari sana we mzee…. Unazeeka na chuki zako
Umenifilisi kila kitu huyu Ustadhi ni shida.John Rupia jina kubwa sana huyu huwezi kumtia daraja moja na wale wajinga wajinga kama Sykes family,Tajadir ............

Huyu ni mwamba tajiri nwerevu jina lake lilitakiwa kuwemo Tanganyika nzima.Mikoa yote ya Tanganyika pamoja na wilaya zake.
 
Ukiyajua ya kimweri utachukia zaidi. Maana ndio Tajiri mwenye mitaa mingi Tanzania.
 
Yaani kilichokuuma hapo ni jina la kikristu badala ya jina la kiislamu

İl-hali wenye tanga yao wako very peaceful

Hatari sana we mzee…. Unazeeka na chuki zako
Timing,
Hapana sina chuki na Mzee John Rupia.

Jitahidi unifahamu na ufahamu ninachoandika:

MIAKA 60 YA UHURU WA TANGANYIKA 1961: TUNAMUENZI JOHN GODFREY RUPIA (1904 - 1978)
Wajukuu ni watamu kuliko wana uliozaa mwenyewe.
Huwezi kujua ukweli wa maneno haya sharti upate mjukuu.
Wajukuu na wao wana mapenzi na babu na bibi zao kushinda wanavyowapenda baba na mama zao.
Nimemjua Joyce Aysha Rupia siku hizi za karibuni.
Joyce ni mjukuu wa John Rupia kwa mwanae Paul Rupia.
Mama yake Joyce ni Biubwa Amour Zahor.
Kilichotukutanisha mimi na Joyce Rupia naamini kwanza ni mahaba yake kwa, "mumuwe," mpenzi yaani babu yake Mzee John Rupia.
Joyce alinitafuta ili ajue historia ya babu yake.
Joyce hakuwa anaijua historia ya babu yake katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika na katika kutaka kujua historia hiyo ndipo aliponitafuta.
Hii ilikuwa baada ya yeye kuwa nje ya nyumbani masomoni toka akiwa na umri wa miaka mitano.
Pili alitaka tukutane kwa kuwabkulikuwa na kitabu cha mama yake, "Mwanamke Mwanamapinduzi," kilichokuwa kinatarajiwa kuzinduliwa Zanzibar na Dar-es-Salaam.
Hiki kilikuwa kitabu cha Biubwa Amour Zahor.
Kwa kiasi fulani nilikuwa nimehusika na kitabu hiki hivyo Joyce alipenda tukutane.
Katika mazungumzo yetu mengi akanifahamisha kuhusu azma yake ya kuweka kumbukumbu katika kaburi la babu yake.
Joyce alinipeleka kuliona kaburi la John Rupia ambalo lipo ndani ya Chuo Cha CCM Kivukoni.
Joyce akaniambia kuwa yuko katika mpango wa kuliboresha kaburi la babu yake lipate haiba kubwa yenye hadhi ya John Rupia kwa heshima yake halisi kiasi wanafunzi wanapofika hapo chuoni kwa mara ya kwanza walione limetokeza na wavutiwe kulisogelea kujua ni nani aliyezikwa hapo.
Wakifika hapo kaburini wanafunzi au yeyote atakaefika chuoni hapo wasome jiwe kubwa atakalosimika hapo ili historia ya babu yake katika kuundanTANU na kupigania uhuru wa Tanganyika ifahamike.
Joyce alinifahamisha kuwa ardhi iliyojengwa Chuo Cha CCM Kivukoni ni ekari 56 na zilitolewa bure na babu yake kwa TANU watumie ardhi ile wapendavyo.
Baba na mama yake John Rupia waliishi hapo na ndipo alipozaliwa na kukulia.
Ndani ya ardhi hii kulikuwa na makaburi ya baba na mama yake John Rupia na pia watu wengine waliokuwa wanaishi Kigamboni zama hizo.
Baada ya kupewa ardhi hiii TANU wakaamua kujenga Kivukoni College kama chuo cha kusomesha itikadi kwa viongozi watakaokuja kutumikia chama cha TANU na serikali zake.
John Rupia aliusia akifa azikwe katika ardhi hiyo pembeni ya wazazi wake.
John Rupia alipofariki mwaka wa 1978 alizikwa hapo na amri ikatolewa kuwa katika makaburi hayo pasizikwe tena mtu mwingine.
Makaburi yale yakawa yamefungwa baada ya amri hii.
Leo nilipata bahati ya kuwa mmoja wapo wa watu wachache walioalikwa kushuhudia kaburi la Mzee John Rupia katika muonekano wake mpya wa kuvutia.
Haya ni katika mapenzi makubwa sana ambayo mjukuu anaweza kumfanyia babu yake.
Joyce si kama kamuenzi babu yake tu ikawa kamaliza.
Joyce kaifanyia Tanzania, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chuo Cha CCM Kivukoni hisani kubwa isiyo na mfano kwa kumuenzi mmoja wa waasisi na wafadhili wakubwa wa TANU na mtu aliyekuwa siku zote pembeni ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakati wa kupigania uhuru wa nchi yetu.
Hatuna cha kumlipa Joyce Aysha Rupia ila sisi kumpongeza na kumshukuru.
 
Back
Top Bottom