Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Sisi Wakazi wa Mtaa wa Kisonge na Mtaa wa Bin Abeid hapa Mkoa wa Mjini Magharibi tuna changamoto ya mifumo ya Maji taka kutowekwa katika mazingira mazuri na kwa ufupi ni kuwa Miundombinu imeharibika lakini Viongozi wetu hawachukui hatua.
Kuna mabomba na chemba za majitaka zinavujisha maji machafu ambayo yanasamba hapa mtaani kwetu.
Wakati huohuo hali ya Barabara zenu nazo sio nzuri, kutokana na ubovu maji yametuama na kusababisha kero zaidi kwetu wakati wa kupita.
Watoto wetu wanapita katika maeneo yenye maji machafu na wengine wanayachezea, tunaomba viongozi wanaohusika wafanye jambo kurekebisha hali hii kwa kuwa ni hatari kwa afya zetu wote.
Watoto wetu wanapita katika maeneo yenye maji machafu na wengine wanayachezea, tunaomba viongozi wanaohusika wafanye jambo kurekebisha hali hii kwa kuwa ni hatari kwa afya zetu wote.