christopher mlewa
Member
- Oct 22, 2018
- 15
- 39
Habarini ndugu zangu,
Naomba nisiwachoshe, bali niingie moja kwa moja kwenye swala la msingi. Kuna mtaa hapa Iringa mjini unaitwa Mashine Tatu, ambao ni mtaa wa pili kwa idadi kubwa ya wafanyabiashara wadogo na wakubwa. Mtaa namba moja kwa shughuli nyingi ni Miyomboni.
Ndugu zangu, mtaa huu unatutia aibu wasomi tulioko mtaani na wale walioko madarakani, hususan kwenye Manispaa ya Iringa. Hali ya mtaa huu imekuwa mbovu kupindukia. Hebu fikiria, kuna mama ambaye anauza samaki hapa Mashine Tatu, lakini gari linamsubiri mama huyu amalizane na mteja ili aweze kutoa samaki njiani ili gari lipite. Mbele yake, kuna bajaji zaidi ya kumi zinapiga debe kuwahamasisha abiria wa Isakalilo na Kihesa. Pembeni, vijana wanadakisha nguo barabarani. Hujakaa sawa, unakutana na mateja wamejazana wakivizia kukuibia simu yako ya Infinix yenye "protector" iliyovunjika.
Tafadhali, naomba wasomi wenzetu walioko madarakani, hasa RC, DC, na Meya, watuheshimishe sisi wengine ambao tuna digrii zetu kutoka RUCU na MKWAWA, kwa kutatua kero hii. Kiukweli, barabara ya kutoka stendi kuu ya zamani kupitia Mashine Tatu haipitiki kabisa na ni kero kubwa.
Wasomi wenzetu waliobahatika kupata madaraka, naomba mjitahidi kuboresha mtaa huu. Mfano mzuri ni ule wa Dodoma kwenye barabara ya "One Way," ambapo vyombo vya moto haviruhusiwi kuingia mtaani, na sehemu hiyo imetengwa kwa watembea kwa miguu na wafanyabiashara wadogo. Hii imeupa mtaa ule thamani na unavutia sana kwa biashara na shughuli za kila siku.
Tafadhali, fanyeni hivyo hapa Mashine Tatu.
ASANTENI.