A
Anonymous
Guest
Mtaa wa Miswe, Kata ya Mbwawa, Mkoa wa Pwani kuna kiwanda cha unga kilichofunguliwa katikati ya makazi yetu tangu Mwaka 2025. Kiwanda hicho kinamilikiwa na wawekezaji kutoka Nigeria na kimekuwa kikitoa kelele kubwa kutoka kwenye mitambo yake.
Kelele hizo zinatusumbua sana, hasa wazee, wagonjwa na watoto wachanga. Imefikia hatua ya kushindwa kuwasiliana na mtu aliyekaribu nawe bila kusogeleana au kutazamana midomo wakati wa kuzungumza.
Serikali ya mtaa na kata inatambua changamoto hii, lakini mpaka sasa hakuna hatua zilizochukuliwa. Tunajiuliza ilikuwaje halmashauri ikaruhusu kiwanda kujengwa katikati ya makazi ya watu. Zaidi ya hayo, kiwanda hicho hakina bango wala utambulisho wowote unaoonekana.
Kiwanda hicho kipo kando ya Barabara ya Bagamoyo, kutoka Mlandizi, katika Mtaa wa Miswe, Kata ya Mbwawa. Tunaomba mamlaka husika zifuatilie na kuchukua hatua kuhusu kero hii.