Mtaa wa Sheikh Yusuf Badi Lindi

Mtaa wa Sheikh Yusuf Badi Lindi

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
SHEIKH YUSUF BADI WA LINDI

Inaaminika kuwa hakuna picha ya Sheikh Yusuf Badi popote kwani alikuwa hapendi kupigwa picha.

Juhudi zangu za kupata picha yake hazijafanikiwa hadi hivi sasa.

Rafiki yangu ameweka kibao cha mtaa wenye jina ‘’Sheikh Badi.’’

Mtaa huu uko Lindi.

Nimelisikia jina la Sheikh Yusuf Badi Lindi mjini miaka mingi iliyopita wakati nafanya utafiti wa kitabu cha historia ya TANU kupitia maisha ya Abdulwahid Sykes.

Siku ya kwanza nilianza mahojiano yangu na Salum Mpunga tukiwa tumekaa kwenye kibaraza za msikiti mkubwa wa Lindi mjini ulioko karibu na kituo cha mabasi.

Baada ya mazungumzo yangu na Salum Mpunga siku ya pili asubuhi nikawa na mazungumzo na Yusuf Chembera nyumbani kwake kwenye varanda yake ndogo lakini nadhifu.

Hawa watu wawili Salum Mpunga na Yusuf Chembera ndiyo waasisi wa TANU Southern Province mwaka wa 1955.

Kisa cha wazalendo hawa na jinsi walivyoweza kumleta Mwalimu Nyerere Southern Province ni kisa cha kusisimua sana.

Sasa niko na Yusuf Chembera nyumbani kwake mwezi wa Ramadhani.

Yusuf Chembera anasema Kiswahili kizuri na alikuwa mtu fasaha sana akijua kupanga maneno yake.

Alianza kunieleza historia ya TANU kwa kunitajia maisha yake ya udogoni na hapo ndipo kwa mara ya kwanza nikalisikia jina la Sheikh Yusuf Badi.

‘’Nilipofika umri wa kusoma baba yangu akanipeleka chuoni kwa Sheikh Yusuf Badi kusoma.

Chuo cha Sheikh Badi ndicho kilikuwa chuo kikubwa na yeye mwenyewe alikuwa sheikh akiheshimika kusini nzima.’’

Yusuf Chembera akanieleza yote waliyokutananayo katika kuasisi TANU wakisaidiana na mzee wao Suleiman Masudi Mnonji ambae nyumba yake ndiyo ilikuwa ofisi ya TANU ya kwanza Lindi.

Southern Province kulikuwa na vitisho vingi dhidi ya TANU watu wakitishwa kwa kuambiwa kuwa TANU ni chama cha Waislam ambao wanataka kuleta vita vingine vya Maji Maji.

Uongozi wa TANU Lindi ukaamua kumtuma Salum Mpunga na Ali Ibrahim Mnjale Dar es Salaam kumwalika Nyerere aje Lindi ili asafishe hii propaganda na wananchi waiunge mkono TANU kupigania uhuru wa Tanganyika.

Nyerere akiongozana na Ali Mwinyi Tambwe na Rajab Diwani walifika Lindi, Mikindani, Masasi na Nachingwea na baada ya ziara hii TANU haikuwa tena na kizuizi ila watu walijiunga na chama kwa wingi.

Hii ilikuwa mwaka wa 1955 na Nyerere alikuwa amekwenda na kurudi UNO safari ya kwanza.

Mwaka wa 1956 Nyerere alirejea tena Lindi na safari hii mapokezi yake yalikuwa makubwa na ya kupendeza.

Katika ile safari ya kwanza serikali ilikataza maandamano ya kumpokea Nyerere mjini.

Ilibidi Nyerere na ujumbe wake upokelewe kijiji cha Mbanji nje ya mji na wanachama wa TANU waingie mjini kimya kimya na wageni wao kama vile wanasindikiza msiba.

Mara baada ya safari ya kwanza ya Nyerere Lindi ili kukipa chama nguvu mwanafunzi wa Sheikh Yusuf Badi, Yusuf Chembera alimfuata mwalimu na sheikh wake Sheikh Badi kumuomba ajiunge na TANU ili chama kipate nguvu.

Sheikh Yusuf Badi alipojiunga na TANU alikuja na jeshi kubwa la na murid wake wa Tariqa Qadiriyya.

Sheikh Yusuf Badi aliipa TANU mjini Lindi na pembezoni heshima kubwa.

Mwaka wa 1956 Nyerere alipokuja Lindi hali ya TANU ilikuwa imebadilika chama kikiwa na nguvu kubwa isiyo na kifani.

Katika mapokezi ya Nyerere Sheikh Yusuf Badi alitoka na chuo chake na wanafunzi wake kwa maandamano wanafunzi wakipiga dufu huku wakisoma kasida sauti za matari zikisikika kote.

Hii ilikuwa siku ya shamrashamra kubwa mjini Lindi.

Usiku wake Mtaa wa Makonde nyumbani kwa Suleiman Masudi Mnonji Sheikh Yusuf Badi alifanya dua kubwa iliyohudhuria na Waislam aliowachagua yeye sheikh mwenyewe maalum kwa hafla hiyo.

Dua hii ilihudhuriwa pia na masheikh wengine maarufu pale Lindi na kutoka vijiji jirani.

Katika dua hii alikuwapo Bi. Sharifa bint Mzee mmoja wa akina mama waliofanya kazi kubwa kuwavuta wanawake kujiunga na TANU.

Mussa Athumani Lukundu, kiongozi wa Dockworkers Union Lindi aliandaa karamu kubwa kwa heshima ya Nyerere.

Siku ya ukumbusho mkubwa sana mjini Lindi ilikuwa siku ya uhuru, tarehe 9 Desemba, 1961.

Sheikh Badi, ambae alikuwa bingwa wa kutunga mashairi, aliombwa na TANU kuandika hotuba ya uhuru.

Hotuba hii ilisomwa na mwanafunzi wake Yusuf Chembera mbele ya DC akiwa kama mwakilishi wa utawala wa Kiiereza uliokuwa uking’oka.

Hotuba hiyo ya Sheikh Badi iliandikwa kwa Kiarabu na Chembera alinionyesha nikaishika kwa mikono yangu.

Sheikh Badi hakuona kama ipo hotuba yoyote iliyoandikwa na mwanadamu iliyostahiki hafla kama ile ya siku ya kujikomboa kutoka minyororo ya ukoloni.

Sheikh Badi alimsomea mwanafunzi wake Chembera, dua ya kunut ambayo husomwa na Waislam katika kila sala ya alfajir.

Usiku wa manane wa tarehe 9 Desemba, 1961 ulikuwa usiku adhim sana kwa wote wawili, mwalimu na mwanafunzi wake, pale watu walipokusanyika katika Uwanja wa Gofu kumsikiliza Chembera akisoma kunut kupokea uhuru wa Tanganyika.

Maspika yalisikika yakitoa sauti ya Yusuf Chembera akisoma Dua ya Kunut na wananchi wakiitika Amin, Amin, Amin.

Hakuna popote jambo kama hili lilitokea katika kupokea uhuru wa Tanganyika.

Hakika kwa watu wa Lindi hawakukosea kumpa mtaa Sheikh Yusuf Badi.

Sheikh Badi anastahili kukumbukwa na anastahili heshima hii.

Picha ya kwanza Mtaa wa Sheikh Badi, Bi. Sharifa bint Mzee katika utu uzima na wajukuu zake, Yusuf Chembera na Salum Mpunga.

Screenshot_20200623-224647.jpg
 
Asante sana mkuu kwa historia nzr na tamu kweli kweli. Ubarikiwe sana na usichoke kutuletea vitu adimu Kama hv.
 
Azarel,

Nakusihi usiniite "Mudy," sipendi mimi ni mtu mzima wa miaka 68 usipitiwe ukadhani ni kijana mwenzio unaweza kunitania.

Nakuomba unifanyie staha kama mimi ninavyokuheshimu.

Ikiwa moyo wako unaumizwa na niandikayo dawa si kunifuatafata kwa kejeli na kunivunjia heshima.

Huu si uungwana unaweza ukawa unazipita post zangu ukasoma nyingine.

Nakusihi.

Sijaandika uzushi wala uongo na ushahidi wangu ni huo hapo chini:

1. PUBLICATIONS/RESEARCH PAPERS/ARTICLES
2. The Life and Times of Abdulwahid Sykes 1924 –1968 The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press London, 1998 translated into Kiswahili as Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924-1968 Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza, Phoenix Publishers, Nairobi, 2002.
3. The Torch on Kilimanjaro, Oxford University Press, Nairobi, 2006
4. Contributing author for an African anthology: The Mermaid of Msambweni and Other Stories, Oxford University Press 2007, Nairobi.
5. Contributing author Dictionary of African Biography (DAB), Oxford University Press 2011, New York.
6. Uamuzi wa Busara, Abantu Publications 2008, Dar es Salaam.
7. Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No. 1, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam.
8. Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No.2, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam
9. Dar es Salaam na Wazalendo Wake Mashujaa Katika Kupigani Uhuru wa Tanganyika Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaaam
10. Watu Mashuhuri Katika Kuulingania Uislam Tanzania, Sheikh Ilunga, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam
11. Dola, Kanisa na Tatizo la Udini Tanzania, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam
12. The School Trip to Zanzibar, Africa Proper Education Network 2020, Dar es Salaam
13. In Praise of Ancestors (1987) Africa Events (London).
14. Abdulwahid Sykes: Founder of Political Movement (1988) Africa Events (London).
15. Islam and Politics in Tanzania (1989) Al Haq International (Karachi)
16. The Plight of Tanzanian Muslim (1993) Change (Dar es Salaam).
17. Tanzania - The "Secular" Unsecular State (1995) Change (Dar es Salaam).
18. The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A Muslim Riddle (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Intercultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003).
19. Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000’ (Paper presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15th – 17th 2003).
20. Sheikh Hassan bin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 – 1968) (Paper presented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27th February – 4th March 2004).
21. Islamic Movement and the Christian Lobby in Tanzania - the Experience of the late Prof. Kighoma Ali Malima (1938 – 1995) (Paper Presented to Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) Sokoine University of Agriculture (SUA) Morogoro 11th April 2004).
22. Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience (Paper Presented at the Conference on Islam, Terrorism and African Development University of Ibadan, Nigeria 8th - 10th February 2006).
23. Al Marhum Sheikh Kassim bin Juma bin Khamis (1940 – 1994) and the Pork Riots of 1993. (Paper Presented at the Regional Conference on Islam in Eastern Africa: Islam Encounter with the Challenges of the 21st Century 1st - 3rd August 2006, Kenyatta University, Nairobi.
24. 14. Muslim Bible Scholars of Tanzania – The Legacy of Sheikh Ahmed Deedat (1918 – 2005) Paper Presented at the International Symposium on Islamic Civilisation in Southern Africa Organised by The Organisation of Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA) The National AWQAF Foundation of South Africa (AWQAF SA 1 – 3 September 2006 University of Johannesburg.
25. Tanzania: A Nation Without Heroes Seminar Organised by IFRA French Institute for Research in Africa and BIEA British Institute in East Africa 23rd and 24th September 2013 at IFRA Nairobi.
26. Awards: Several Awards
27. Visiting Scholar: (2011)
28. University of Iowa, Iowa City, USA
29. Northwestern University, Chicago, Illinois, USA
30. Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin.
31. OTHER COUNTRIES VISITED
32. Zambia, Ethiopia, Great Britain, Swaziland, Msumbiji, Zimbabwe, Zambia, Sudan, Egypt, Saudi Arabia, United Arab Emirates, Oman, Yemen, Uganda, Switzerland, Iran, France, Netherlands, Turkey and Abu Dhabi.

Hapo chini ni kimoja ya vitabu vitano nilivyotoa kati ya 2018 - 2000.
 

Attachments

  • ASHA THE SCHOOL TRIP TO ZANZIBAR.jpeg
    ASHA THE SCHOOL TRIP TO ZANZIBAR.jpeg
    90.3 KB · Views: 5
Hivi mwaka 1955 kulikuwa na serikali hasaa yenye nguvu ya kukataza maandamano ya kumpokea Nyerere mjini?

Serikali ipi? Chini ya kiongozi yupi? Hebu fafanua hapo sheikh
 
Hivi mwaka 1955 kulikuwa na serikali hasaa yenye nguvu ya kukataza maandamano ya kumpokea Nyerere mjini?

Serikali ipi? Chini ya kiongozi yupi? Hebu fafanua hapo sheikh
Azarel,
Serikali iliyokuwapo madarakani ilikuwa serikali ya kikoloni na ilikuwa ikiwakandamiza sana Waafrika.

Ushahidi ni kuwa kati ya mwaka wa 1951 - 1953 serikali ilitoa Government Circular No. 1 - 3 zikiwaonya watumishi wa serikali kukaa mbali na siasa.

Kwenye Wasifu wa Julius Nyerere kitabu cha pili kuna barua nyingi kati ya Nyerere na Gavana Twining kuhusu unyanyasaji dhidi ya TANU.

Unajua mimi nimetafiti historia ya TANU hivyo najua mengi.

Nakukumbusha tena.

Mimi si "sheikh,"kama wewe ulivyokuwa si shamasi au mchungaji.

Ukinipa cheo ambacho sistahili unawapoteza wasomaji wengine.

Ikiwa unapenda kunipa "title," basi jaribu kuniita mzee.

Hili jina litanienea vizuri.
 
Waislamu wa zaman walikuwa shupavu wamepigania sana uhuru, lakin wa sasa hivi ni wanyonge sana, shida ni nini?
 
mashehe wa uamsho wako jela mwaka wa 7, waislam kimya, ajira zinawabagua, waislam kimya, huo sio unyonge?
Hata wewe ni Muislam je umefanya nini?

Hebu thibitisha kwa mfano ni wapi Waislam walibaguliwa katika ajira?
 
mashehe wa uamsho wako jela mwaka wa 7, waislam kimya, ajira zinawabagua, waislam kimya, huo sio unyonge?
Laki...
Hayo yote uliyosema ni kweli.

Afanyayo hayo na akaona wanaofanyiwa wako kimya bila shaka atatafsiri kuwa hawa wanaodhulumiwa ni wanyonge.
 
Laki...
Hayo yote uliyosema ni kweli.

Afanyayo hayo na akaona wanaofanyiwa wako kimya bila shaka atatafsiri kuwa hawa wanaodhulumiwa ni wanyonge.
Sijawahi kuskia muislam akipaza sauti kukemea dhulma wanayofanyiwa, BAKWATA ndio hao wanaokaa na wanakunywa chai na kucheka na wanaowadhulumu, unadhani kukaa kwenu kimya ndio dhuluma itaisha? hata kukemea mmeshindwa?
 
Tunashukuru sana Mohamed Said kwa historia isiyoelezwa mara nyingi juu ya mchango wa Waislamu kwenye vuguvugu la kuleta Uhuru.
 
sijawahi kuskia muislam akipaza sauti kukemea dhulma wanayofanyiwa, BAKWATA ndio hao wanaokaa na wanakunywa chai na kucheka na wanaowadhulumu, unadhani kukaa kwenu kimya ndio dhuluma itaisha? hata kukemea mmeshindwa?
Laki...
Kila jambo linahitaji hekima na njia bora ya kuliendea.

Vinginevyo unaweza ukawadhuru watu.
 
Mchango wa Waislamu na watu wa Pwani katika harakati za kudai uhuru zilichangia kwa kiasi kikubwa sana kwa uhuru wa Tanganyika. Ila sijui ni kwa makusudi au kwa bahati mbaya kuna kikundi cha watu kinajaribu kuzipuuza juhudi hizi na kumvisha u "hero" asiyehusika.
 
Back
Top Bottom