Mtaala wa Udaktari Udurusiwe

Mtaala wa Udaktari Udurusiwe

Alafu eti mhitimu wa Cheti cha Utabibu anaitwa jina moja la CO (Clinical Officer) yaani Tabibu sawa na mhitimu wa Stashahada ya Utabibu! Ina maana mtaala wa Cheti cha Utabibu na mtaala wa Stashahada ya Utabibu vinalingana kwenye maudhui? Cheti na Stashahada vina hadhi sawa? Baghosha Tz!

Wabunge mliwashe kieleweke.
Mwenye cheti cha utabibu anaitwa assistant clinical officer
Mwenye diploma ya utabibu anaitwa clinical officer.
Utendaji kazi ni ule ule hauna tofauti yoyote tofauti ipo katika vyeo tu
 
Mkuu hujanishawishi.

Unamaanisha kidato cha 6 bila Diploma ya Utabibu yuko sawa na kidato cha 6 mwenye Diploma ya Utabibu?

Je, kidato cha 6 bila Diploma ya Utabibu anajuwa yafuatayo?

1. Pharmacology.
2. Surgery.
3. Anatomy and Physiology.
4. Medical Psychology.
5. Lab Technics.
6. Pathology (Bacteriology & Virology).

Hapo 1- 4 namaanisha je, mhitimu wa kidato cha 6 anajuwa kuandika dawa? Je, anajuwa upasuaji mdogo? Je, anajuwa kusoma ripoti za Maabara? Je, anajuwa kushona nyuzi? Je, anajuwa kudunga sindano? Je, anajuwa kuzalisha mjamzito? Je, anajuwa kuweka dripu?

Wenye Diploma ya Utabibu wakienda Digrii ya Udaktari wapunguziwe miaka ya kozi.
Hizo Products tunazipima muda upi before hawajawa enrolled na vyuo au after wamepata hiyo MD!!


Kama kigezo ndio hicho tu kujua hizo Courses mkuu!?
 
tubadilishe ngazi za kusomea udaktari zianze kuanzaia ukimaliza kidato cha nne unaelekea huko baada ya miaka 2 advance na sita 6 ya kusomea
 
Uzoefu wenu upo kwenye ngazi ya chini ya uelewa, hata kuruhusiwa kusoma degree ni favour tu mmepewa.....ila kimsingi anayeruhusiwa kusoma degree kwa Tanzania ni aliyefuzu masomo ya A-level.
 
Tujadiliane.

Mhitimu wa Stashahada ya Utabibu (miaka 2) na pengine aliye na uzoefu wa kazi, kwanini akienda kusoma Udaktari kamili (ngazi ya Shahada) asipunguziwe miaka ya masomo toka 5 kurudi chini?

Anapolazimika kusoma miaka 5 sawa na mhitimu wa kidato cha 6 ina maana mtaala wa kidato cha 6 ndiyo huo huo mtaala wa Stashahada ya Utabibu?

Je, kidato cha 6 yuko sawa na mwenye Stashahada ya Utabibu kwamba wote hao wawili wasome miaka na mtaala unaofanana wa Shahada ya Udaktari chuo kikuu?

Aidha, kwanini mhitimu wa Cheti cha Utabibu anaitwa jina moja la CO (Clinical Officer) yaani Tabibu sawa na mhitimu wa Stashahada? Ina maana mtaala wa Cheti cha Utabibu na mtaala wa Stashahada ya Utabibu vinalingana kwenye maudhui? Cheti na Stashahada vina hadhi sawa?

Wabunge mlione hili kwa jicho la 3.
Diploma ya udaktari haijitoshelezi yenyewe na kuna mambo mengi unafundishwa juu juu ni tofauti kabisa na stashahada ya udaktari hivyo hili swala sio la siasa wala nini miaka ibakie vile vile mitano isipunguzwe wala nini
 
Alafu eti mhitimu wa Cheti cha Utabibu anaitwa jina moja la CO (Clinical Officer) yaani Tabibu sawa na mhitimu wa Stashahada ya Utabibu! Ina maana mtaala wa Cheti cha Utabibu na mtaala wa Stashahada ya Utabibu vinalingana kwenye maudhui? Cheti na Stashahada vina hadhi sawa? Baghosha Tz!

Wabunge mliwashe kieleweke.
Na CA ni akina nani mkuu? Uko kwenye medical Field hujui hata Vyeo vyenu vikoje wewe usome miaka mi5 tu hata wakisikiliza malalamiko yako mkuu wangu
 
Elimu inayoeleweka duniani ni katika mpangilio huu : kutoka primary kwenda secondary kwenda high school au advanced na kwenda chuo kikuu.

Mfumo wa kupitia astashahada( certificate) au stashahada( diploma) ni mfumo ulioandaliwa kwa ajili ya wale walioshindwa kuendana na mfumo wa kawaida na aghalabu wanakuwa wamefeli.

Kutokea kidato Cha sita au high school ni mfumo unatambulika dunia nzima kumuanda mwanafunzi kwa masomo ya chuo kikuu. Mwanafunzi aliyetoka advance na kwenda chuo anakuwa competent sana na mwenye uwezo na uelewa mkubwa sana darasani kutokana na kwamba masomo ya advance yanamuandaa mtu kukabiliana na mfumo wa masomo ya Elimu ya juu.
Mkuu hapa umetudanganya,si kila nchi wana mtaala wa kusoma form 1 hadi form 6 mbona Kenya sekondari wanasoma hadi form 4 kisha wanaingia chuo kikuu so unataka kusema wakiingia chuo hawapati competency inayotakiwa kidunia?
 
Mwenye cheti cha utabibu anaitwa assistant clinical officer
Mwenye diploma ya utabibu anaitwa clinical officer.
Utendaji kazi ni ule ule hauna tofauti yoyote tofauti ipo katika vyeo tu
Clinical Officer na Clinical Assistant zamani Medical Assistant na Rural Medical Assistant.
 
😂😂😂😂😂😂imbombo ngafu; Diploma wanataka kupangua meza. Diploma ninyi mpo NACTE huko mnasheria zenu na sisi tupo TCU tunasheria zetu.

Ni huruma tu; hamkutakiwa hata kujiunga degree; mlitakiwa msome Advanced Diploma.
 
Mkuu hujanishawishi.

Unamaanisha kidato cha 6 bila Diploma ya Utabibu yuko sawa na kidato cha 6 mwenye Diploma ya Utabibu?

Je, kidato cha 6 bila Diploma ya Utabibu anajuwa yafuatayo?

1. Pharmacology.
2. Surgery.
3. Anatomy and Physiology.
4. Medical Psychology.
5. Lab Technics.
6. Pathology (Bacteriology & Virology).

.
Basic science ya clinical officer iko too shallow so refer Anatomy and physiology ya Ross and Wilson ( ni kama introduction tu) pathology ndio kabisaa hamna kitu.


Unasoma miaka 2 basic science upya then miaka 3 ndio unasoma medicine.


Sasa huwezi kutoka na basic science ya CO ukapewe medicine ya kikubwa.
 
Back
Top Bottom