Mtaala wa Udaktari Udurusiwe

Mtaala wa Udaktari Udurusiwe

Tunataka wana taaluma mahiri, sio wa ujanja au kudandia. Si udaktari tu, nenda vyuo vya ufundi, ufamasia nk. huwezi punguzo miaka ya kusomea shahada ya uhandisi kwa mwanafunzi kisa kasomea sekondari za ufundi na vyeti vya ufundi .
 
haya mambo hayaishagi sijui kwanni CO vs MD kila mtu ale ugali wake kwa macho yangu nimeshuudia MD akizidiwa mshaara na CO SIkujua kwa nni ila niliamua kupita iv
 
Astashahada siyo cheti, ni vitu viwili tofauti. Iko hivi:-

1. Cheti ni Certificate.

2. Stashahada ni Diploma.

3. Astashahada ni Advanced Diploma (imefutwa Tz. Kuna mtu aliipachika tu kwa maslahi yake)

4. Stashahada ya Uzamili ni Postgraduate Diploma.

5. Shahada ni Degree.

6. Shahada ya Uzamili ni Masters Degree.

7. Shahada ya Uzamivu ni PhD.
Mwamba wewe ni MUHA au mkurya una ubishi usio na maana kabisa hata pale unaposahihishwa

Hiyo Astashahada maana ake nini!?
 
Hapo kwenye Co wanatakiwa wapunguziwe miaka kwasababu wanakuwa Wana uzoefu na wamejitunza mengi Yale ya MD ISIPOKUWA UPASUAJI MKUBWA TU ILA MAGONJWA AU DIAGNOSIS hazibadiliki ila treatment Zina change kutokana na updates ambazo wote watazosoma Kwa guidelines
Unachekesha ujue... ukitaka kujua utofauti uliopo Tafuta Dr aliyesoma CO then MD .. mwenyewe atakuambia shule ya CO ni ndooogo sana sana hata Anatomy anaanza upya kabisa... achilia mbali physiology na mnyama pathology.

No offense CO inatakiwa ifutwe au iwe foundation course ili waje kusoma medicine.
 
Hizo dose unatakiwa uwe nazo kichwani. Ndio maana ukasoma miaka Sita.

+ Uzoefu

+ Unajisomea kila unapopata muda.
unajua chochote kuhusu journals,, au medical search engines.... kuna daily updates na miongozo ... watu wana reseach muda wote na ku-publish ...

So mnapenda sana wale wazee wa Zamani ambao kwenye kabati ana Quinene, GV , pcm na amoxcillin.. baasi anaandika tuu kulingana na alizonazo baasi unaamuona kichwa sana.

Mabadiliko ya kisayansi na technology yanasogeza information karibu yako na unatakiwa ufanye proper refferencing .

NB.. hii mnayoita kugoogle Dr hatumii search engine kama wikpedia ... kuna reliable source ambazo anakuwa registered eg UPToDATE, Med scape etc
 
H
Mkuu hujanishawishi.

Unamaanisha kidato cha 6 bila Diploma ya Utabibu yuko sawa na kidato cha 6 mwenye Diploma ya Utabibu?

Je, kidato cha 6 bila Diploma ya Utabibu anajuwa yafuatayo?

1. Pharmacology.
2. Surgery.
3. Anatomy and Physiology.
4. Medical Psychology.
5. Lab Technics.
6. Pathology (Bacteriology & Virology).

Hapo 1- 6 namaanisha je, mhitimu wa kidato cha 6 anajuwa kuandika dawa? Je, anajuwa upasuaji mdogo? Je, anajuwa kusoma ripoti za Maabara? Je, anajuwa kushona nyuzi? Je, anajuwa kudunga sindano? Je, anajuwa kuzalisha mjamzito? Je, anajuwa kuweka dripu?

Wenye Diploma ya Utabibu wakienda Digrii ya Udaktari wapunguziwe miaka ya kozi.
Hata wewe hujui viti vingi alivyopitia advance.. kuwa mpole. Hta hivyo ninyi ndo wenye favour kubwa kuliko hata hao form six..
 
Mkuu hapa umetudanganya,si kila nchi wana mtaala wa kusoma form 1 hadi form 6 mbona Kenya sekondari wanasoma hadi form 4 kisha wanaingia chuo kikuu so unataka kusema wakiingia chuo hawapati competency inayotakiwa kidunia?
Kaa ujue wanaoenda chuo kikuu Kwa kenya ni wale waliopata ufaulu wa juu sana.. wengine huwa wanajoin vyuo vya kati Halfu chuo kikuu baadaye
 
M
Inategemea unatafuta nini huko mtandaoni kama unatafuta Guidelines za WHO au MoH, CDC sawa.
Ila haitopendeza ufanye mbele ya mgonjwa, lazima atapata mashaka.

Na tena ukiwa ni kijana. Hakuna imani kabisa.
Madr wa siku Hizi Hasa hawa vijana wanakaa na vitabu vyao kabsa na wanatafuta wakuandikie sawa ipi mbele Yako mgonjwa... Lkn nadhan miongozo inaruhusu
 
Mkuu hujanishawishi.

Unamaanisha kidato cha 6 bila Diploma ya Utabibu yuko sawa na kidato cha 6 mwenye Diploma ya Utabibu?

Je, kidato cha 6 bila Diploma ya Utabibu anajuwa yafuatayo?

1. Pharmacology.
2. Surgery.
3. Anatomy and Physiology.
4. Medical Psychology.
5. Lab Technics.
6. Pathology (Bacteriology & Virology).

Hapo 1- 6 namaanisha je, mhitimu wa kidato cha 6 anajuwa kuandika dawa? Je, anajuwa upasuaji mdogo? Je, anajuwa kusoma ripoti za Maabara? Je, anajuwa kushona nyuzi? Je, anajuwa kudunga sindano? Je, anajuwa kuzalisha mjamzito? Je, anajuwa kuweka dripu?

Wenye Diploma ya Utabibu wakienda Digrii ya Udaktari wapunguziwe miaka ya kozi.
Ni kweli wa kidato cha sita hana ujuzi wala uzoefu sawa wa aliyekuwa chuoni.
Ila wanapofanya shahada, hata waliopitia chuo, wasome miaka sawa ili na waliotoka kidato cha sita, itasaidia kuwafunda zaidi kwani taasisi za elimu ni tofauti na hata vifaa na ufundishaji ni tofauti.
 
Tujadiliane.

Mhitimu wa Stashahada ya Utabibu (miaka 2) na pengine aliye na uzoefu wa kazi, kwanini akienda kusoma Udaktari kamili (ngazi ya Shahada) asipunguziwe miaka ya masomo toka 5 kurudi chini?

Anapolazimika kusoma miaka 5 sawa na mhitimu wa kidato cha 6 ina maana mtaala wa kidato cha 6 ndiyo huo huo mtaala wa Stashahada ya Utabibu?

Je, kidato cha 6 yuko sawa na mwenye Stashahada ya Utabibu kwamba wote hao wawili wasome miaka na mtaala unaofanana wa Shahada ya Udaktari chuo kikuu?

Aidha, kwanini mhitimu wa Cheti cha Utabibu anaitwa jina moja la CO (Clinical Officer) yaani Tabibu sawa na mhitimu wa Stashahada? Ina maana mtaala wa Cheti cha Utabibu na mtaala wa Stashahada ya Utabibu vinalingana kwenye maudhui? Cheti na Stashahada vina hadhi sawa?

Wabunge mlione hili kwa jicho la 3.
Mbunge kama msukuma kibajaji na wengine unategemea wakutete wewe msomi
Wakati hawajui kitu
Wao wapo pale kutetea biashara zao tuu

Baraza na chama chenu kazi yake ni nn??
 
Mwamba wewe ni MUHA au mkurya una ubishi usio na maana kabisa hata pale unaposahihishwa

Hiyo Astashahada maana ake nini!?
Wewe fundi gereji ya kirikuu utashindana na HR wapi na wapi?[emoji38][emoji16][emoji23][emoji851]
 
Kumbe walifeli matriculation, ndo ujue walifeli.

Sasa unakataa nn, khaaaaah [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Baghosha!

Siyo wewe ulibisha kwamba Form Six aliyefaulu hawezi kusoma Diploma!!!???

Nimeamini 100% wewe ni mwezi mchanga! [emoji38][emoji16][emoji441][emoji344]
 
Baghosha!

Siyo wewe ulibisha kwamba Form Six aliyefaulu hawezi kusoma Diploma!!!???

Nimeamini 100% wewe ni mwezi mchanga! [emoji38][emoji16][emoji441][emoji344]
Unajua unacho kiandika lakini? Umesema alifaulu ila matriculation alifeli, means angefaulu asingeenda diploma.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] poleeee baba, miaka ya degree iko pale pale na haibadiliki, lia na utoe chozi, ukichoka kunywa maji mengi na upumzike.
 
Alafu eti mhitimu wa Cheti cha Utabibu anaitwa jina moja la CO (Clinical Officer) yaani Tabibu sawa na mhitimu wa Stashahada ya Utabibu! Ina maana mtaala wa Cheti cha Utabibu na mtaala wa Stashahada ya Utabibu vinalingana kwenye maudhui? Cheti na Stashahada vina hadhi sawa? Baghosha Tz!

Wabunge mliwashe kieleweke.
Cheti Cha utabibu= C.A. (Tabibu msaidizi)
Stashahada=C.O (Tabibu)
 
India kuwa daktari bingwa unaanzia umri wa miaka 21 minimum.
Si kweli.
System ya elimu ya tanzania na India hazijatofautiana sana.
Kindergarten 2 years
Primary education 7 years(lower primary 5yrs, upper primary 2 years)
Secondary education 3 years
Higher secondary 2 years
After that, mtu aende medical school 5 years
Internship 1 year
Then aende akasomee ubingwa ambao minimum ni 3 years...
Anatokea wapi daktari bingwa wa below 21 years hapo 🤣🤣
 
Astashahada siyo cheti, ni vitu viwili tofauti. Iko hivi:-

1. Cheti ni Certificate.

2. Stashahada ni Diploma.

3. Astashahada ni Advanced Diploma (imefutwa Tz. Kuna mtu aliipachika tu kwa maslahi yake)

4. Stashahada ya Uzamili ni Postgraduate Diploma.

5. Shahada ni Degree.

6. Shahada ya Uzamili ni Masters Degree.

7. Shahada ya Uzamivu ni PhD.
Acha UONGO, kwamba kiswahili kingine chá cheti ni certificate?[emoji1][emoji1][emoji1]
Astashahada ndio cheti
Stashahada ni diplôme
Shahada ni degree
Shahada ya uzamili ni masters
Shahada ya uzamivu ndio PhD
 
Back
Top Bottom