Pamoja sana mkuu. Nimekuwa nikipitia shombo za watu wengi mitandaoni wakimbeza Harmonize kwa alichokifanya. Ila nimegundua wengi hawajui uhalisia wa kile alichokifanya "Konde boy".
"Konde boy" alijirisk sana, na nampa hongera alifanikiwa kwa kiwango kikubwa. Humu ndani kwenyewe(kwa watu wa medani) kile kitu hufanywa na watu wachache sana tena ambao hufanya mazoezi ya kuridhisha kabla ya tukio/ushereheshaji husika. Isipokuwa wale jamaa zangu wa unit 92, wale ni maisha yao hayo mavurugu ni kuwashtua tu wanafanya na inaisha kibabe, Maana pale hizo mambo ni kama salamu tu, shikamoo....marhaba!
Konde asibezwe, amejitahidi sana. Hongera kwake.