GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Kasema yafuatayo:
1. Wanayanga wote watakaoenda Uwanjani wahakikishe wameshandika ' Urithi ' kwa Watoto na Wake zao.
2. Wanasimba wote wahakikishe wanavalia tu Nguo Nyekundu na asibakie Mtu Nyumbani ili Uwanja ujae.
3. Kikosi cha Simba SC kiwe hivi...Aishi Manula, Nicolas Gyan, Asante Kwasi, Pascal Serge Wawa, Juuko Murshid, James Kotei, Jonas Mkude, Clatous Chota Chama, Mohamed Kagere, John Boko na Emanuel Okwi.
4. Yanga SC wakimpanga Golini Ramadhani Kabwili watafungwa Goli Saba ( 7 ) kwa Sifuri ( 0 ) ila wakimpanga Klaus Kindoki watafungwa Goli Tano ( 5 ) kwa Sifuri ( 0 ) hivyo maamuzi wanayo Wao.
5. Kuna Fujo Kubwa itatokea kati ya dakika 15 za mwisho za Kipindi cha Kwanza au dakika 15 za Kwanza za Kipindi cha Pili.
6. Kuna Kadi Nyekundu mbili moja kwa Yanga SC na moja kwa Simba SC.
7. Mchezaji wa Yanga SC Nahodha Ibrahim Ajib asikubali kubebeshwa Hirizi Siku hiyo kwani Mchezaji wa Simba SC ( jina nalihifadhi ) ambaye ndiyo atabeba Hirizi ana Nyota Kali na Hirizi yake hiyo ina nguvu hivyo Ajib anaweza kupatwa na ' Majanga ' makubwa na hata Klabuni Yanga wakatangaza Msiba mzito na wakamzika Kijana wa Watu.
8. Kuna Goli litafungwa ila litakataliwa japo halitakuwa lina makosa ila kwa aina ya Uchawi ambao Timu hizi mbili itatumia Siku hiyo Mwamuzi ( Referee ) atakuwa anajichanganya mara kwa mara kwakuwa ' Majini ' yatakuwa yanamtesa.
9. Wachezaji wa Simba SC wakiwa wanaenda Kufanya ' Warm Up ' yao kila mmoja ahakikishe amebeba ama Ndimu au Limao na wakikosa hiyo basi wabebe Chumvi Viganjani mwao na wakiingia katika ' pitch ' watupe ili Kuua ' Uchawi ' mkali wa Yanga SC ambao wataufanya Kesho Usiku Uwanja wa Taifa au Kwa Mkapa badala ya Kukatazwa sasa Kuita kwa Mchina.
10. Nahodha wa Simba SC ahakikishe anachagua kuanzia Goli la Kusini ili baadae wamalizie Goli la Kaskazini ambapo ' Kinyota ' ndilo lina ' Magoli ' mengi sana Siku hiyo.
11. Kuna tukio la Kuhuzunisha linaweza ( narudia tena kusema ) linaweza kutokea la Mtu mmoja maarufu wa hizi Timu mbili Kupoteza Maisha / Uhai ( namaanisha Kufa ) ama Kesho Ijumaa au Siku ya mechi au baada ya Mechi kwani ' Kafara ' linalotumika sasa na Timu zote mbili ni la Kuua.
12. Simba SC hasa Wachezaji watakaonza kama wataweza wawapitishie katika moja ya Mageti ya kilipo Chuo cha DUCE na wasiingilie Mlango mkubwa kwakuwa Yanga SC safari hii nao wameamua Kufanya Ulozi / Uchawi wa hatari sana ila watazidiwa kidogo na wa Simba SC kwakuwa Simba SC wanachanganya wa Kitabu na Mizizi bila kusahau Kafara.
13. Wakati Timu zikisalimiana Wachezaji wa Simba SC wahakikishe hawazungukwi na wa Yanga SC na pale wakishasalimiana nao tu kila mmoja atawanyike ili kuzuia wasizungukwe na hatimaye Kufungwa Kiuchawi / Kindumba.
14. Yanga SC kama wanaweza kuanzia Usiku huu huu GENTAMYCINE natiririka na naserereka hapa na huu ' Uzi ' wamtafute haraka Kipa Ben Kakolanya wamuombe radhi na ikibidi Kuanzia Viongozi wa Yanga SC wote hadi Kocha wao wampigie Magoti na wamlambe si tu Miguu bali hadi Unyayo ili wamuombe adake Yeye ambapo kwa Nyota yake Kali Yanga SC anaweza akatoka Sare au akabahatisha Ushindi ili akipangwa Kabwili wanakula / wanafungwa Goli 7 bila na akipangwa Kindoki wanakula / wanafungwa Goli 5 bila.
Na ni matumaini yangu makubwa kuwa mpaka muda huu Wanasimba wote mmeshaandaa Pesa zenu ili Kesho muwahi Kununua Tiketi zenu na hakikisheni mnaujaza Uwanja ' Kwa Mkapa ' hadi pomoni ( kuzidi Kiwango ) na hakikisheni Nguo zenu ziwe ni Nyekundu tupu tafadhali ili ' Majini ' yetu ya Ushindi yafurahi.
Wana Simba SC wote popote pale mlipo tembeeni Kifua mbele Kazi imekwisha na huko Jangwani watatafutana na tegemeeni ' Mgogoro ' mkubwa sana Jangwani baada ya Kufungwa na Simba SC hizo Goli 7 au 5 kwa Bila / Sifuri hiyo Jumamosi ya tarehe 16, February 2019.
Nawasilisha.