Mtaalamu wa Dawa na Tiba: Ninakaribisha maswali kuhusu Magonjwa, Tiba na Dawa

mkuu nasumbuliwaa na meno sana tena sana, nimeng"oa meno matano lkn bado mawili yametoboka na yanaumwa sana, please nisaidie

Mkuu ushauri wangu ni hivi:
1. Tafadhali kamuone daktari wa meno ili akuambie kinachohitajika kufanya. kwa mfano kuziba hizo nafasi.
2. Piga mswaki na dawa ya meno nzuri kama colgate kila siku mara mbili, asubuhi na usiku.
3. Tumia Listerine mouth wash baada ya kupiga mswaki
4. usile chakula yeyote baada ya kupiga mswaki
5. Mpaka utakapo muona daktari wa meno, unaweza kupakaa Quadrajel cream na kutumi ibuprofen kidonge kimoja ili kupunguza maumivu.

Asante.
 
Docter huwa naumwa sana na tumbo cku za period na cku zng kubadilika ttzo nini? Pia nna ttzo la allergy ya dawa km declofanic bruphen etc naomba dawa itakayonisaidia kupunguza makali ya tumbo ambayo si NONSAID

Dada, kawaida NSAID ndiyo inatumika kupunguza maumivu. Lakini pia ni muhimu kujuwa kwamba hiyo maumivu ni ya kawaida au linatokea kwasababu ya tatizo. Ushauri wangu ni ukamuone Gynecologist akupime na akupe ushauri.
 
Dr ni nini dawa ya kufany "anal sphinter" ziweze kurelax?? kufunguka muda unapohitajika
Dr ni nini dawa ya kufany "anal sphinter" ziweze kurelax?? kufunguka muda unapohitajika
Kwani shida ni nini ?
 

Ushauri wangu ni hivi:
1. Ni vizuri ukamuone gynecologist kujuwa kwamba kuna tatizo au ni maumivu la kawaida.
2. Dawa hii inasaidia sana kupunguza maumivu. Unaweza kuitumia wakati unaona maumivu. Flammar-Mx, kidonge kimoja.

Asante.
 

Mkuu dalili zako zinaweza kuwa mambo mengi.
Tafadhali nenda kituo cha afya na fanya vipimo hizi:
1. RBG, HbA1c, ECG, ECHO.
 
Asante Doctor.Mimi napenda kuuliza tatizo la kutoa makohozi kooni na mishipa ya shingo kuuma baadhi ya muda husababishwa na nini hasa? Tatizo hili halisababishi maumivu yoyote wakati wa kula chakula.

Yaonyesha una infection ya koo. Tumia Amoxiclav 625mg kutwa mara mbili kwa muda wa siku 7.
Pia kwa siku chache kunywa maji ya kawaida na siyo ya baridi.
Asante.
 

Ndiyo ugonjwa wa migraine unatibika. Ni kweli inatokea kwamba tatizo la macho husababisha maumivu ya kichwa. Kama hiyo ndiyo shida kachekishe macho alafu niambie ripoti ya vipimo vya macho.
 
Dr Naomba majibu ya swali langu la mtoto wa miaka minne kushindwa kuongea plz

Mkuu tatizo hiyo inaweza kuwa anatomical. Siwezi kutoa ushauri juu ya hilo mpaka nimuone huyo mtoto.

Ushauri wangu ni umuone daktati binwa wa watoto ndiyo amuone mtoto wako na akupe ushauri bora.
 
Tatizo la hormone imbalance kwa mwanamke nini tiba yake!? Estrogen ikiwa juu kuliko postrogene
 

Asante kwa furaha yako mkuu. Kwa tatizo hilo la Tinnitus, ushauri wangu ni yafuatayo:
1. Safisha sikio na ondoa uchafu yeyote ndani ya sikio.
2. Inaweza kuwa unachukua dawa inayosababisha hiyo tatizo.
3. Kuna watu wengine sauti ya pangaboi na A/C inasaidia kupunguza sauti ya Tinnitus.
4. Kwa kupunguza pombe, eneo yenye sauti nyingi na mawazo (stress) itasaidia kupunguza sauti.
5. Tafadhali chukua multivitamins yenye Zinc kama Zincovit, kidonge kimoja kila siku kwa muda wa miezi moja.
 
daahh neno moja la kumaanisha mwezi mchanga mkuu cjalijua ila kwa ninavyoelewa
mwezi mchanga-mtu huwa anachanganyikiwa(anakuwa chizi) kwa kipindi flan kila mwaka ila kuna kipindi anakuwa sawa na mzima kabisa

Samahani sijawahi kusikia tatizo hilo mkuu, Na mpaka nipate kingereza chake itakuwa ngumu. Lakini kama ni tatizo la kuwa chizi unaweza kumpeleka huyo mgonjwa kwa madaktari bongwa wa akili; Psychiatrist. Asante.
 
Dokta naomba kuuliza naweza kutumia dawa gani ya kurekebisha homoni,maana tatizo langu maziwa yanatoka kama na nyonyesha au mjamzito ila sio mengi nimeenda hospital nimepata tiba ila bado naona tatizo lipo nikitumia dawa zinanisaidia kwa muda ule ninaotumia baadae tatizo naliona mara ya mwisho hospital nilipewa dawa aina ya Bromocriptine naomba unisaidie kwa Ilo nitumie dawa gani kuondoa tatizo kabisa.
 
Dokta nina tatizo la kutokwa na damu puani hasa kipindi cha joto. Tangia utotoni mpaka saiv. Sijui ni tatizo gani hilo

Mkuu, hiyo tatizo inasababishwa na magonjwa mengine. Kwa kawaida tatizo hiyo haitakiwi kutokea mara kwa mara. Tafadhali fika kituo cha afya ili daktari akuone na akupime pia.
 

Huwa watu wanapew Horomonal Replacement Therapy kwa kuchukuwa Estrogen au Progesterone. Hiyo itabidi ufike kituo cha afya.
 

Mkuu, tatizo lako linarudia mara kwa mara. Hii itakua tatizo kubwa zaidi, Naona hii ni tatizo ya korodani na siyo infection pekee. Tafadhali kamuone daktari wa "General Surgery". Hawa ni daktari bingwa na watakusaidia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…