Dr. Sajjad Fazel
JF-Expert Member
- Jan 7, 2014
- 435
- 428
- Thread starter
-
- #421
Dr nina tatizo la kuwashwa baada kutoka kuoga hasa nyakati za mchana au jioni. Nikioga asubuhi sana kuwashwa kunakuwa hakupo. Je tatizo ni nini hasa? Dawa ni nini? Kuwashwa huku hutokea sehemu mbali mbali mwilini kama miguuni, kwenye mapaja, mikono, mgongoni na tumboni. Na hudumu kwa dakika 3 mpaka kumi.
Ahsante sana doktaHuwa watu wanapew Horomonal Replacement Therapy kwa kuchukuwa Estrogen au Progesterone. Hiyo itabidi ufike kituo cha afya.
Dawa za kwanza kabisa ni Salbutamol Inhaler na Ipratropium Bromide inhaler.nahitaji kujua dawa ya kutibu pumu
dokta samahani mm nasumbuliwa na tatizo la kulegea mishipa ya uume, mpaka inapelekea uume kutosimama vzur wakat Wa tendo la ndoa,, naomba ushauri Wa dawa gani nitumie ambayo haitaleta madhara huko mbeleni, na naweza kuipata wapi?
Ukiambiwa INI linafanya Kazi kuliko uwezo wake nini inasababisha
Huu ni ugonjwa gani?
Unapolala na mwenzi wako mnasex baada ya muda mfupi unasikia maumivu makali kwenye njia ya mkojo na kuanza kuona usaha, maana najua kama ni gono ukimaliza kusex utakaa muda ata siku moja kuona dalili..
Limeanza kama miezi 4 baada ya kujifungua.
Dr nina mtoto ana miaka 4 kufikia mwezi Novemba mwaka huu. tatizo lake hasemi mpaka sasa, ni mara chache anaweza kusema baba au mama basi, anasikia vizuri, Nilimpeleka muhimbili Dr kasema tumpeleke shule ya awali ajichanganye na wenzake na kwamba hana tatizo lolote la kumzuia asiongee. nimempeleka shule huu ni mwezi wa sita sasa bado hasemi na kule shule anaendelea kwenda Naomba msaada Dr. kwa mawasiliano 0715586022
Dawa inayoweza kutibu taifodi inayojirudia mara kwa mara mkuu. Tunazingati taratibu kadha ikiwemo kuchemsha maji ya kunywa, kuosha mayunda kabla ya kuyala, kutokula mbagamboga mbichi kama kachumbari nk.
Yani nilifanya vipimo nilikua na maumivu tumboni upande Wa kulia nikaambiwa ini linafanya Kazi kuliko uwezo wakakosa nini inasababisha
Mtu mwenye matatizo ya kutupa miguu atembei kama kawaida dawa yake nini
Nnatatizo la kupooza mkono mmoja either wa kulia au kushoto nyakati za usiku wa manane, nnashtuka nakuta umepooza na hauwezi fanya chochote. Nnaupikicha alafu baada kama ya dakika 5 unarudi hali ya kawaida na unakua mzima kabisa. Inatokea mara moja moja sio siku zote, ngependa kujua tatzo ni nini tafadhari
Dr ninatatizo la maumivu sehemu za mgongoni hadi juu kwenye mabega tatizo hili lina kama miezi mitatu bila kupungua mwanzo nilijua maumivu tu ya kawaida tu......Je inaweza kuwa tatizo ganj au dawa gani zinaweza kuwa suluhisho dr