Mtaalamu wa Dawa na Tiba: Ninakaribisha maswali kuhusu Magonjwa, Tiba na Dawa

Mtaalamu wa Dawa na Tiba: Ninakaribisha maswali kuhusu Magonjwa, Tiba na Dawa

Dr nina tatizo la kuwashwa baada kutoka kuoga hasa nyakati za mchana au jioni. Nikioga asubuhi sana kuwashwa kunakuwa hakupo. Je tatizo ni nini hasa? Dawa ni nini? Kuwashwa huku hutokea sehemu mbali mbali mwilini kama miguuni, kwenye mapaja, mikono, mgongoni na tumboni. Na hudumu kwa dakika 3 mpaka kumi.

Tumia Fexofenadine 60mg kidonge kimoja kila siku kwa muda wa wiki mbili alafu nipe mrejesho
 
dokta samahani mm nasumbuliwa na tatizo la kulegea mishipa ya uume, mpaka inapelekea uume kutosimama vzur wakat Wa tendo la ndoa,, naomba ushauri Wa dawa gani nitumie ambayo haitaleta madhara huko mbeleni, na naweza kuipata wapi?

Saa moja Kabla kitendo unaweza kutumia sildenafil 50mg kidonge kimoja, unaipata duka la dawa yeyote.
 
Huu ni ugonjwa gani?

Unapolala na mwenzi wako mnasex baada ya muda mfupi unasikia maumivu makali kwenye njia ya mkojo na kuanza kuona usaha, maana najua kama ni gono ukimaliza kusex utakaa muda ata siku moja kuona dalili..

Umepata infection ya eneo hilo. Tumia dawa hizi:
1. Ciprofloxacin 500mg kidonge kimoja.
2. Doxycycline 100mg, kidonge kimoja kutwa mara mbili kwa siku saba.
3. Metronidazole 400mg kidonge kimoja kutwa mara tatu kwa siku saba.
 
Dawa inayoweza kutibu taifodi inayojirudia mara kwa mara mkuu. Tunazingati taratibu kadha ikiwemo kuchemsha maji ya kunywa, kuosha mayunda kabla ya kuyala, kutokula mbagamboga mbichi kama kachumbari nk.
 
Dr nina mtoto ana miaka 4 kufikia mwezi Novemba mwaka huu. tatizo lake hasemi mpaka sasa, ni mara chache anaweza kusema baba au mama basi, anasikia vizuri, Nilimpeleka muhimbili Dr kasema tumpeleke shule ya awali ajichanganye na wenzake na kwamba hana tatizo lolote la kumzuia asiongee. nimempeleka shule huu ni mwezi wa sita sasa bado hasemi na kule shule anaendelea kwenda Naomba msaada Dr. kwa mawasiliano 0715586022

Mkuu, kamuone daktari bingwa wa watoto.
 
Dawa inayoweza kutibu taifodi inayojirudia mara kwa mara mkuu. Tunazingati taratibu kadha ikiwemo kuchemsha maji ya kunywa, kuosha mayunda kabla ya kuyala, kutokula mbagamboga mbichi kama kachumbari nk.

Mpaka sasa hivi umetumia dawa gani ya typhoid?
 
Yani nilifanya vipimo nilikua na maumivu tumboni upande Wa kulia nikaambiwa ini linafanya Kazi kuliko uwezo wakakosa nini inasababisha

Yaani ukisema inafanyakazi kuliko uwezo. Ukimaanisha kama nguvu yake imepungua kuna tatizo nyingi. Pombe inasababisha hilo, Hepatitis pia inasababisha hilo. La kwanza punguza kula nyama. La pili, kafanye vipimo vya ini (ALT, AST, ALP, PT/INR, Albumin, Billirubin) na Hepatitis.
 
Kwa kweli kuzitaja kwa majina ni ngumu kidogo kwa utamaduni wa Watanzania wengi ila nimeshatumia dawa nyingi sana za kitaalama (vidonge) hata nimechoka, leo nina siku ya tatu natumia dawa za asili masna huko phamacy pamenichosha. Nikujikadiria kwa mwaka naweza kutumia dozi 4 hadi 5.
 
Dr ninatatizo la maumivu sehemu za mgongoni hadi juu kwenye mabega tatizo hili lina kama miezi mitatu bila kupungua mwanzo nilijua maumivu tu ya kawaida tu......Je inaweza kuwa tatizo ganj au dawa gani zinaweza kuwa suluhisho dr
 
Nnatatizo la kupooza mkono mmoja either wa kulia au kushoto nyakati za usiku wa manane, nnashtuka nakuta umepooza na hauwezi fanya chochote. Nnaupikicha alafu baada kama ya dakika 5 unarudi hali ya kawaida na unakua mzima kabisa. Inatokea mara moja moja sio siku zote, ngependa kujua tatzo ni nini tafadhari

Tumia dawa hii:
Neuroton, kidonge kimoja kila siku kwa muda wa miezi moja. alafu nipe mrejesho.
 
Dr ninatatizo la maumivu sehemu za mgongoni hadi juu kwenye mabega tatizo hili lina kama miezi mitatu bila kupungua mwanzo nilijua maumivu tu ya kawaida tu......Je inaweza kuwa tatizo ganj au dawa gani zinaweza kuwa suluhisho dr

unatumia dawa gani kwaajili ya maumivu hayo ya mgongo na mabega?
 
Back
Top Bottom