Mtaalamu wa Dawa na Tiba: Ninakaribisha maswali kuhusu Magonjwa, Tiba na Dawa

CLOBEN-G ndiyo dawa walinipa ya kupaka nilipewaTube 1 na niliitumia mpaka nikaimaliza lakini vipele havijaisha

Tumia tube ya Trioderm, pakaa mara mbili kila siku kwa siku kumi alafu nipe mrejesho.
 
Zipo usoni ni ndogo ndogo, na aina ya ngozi yangu ni kavu kiasi,

Mkuu, Tumia Retin-A (Retinoid) Cream. Pakaa usoni baada ya kuoga kila siku mara moja kwa muda wa wiki mbili alafu nipe mrejesho. Asante.
 
Dawa ya Malaria Sugu dr.

Artesunate na Dihydroartemisinin-piperaquine ni dawa nzuri za malaria. Lakini unaweza kuchukua dawa ili usipate malaria. Tumia Doxycycline 100mg kila siku kwa muda wa miezi moja.
 
Niambie nikusaidiaje mkuu?
Dr kwanza nakupa hongera kwa moyo wako huo wa kujitolea..,
Baada ya pongezi hzo naomba unisaidie tatizo langu, nina binti yangu wa kazi anawashwa kwenye vidole na pia ngozi inababuka, baada ya check up hospital wakasema ni fungus, akapewa dawa ya kupaka, akachomwa sindano ya power safe na vidonge vya Fluconazole kwa siku 7, baada ya kutumia hali ikapungua kdogo then ikarejea, nlipompeleka tena akapewa canditra vidonge kwa siku 7, amemaliza leo anasema ameanza kuwashwa, je nimpatie dawa gan tena??
 
Hongera kwa kazi nzuri Dr;
Ninachangamoto katika mguu wangu nikiwa nimekaa kwa muda au nikitoka kuamka huwa nikikanyaga chini unauma hivyo wanilazimu kuchechemea kwa muda kisha ukishachanganya ndio natembea na kukanyaga chini kama kawaida. Je tatizo laweza kuwa nini?!
 
Dr Mimi kuna siku nilikuwa nasafisha sikio la kulia na kijiti baadae nikahisi nguvu ya usikivu kwa hili sikio imepungua sana sana sana naona sikio la kushoto ndio linasikia vizuri je kuna uwezekano kuwa nilipasua ngoma ya sikio?
 
habari yako doctor, ninatatizo la kukosa balance, kushikwa ganzi miguuni na miguu kuishiwa nguvu. yote haya yametokana na maumivu ninayopata eneo la chini ya mgongo (lower back). ilianza mwaka jana then ikapotea yenyewe, ila mwaka huu imekuja speed sana na hali yangu imekua mbaya mpaka nashindwa kutembea. mwaka jana nilipiga x-ray ila haikuonyesha tatizo lolote kwenye mgongo. tafadhali naomba msaada juu ya tatizo hili. thanks in advance!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…